Uchaguzi 2020 Lipumba, Shibuda kutumika kumdhibiti Lissu asigombee Urais?

Uchaguzi 2020 Lipumba, Shibuda kutumika kumdhibiti Lissu asigombee Urais?

haka kanatakiwa kaitwe kauchaguzi maaana mshindi haihitaji ata kampeni
 
Safi sana Prof Lipumba na Shibuda tunawaaminia, na vyama vingine vitakuwa nyuma yenu.Kataeni huyo kibaraka wa ubeligiji
 
Tume muwe makini msije tuletea machafuko Tundu lissu mpitisheni wakapambane uwanjani
Kavunja kanuni. Unampitishaje? Mwanasheria mzima kanuni hazijui. Kati ya wagombea wote zaidi ya kumi, umemuona nani anatafita wadhamini kwa mikutano na hotuba
 
yaan popote alipo jiwe lazima paharibike jambo..kule chamani amefanikiwa kuwakata akina membe ili agombee peke yake huku nako anataka apite kwa kukata watu..hivi huyu mzee ana matatizo gani aache upuuzi..
 
Science gani wakati tume mmeiagiza kuja na idadi ya kubumba ya wapiga kura? Watanzania tunakaribia 60m, huku idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa tume ni 29m+. Inawezekana vipi nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kupiga kura? Na ni kweli kuwa watu wenye miaka 18+ ni nusu sawa ya walio chini ya miaka hiyo? Kama sio Magufuli na ccm wamejiandaa kutangaza matokeo ya uongo, na kuuingiza nchi hii kwenye umwagaji wa damu ni nini zaidi?
Mshaanza kulalamika na wapiga kura tena...
 
Mbio za kuwania urais wa Tanzania kwa Tundu Lissu, huenda zikafikia ukingoni siku chache baada ya kukabidhi fomu zake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Lissu alipitishwa na chama chake, CHADEMA kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi wa mwaka huu, 2020 uliopangwa kufanyika Oktoba 28.

Read more > Urais 2020: Lissu kuwekewa vikwazo kimkakati - Imevuja!
CHADEMA SI MNAJIFANYA WANAUME NYIE? MBONA KULIA LIA HIVO? TUIENI DAWA IWAINGIE VIZURI.
 
Mshaanza kulalamika na wapiga kura tena...

Sina popote ninapolalamika, bali nimesema wazi kuwa NEC imepika idadi ya wapiga kura ili kutoa matokeo ya uongo wakati wa uchaguzi. Na maelezo ya ushahidi wangu yako wazi. Labda ukanishe ukweli wangu kwa maelezo yasiyoacha shaka.
 
ukiona adui yako anafurahia au kukuacha ufanye jambo fulani ujue lina madhara kwako, polisi kumsindikiza lisu na kuruhusu mikusanyiko na kumuacha aihutubie wakati anatafuta wadhamini ni kielelezo tosha alianza kampeni kabla,
YAFAHAMU MAPINGAMIZI HALALI YA KISHERIA AMBAYO ANAWEZA AKAWEKEWA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS NCHINI TANZANIA.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo. Wanao muandama Lisu na style yake ya Kurafuta Kura za uzamini eti anafanya Campaign watasubiri sana.. Labda mtwambie Siyo Rai kwa kukaa nje ya nchi kwa 3yrs
 
Kavunja kanuni. Unampitishaje? Mwanasheria mzima kanuni hazijui. Kati ya wagombea wote zaidi ya kumi, umemuona nani anatafita wadhamini kwa mikutano na hotuba
CCM walizuia mikutano ya siasa kwa mda wa Miaka mitano lakini wao walikuwa wakifanya mikutano hata juzi wameandaa tamasha uwanja wa Taifa wasanii wakapigana mitama
 
Kwa kuwa mahakama ipo chini yao tutaona itakavyo kuwa.... Nguvu ya umma labda Tz haipo...
Vitu vingine msitamke bila kujua maana yake..eti nguvu ya imma, unamaanisha Nini hapa manake nikichukua tafsiri ya umma ni 90% wapo nyuma ya Magufuli, 10% gawanya 3 ACT, 2 chadema,1 nccr,1cuf na 3 vyama vingine vilivyobaki..Sasa hii nguvu unayoisemea jomba haina lolote, umechina tu wewe..nipange upya
 
yaan popote alipo jiwe lazima paharibike jambo..kule chamani amefanikiwa kuwakata akina membe ili agombee peke yake huku nako anataka apite kwa kukata watu..hivi huyu mzee ana matatizo gani aache upuuzi..
Ana shetani na roho mbaya sana
 
Back
Top Bottom