minyoo
JF-Expert Member
- May 25, 2013
- 22,405
- 21,100
Sakaya ni mchepuko wa Lipumba lakini ana michepuko mingineyo Mingi, hajatulia kabsaHalafu na yule mama Sakaya mbona kachujuka sana usoni utadhani kuna njemba ilimdufuanga mwili mzima
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sakaya ni mchepuko wa Lipumba lakini ana michepuko mingineyo Mingi, hajatulia kabsaHalafu na yule mama Sakaya mbona kachujuka sana usoni utadhani kuna njemba ilimdufuanga mwili mzima
Huyo msaliti Lipumba, hiyo dhambi anayotaka kuifanya, atambue tu kuwa haitasamehewa milele na Taifa hili!Lipumba mvurugaji tu hatoshi hata udiwani
Hivi wewe unajifanya umeshasahau kampeni alizopiga huyo Jiwe wako wakati aliwapiga marufuku wapinzani wasifanye mikutano yoyote ya hadhara, hadi mikutano ya ndani??Hata mimi, kama mpiga kura niliyejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, nafikiria very seriously, KUMUWEKEA LISSU PINGAMIZI kwani kaanza kampeni mapema. Ninashauriana na Mawakili wangu na kuzipitia CLIP TULIZOKUSANYA wakati akiwa kwenye hiyo misafara yake ya "kutafuta wadhamini". Pia tunajaribu kuangalia kutoka kona nyingine ya KUTUMIA LUGHA YA MATUSI kwenye hiyo misafara yake. Ninataka nione huyo Amsterdam atakacho kuja kufanya kumsaidia huyu mteja wake.
ujuaji mwingi mbele kiza, hebu twende na namba 13 kwanza, ...unayajua maadili ya uchaguzi weye???, unakurupuka tu eti sio raiaYAFAHAMU MAPINGAMIZI HALALI YA KISHERIA AMBAYO ANAWEZA AKAWEKEWA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS NCHINI TANZANIA.
Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;
(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.
(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.
(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.
(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.
(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.
(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.
(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.
(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.
(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=
(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.
(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.
(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.
(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.
(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.
(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.
(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.
(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.
(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.
Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo. Wanao muandama Lisu na style yake ya Kurafuta Kura za uzamini eti anafanya Campaign watasubiri sana.. Labda mtwambie Siyo Rai kwa kukaa nje ya nchi kwa 3yrs
Kwani mkuu daftari ya kupiga kura inajiandikisha automatically bila mlengwa kuja mwenyewe kujiandikisha?Science gani wakati tume mmeiagiza kuja na idadi ya kubumba ya wapiga kura? Watanzania tunakaribia 60m, huku idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa tume ni 29m+. Inawezekana vipi nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kupiga kura? Na ni kweli kuwa watu wenye miaka 18+ ni nusu sawa ya walio chini ya miaka hiyo? Kama sio Magufuli na ccm wamejiandaa kutangaza matokeo ya uongo, na kuuingiza nchi hii kwenye umwagaji wa damu ni nini zaidi?
Kwani mkuu daftari ya kupiga kura inajiandikisha automatically bila mlengwa kuja mwenyewe kujiandikisha?
Kujiandikisha hadi kupewa kitambulisho hakuna mlolongo mkubwa kama kitambulisho cha NIDA.
Mass exodus ya wabunge, madiwani na viongozi wa vyama vya upinzani hasa Chadema kuhamia CCM imevunja sana mioyo ya wanamageuzi,nadhani wapiga kura wapya hawakuvutiwa kujiandikisha,lakini na wale walio kwenye daftari baadhi yao hawatapiga kura,wamekata tamaa.
Kupiga kura sio jambo la lazima Tanzania, japo zipo nchi kama Switzerland ni lazima kwa mujibu wa sheria yao.
Nimekuelewa lakini hata hiyo namba 29 ml kama ingekuwa kweli itapunguwa sana kwa watakaojitokeza siku ya kupiga kura.Mkuu umeona hoja yangu ilipo? Kama wapiga kura ni 29m+, basi hakuna mtu yoyote mwenye umri wa kupiga kura hajajiandikisha. Sasa unaposema watu wamevunjika moyo kisha watu wazima wote kuanzia miaka 18 na kuendelea wamejiandikisha unamaanisha nini?
Hatari sanaaMbio za kuwania urais wa Tanzania kwa Tundu Lissu, huenda zikafikia ukingoni siku chache baada ya kukabidhi fomu zake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Lissu alipitishwa na chama chake, CHADEMA kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi wa mwaka huu, 2020 uliopangwa kufanyika Oktoba 28.
Read more > Urais 2020: Lissu kuwekewa vikwazo kimkakati - Imevuja!
Nimekuelewa lakini hata hiyo namba 29 ml kama ingekuwa kweli itapunguwa sana kwa watakaojitokeza siku ya kupiga kura.
Tarehe 26/8 nitakutafuta na uturn yako maana unaonekana mganga wa kienyeji kupiga ramliOK. Tusubiri. Hasira na mapovu ya nini gTurn!?
Wale wale! Badala ya hoja ili tuyajenge humu JF wanakuja na vihoja na vioja!Hujaweka na namba ya simu upate uteuzi kabla ya uchaguzi
Mataga mwaka huu mtatukana sana lakin lazima mtage na babayenu mliyemdanganya anakubalika kumbe mlikuwa mnapiga hela kwa kununua wapinzani lissu juuuuuuuuJaribu wewe uone sijui Nali ndio nchi gani!! hapa hutamwaga damu ya mtu wala nini, jaribu hata kumwaga mkojo hadharani uone kazi, c. h.i z wewe
JUU ZAIDI HADI UBELGIJI!Mataga mwaka huu mtatukana sana lakin lazima mtage na babayenu mliyemdanganya anakubalika kumbe mlikuwa mnapiga hela kwa kununua wapinzani lissu juuuuuuuu
Msikilize aliyoko makanisani kwanza halafu urejee hapaHata mimi, kama mpiga kura niliyejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, nafikiria very seriously, KUMUWEKEA LISSU PINGAMIZI kwani kaanza kampeni mapema. Ninashauriana na Mawakili wangu na kuzipitia CLIP TULIZOKUSANYA wakati akiwa kwenye hiyo misafara yake ya "kutafuta wadhamini". Pia tunajaribu kuangalia kutoka kona nyingine ya KUTUMIA LUGHA YA MATUSI kwenye hiyo misafara yake. Ninataka nione huyo Amsterdam atakacho kuja kufanya kumsaidia huyu mteja wake.
Kati ya mapingamizi ya kisheria yaliyoko hapo chini watatumia lipi?? MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.Mbio za kuwania urais wa Tanzania kwa Tundu Lissu, huenda zikafikia ukingoni siku chache baada ya kukabidhi fomu zake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Lissu alipitishwa na chama chake, CHADEMA kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi wa mwaka huu, 2020 uliopangwa kufanyika Oktoba 28.
Read more > Urais 2020: Lissu kuwekewa vikwazo kimkakati - Imevuja!
Kawahiyo yule aliyokua akihutubia pekeyake yy na kebinet ya chama chake tu ilikua akitangaazaa niniukiona adui yako anafurahia au kukuacha ufanye jambo fulani ujue lina madhara kwako, polisi kumsindikiza lisu na kuruhusu mikusanyiko na kumuacha aihutubie wakati anatafuta wadhamini ni kielelezo tosha alianza kampeni kabla,
Mgombea Wa CCM alikuwepoCCM walizuia mikutano ya siasa kwa mda wa Miaka mitano lakini wao walikuwa wakifanya mikutano hata juzi wameandaa tamasha uwanja wa Taifa wasanii wakapigana mitama
Pole sana ndugu,Wale wale! Badala ya hoja ili tuyajenge humu JF wanakuja na vihoja na vioja!