Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Mama anapata usingizi vizuri kweli? Unatoka kutoa boko unapa taarifa ya kukuchapa kibao🥲😂😂 Yaani ni bandika bandua, kila ukijaribu kumkandamiza ndio kama unamuweka kwenye spotlight ili aonekane vizuri😂.
====
Muungano wa vyama vya kidemokrasia duniani (IDU) umehitimisha mfululizo wa mikutano yake Jijini Brussels, Ubelgiji kwa kufanya uchaguzi wa safu mpya ya uongozi.
Katika mkutano huo ambako chama kiliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Democracy Union of Africa (DUA) Kanda ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Deogratias Munishi, wajumbe walimchagua Waziri Mkuu mstaafu wa 22 wa Canada Mheshimiwa Stephen J Harper kuendelea kuwa Mwenyekiti kwa miaka mitatu ijayo.
Aidha, mkutano mkuu kwa kauli moja ulimchagua Mwenyekiti wa chama Taifa Mhe. Tundu Antiphas Lissu kuwa sehemu ya jopo la Makamu Wenyeviti wa umoja huu.
Rekodi ya msimamo usioyumba katika kupigania haki, utawala bora na demokrasia Tanzania licha ya mazingira hatarishi ikiwemo jaribio la kutolewa uhai kama ilivyoelezwa kwenye mkutano mkuu ndiyo iliyowapa imani wajumbe kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni kumchagua Mhe Lissu katika wadhifa huu.
Zaidi, wajumbe wa mkutano mkuu wa IDU walitanabaisha kuwa, kwa uzoefu wake katika mapambano ya kutafuta demokrasia ya kweli, haki na uhuru wa kweli, Mh Lissu atatoa mchango mkubwa ndani ya IDU hasa katika kumulika maeneo yanayokabiliwa na changamoto za kuporomoka au kudorora kwa demokrasia na kuibuka kwa tawala za kihimla husani bara la Afrika.
Imetolewa leo Jumamosi, 24 Mei 2025.
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

TAARIFA KWA UMMA
KUCHAGULIWA KWA MHE. TUNDU LISSU KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA IDU