PreGE2025 Lissu achaguliwa kuwa sehemu ya jopo la Makamu Wenyeviti IDU akiwa gerezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huwezi kufunika jua kwa ungo, tulisema toka mwanzo. Mungu kumnusuru na zile risasi na kumponyesha majeraha. Alikuwa bado ana kazi naye.

Mpaka hiyo kazi ikamilike, Lissu ni aina ya binadamu wachache, hutumwa na Mungu kwa kazi maalumu. Waache wahangaike naye, lazima atawashinda. Kuna siku historia itaandikwa kivingine kabisa.
 
Kamponya alafu akatuamulia ugomvi dhidi ya kisababishi.🙏
 
Tundu Lissu ameteuliwa kuwa mmoja wa Makamu Mwenyekiti Watendaji (Executive Vice Chairmen) wa International Democrat Union (IDU), shirika la kimataifa linalojumuisha vyama vya siasa vya mrengo wa kulia na kati-kulia kutoka kote duniani. Taarifa hii imethibitishwa kupitia tovuti rasmi ya IDU, ambapo jina lake linaorodheshwa pamoja na viongozi wengine wa kimataifa kama Priti Patel (Uingereza), Scott Morrison (Australia), na David McAllister (Ujerumani) .

Uteuzi huu unakuja wakati ambapo Lissu anakabiliwa na changamoto kubwa kisiasa nchini Tanzania. Mnamo Aprili 2025, alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uhaini kufuatia hotuba yake iliyodaiwa kuhamasisha wananchi kupinga uchaguzi mkuu ujao. Chama chake, CHADEMA, pia kiliondolewa kushiriki katika uchaguzi huo baada ya kukataa kusaini kanuni za uchaguzi zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi .

IDU imelaani vikali mashtaka dhidi ya Lissu, ikiyataja kuwa hayana msingi wa kisheria na kwamba yanakusudia kunyamazisha upinzani wa kisiasa. Pia, IDU ilielezea wasiwasi wake kuhusu kuhamishwa kwa Lissu kwa siri hadi Gereza la Ukonga na kuwekwa katika kifungo cha upweke, ikitaja hatua hiyo kama ukiukwaji wa haki za binadamu .

Uteuzi wa Lissu katika nafasi ya juu ndani ya IDU unaashiria kuungwa mkono kimataifa kwa juhudi zake za kutetea demokrasia na haki za binadamu nchini Tanzania, hasa wakati huu mgumu wa kisiasa kwake binafsi na kwa chama chake.
Hongera kwake mpigania mageuzi huyu.
 
Wakuu,

Mama anapata usingizi vizuri kweli? Unatoka kutoa boko unapa taarifa ya kukuchapa kibao🥲😂😂 Yaani ni bandika bandua, kila ukijaribu kumkandamiza ndio kama unamuweka kwenye spotlight ili aonekane vizuri😂.

====

TAARIFA KWA UMMA

KUCHAGULIWA KWA MHE. TUNDU LISSU KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA IDU​

Muungano wa vyama vya kidemokrasia duniani (IDU) umehitimisha mfululizo wa mikutano yake Jijini Brussels, Ubelgiji kwa kufanya uchaguzi wa safu mpya ya uongozi.

Katika mkutano huo ambako chama kiliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Democracy Union of Africa (DUA) Kanda ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Deogratias Munishi, wajumbe walimchagua Waziri Mkuu mstaafu wa 22 wa Canada Mheshimiwa Stephen J Harper kuendelea kuwa Mwenyekiti kwa miaka mitatu ijayo.

Aidha, mkutano mkuu kwa kauli moja ulimchagua Mwenyekiti wa chama Taifa Mhe. Tundu Antiphas Lissu kuwa sehemu ya jopo la Makamu Wenyeviti wa umoja huu.

Rekodi ya msimamo usioyumba katika kupigania haki, utawala bora na demokrasia Tanzania licha ya mazingira hatarishi ikiwemo jaribio la kutolewa uhai kama ilivyoelezwa kwenye mkutano mkuu ndiyo iliyowapa imani wajumbe kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni kumchagua Mhe Lissu katika wadhifa huu.

Zaidi, wajumbe wa mkutano mkuu wa IDU walitanabaisha kuwa, kwa uzoefu wake katika mapambano ya kutafuta demokrasia ya kweli, haki na uhuru wa kweli, Mh Lissu atatoa mchango mkubwa ndani ya IDU hasa katika kumulika maeneo yanayokabiliwa na changamoto za kuporomoka au kudorora kwa demokrasia na kuibuka kwa tawala za kihimla husani bara la Afrika.

Imetolewa leo Jumamosi, 24 Mei 2025.

Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

Sio mchezo. Kumekucha
 
Mtaendelea kuchaguana kwenye vyeo vusivyo na maana na huko ndiko Kibaraka Lisu anafaa Sasa sio kwenye Urais.
 
Back
Top Bottom