PreGE2025 Lissu achaguliwa kuwa sehemu ya jopo la Makamu Wenyeviti IDU akiwa gerezani

PreGE2025 Lissu achaguliwa kuwa sehemu ya jopo la Makamu Wenyeviti IDU akiwa gerezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hongera kwake Mh Tundu Lissu! 🙌🏽
Kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IDU ni hatua kubwa sana! Heshima hii inaonesha jinsi dunia inavyotambua jitihada zake kwenye mapambano ya haki na demokrasia. Tunajivunia yeye! 🇹🇿🔥
#TeamHaki #Chadema #Demokrasia
Mh. Tundu Lissu ni mwalimu na zana halisi kwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa jumla.

Hongera kaka umekuwa kalamu ya kuandika nchi yako duniani.

Tatizo la vijana watanzania ni wanafiki na waoga. Wakiamua maandamano nchi nzima mbona serikali na dola watapiga magoti fasta.
 
Sawa sawa
Sema kitu bhana.

Wengi wanadai yasipotokea mabadiliko ya msingi katika uhai wa TAL, huenda yasiwepo tena kwa miongo mingi, mingi sana ijayo.

Je, unakubaliana na hoja hiyo?

Yale mawe tuliyoambiwa yataongea wakati viongozi wakweli na wazalendo wa Sidiemu wakinyamazishwa, sasa tunaona waziwazi yameanza kweli kuongea.

All in all, tulitakie taifa letu mchakato mzuri wa haki iletayo amani ya kweli.
 
Mmh ila hii ni vita baridi ,kuchafua image ya sa100 indirectly .watu tulisema haina haja ya kumfunga wala kumpiga kila mfu afanye siasa kivyake mbona mambo yangeenda tu ila kukopy mfumo wa mwenda zake imewacost next stop vikwazo vya kiuchumi
Huwa wanaanza hivi hivi sasa vikwazo vya kiuchumi kwa nchi kama Tz. Aisee tutahamia Burundi kama alivyosemaga bwana Chemba
 
Na lazima atapewa mawakili wa kimataifa kosa kubwa alifanya samia juzi kupiga wale wanaharakati imezidi kumsagia kunguni nje ya mipaka ya nchi.
Aisee.
Kwa hiyo Samia na Serikali yake ya CCM wamemweka gerezani kwa tuhuma za kisiasa Makamu Mwenyekiti wa IDU ambayo ndani yake kuna vyama vinavyoongoza Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ubelgiji?

Kweli tumefika pazuri sana.
 
Back
Top Bottom