Pre GE2025 Lissu ahoji Rais anapata wapi pesa za kugawa kwa viongozi wa dini? kwa mshahara gani?

Pre GE2025 Lissu ahoji Rais anapata wapi pesa za kugawa kwa viongozi wa dini? kwa mshahara gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wakati akifanya mahojiano na ITV, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amehoji ni wapi Rais anatoa fedha za kuwapa viongozi wa dini? kwa mshahara upi?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Hatupendi viongozi wetu wa dini wahongwe, hatutaki viongozi wetu wa kidini wapewe mamilioni ya pesa na Rais wa nchi yetu. Rais anapata wapi pesa, mamilioni ya kugawa makanisni au misikitini?" - Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA

Soma: Pre GE2025 - Hizi ndizo zawadi, misaada na michango iliyotolewa na Rais Samia tangu aingie Ikulu. Ni maandalizi ya Urais 2025?
 
Ni ujinga tu wa Watanzania ndo mana kila siku Wanasiasa wanawaibia na kufisadi pesa zao hadi basi.

Watanzania wanapaswa kujua hakuna kitu kinaitwa pesa za Rais. Pesa zote za Serikali ni pesa za Wananchi na zinapaswa kutumiwa kwa utaratibu uliopitishwa na Bunge katika Bajeti ya Serikali iliyoidhinishwa Bungeni.

Ukisoma bajeti huwezi kuta kifungu kinachosema Fedha za kununua magoli. Ukisoma bajeti huwezi kuta kifungu kinachoonesha Pesa za kuchangia au kuwapa/ kuwahonga maaskofu.

Hizi ni Pesa za Walipakodi wa Nchi hii ambazo zinapaswa kutumika kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanapata huduma bora kila siku kama maji, madawa hospitali, shule bora na nzuri kwa watoto wao na barabara bora hadi kwenye nyumba zao.

Ila kutokana na ubovu wa Katiba yetu inayowapa Wanasiasa kuwa miungu watu kwa sababu hawawajibishwi fedha za wananchi zinatumiwa kwa matumizi ya kijinga tu huku wananchi wakiwa hawana lolote la kufanya na mbaya zaidi utawakuta wanashukuru na kupiga magoti kumbe ni ujinga tu.

Nchi hii inaibiwa sana na ikitokea wananchi wakapata akili hawa viongozi wanaweza kuchomwa moto wote
 
Ni ujinga tu wa Watanzania ndo mana kila siku Wanasiasa wanawaibia na kufisadi pesa zao hadi basi.

Watanzania wanapaswa kujua hakuna kitu kinaitwa pesa za Rais. Pesa zote za Serikali ni pesa za Wananchi na zinapaswa kutumiwa kwa utaratibu uliopitishwa nq Bunge katika Bajeti ya Serikali iliyoidhinishwa Bungeni.

Ukisoma bajeti huwezi kuta kifungu kinachosema Fedha za kununua magoli. Ukisoma bajeti huwezi kuta kifungu kinachoonesha Pesa za kuchangia au kuwapa/ kuwahonga maaskofu.

Hizi ni Pesa za Walipakodi wa Nchi hii ambazo zinapaswa kutumika kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanapata huduma bora kila siku kama maji, madawa hospitali, shule bora na nzuri kwa watoto wao na barabara bora hadi kwenye nyumba zao.

Ila kutokana na ubovu wa Katiba yetu inayowapa Wanasiasa kuwa miungu watu kwa sababu hawawajibishwi fedha za wananchi zinatumiwa kwa matumizi ya kijinga tu huku wananchi wakiwa hawana lolote la kufanya na mbaya zaidi utawakuta wanaahukuru na kupiga magoti kumbe ni ujinga tu.

Nchi hii inaibiwa sana na ikitokea wananchi wakapata akili hawa viongozi wanaweza kuchomwa moto wote
Fungu la bajeti ya Ofisi ya Rais

Hata enzi za JK Viongozi wa Chadema Walikuwa wanaenda Ikulu Kunywa Juice na Samosa lilitumika fungu hili

Ahsante sana 😄
 
Fungu la bajeti ya Ofisi ya Rais

Hata enzi za JK Viongozi wa Chadema Walikuwa wanaenda Ikulu Kunywa Juice na Samosa lilitumika fungu hili

Ahsante sana 😄
Hilo fingu la Bajeti liweke hapa tuone kama kuna pesa za kununua magoli na kuwahonga maaskofu na masheikh.

Hii nchi kuna watu tuna akili. Msituone wote ni wapumbavu.
 
Hilo fingu la Bajeti liweke hapa tuone kama kuna pesa za kununua magoli na kuwahonga maaskofu na masheikh.

Hii nchi kuna watu tuna akili. Msituone wote ni wapumbavu.
Hilo fungu huwa halijadiliwi Bungeni

Kama unabisha waulize Wenyeviti wa kamati za Fedha Bungeni ambao miaka yote wametoka Chadema 😂😂😂
 
Wakati akifanya mahojiano na ITV, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amehoji ni wapi Rais anatoa fedha za kuwapa viongozi wa dini? kwa mshahara upi?

"Hatupendi viongozi wetu wa dini wahongwe, hatutaki viongozi wetu wa kidini wapewe mamilioni ya pesa na Rais wa nchi yetu. Rais anapata wapi pesa, mamilioni ya kugawa makanisni au misikitini?" - Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3240205
Chadema kura za viongozi wa dini wameshazikosa tayari kwa hili tamko la Lisu
 
Back
Top Bottom