Pre GE2025 Lissu ahoji Rais anapata wapi pesa za kugawa kwa viongozi wa dini? kwa mshahara gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe ametumwa mara kadhaa kupeleka michango ya Rais Kwa viongozi wa dini akiwa kama Mwenyekiti wa Chadema
Kwa kutumwa Mbowe (kama unavyodai) hiyo inahalalisha haramu ya rushwa kwa viongozi wa dini kutoka kwa Rais?!
 
Ukishakuwa masikini huna akili unaona pesa za mwenzako anazitumia vibaya...
Basi muombeni Samia awachangie na nyie
 
Wakati akifanya mahojiano na ITV, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amehoji ni wapi Rais anatoa fedha za kuwapa viongozi wa dini? kwa mshahara upi?

"Hatupendi viongozi wetu wa dini wahongwe, hatutaki viongozi wetu wa kidini wapewe mamilioni ya pesa na Rais wa nchi yetu. Rais anapata wapi pesa, mamilioni ya kugawa makanisni au misikitini?" - Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3240205
Soma: Pre GE2025 - Hizi ndizo zawadi, misaada na michango iliyotolewa na Rais Samia tangu aingie Ikulu. Ni maandalizi ya Urais 2025?
Sitaki
Hiyo bajeti inapitishwa na nani na ni sh ngapi kwa muda gani?
Are you serious kwamba hujui kila mwaka bunge linapitisha fungu la Rais?
Mi nikidhani Lisu tu hajui kumbe hata wewe!
Kuna mwaka J. Mnyika alihoji bungeni matumizi ya hili fungu, akajibiwa na Hawa Ghasia kuwa kuna watoto wadogo wameingia bungeni juzi wanataka kujua ht visivyoruhusiwa na ikaishia hapo
 
Tuoneshe zimewekwa shilingi ngapi kwenye miaka hii ya Urais wa Samia na matumizi yake yakoje?

Acheni kutetea wizi! Hizi ni pesa zinazopaswa kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanakuwa na maisha bora.
 
Sasa umeona jinsi tulivyo na Katiba Mbovu? Kwa nini matumizi ya kodi za wananchi yasijadiliwe Bungeni?

Huoni hicho ndo kichaka cha Wanasiasa kufisadi hela za Wananchi? Matumizi ya kodi za Wananchi lazima yajulikane kwa Wananchi na huo ndio utawala bora.

Ndugu zako wanakosa madawa hospitali, tuna miundombinu mibovu ya barabara, kuna maeneo mijini na vijijini watu hawana maji hadi majumbani mwao wanaenda kuchota maji na Motorori kwenye visima na mabwawa. Alafu unapanua mdomo hapa eti kuna kifungu cha pesa hakijadiliwi Bungeni wakati watu wanaiba kodi zenu na kutumia kufanya ufisadi na ufedhuli nyie mkiwa mnaangalia tu.
Zingine anaenda kujenga Zanzibar zinachotwa tu hakuna namna
 
Wakati akifanya mahojiano na ITV, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amehoji ni wapi Rais anatoa fedha za kuwapa viongozi wa dini? kwa mshahara upi?

"Hatupendi viongozi wetu wa dini wahongwe, hatutaki viongozi wetu wa kidini wapewe mamilioni ya pesa na Rais wa nchi yetu. Rais anapata wapi pesa, mamilioni ya kugawa makanisni au misikitini?" - Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3240205
Soma: Pre GE2025 - Hizi ndizo zawadi, misaada na michango iliyotolewa na Rais Samia tangu aingie Ikulu. Ni maandalizi ya Urais 2025?
Kumekucha
 
Anachukua hazina then anagawa kama njugu pesa za walipa Kodi bila hata kuona aibu, Kwa kweli inasikitisha sana
Wakati akifanya mahojiano na ITV, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amehoji ni wapi Rais anatoa fedha za kuwapa viongozi wa dini? kwa mshahara upi?

"Hatupendi viongozi wetu wa dini wahongwe, hatutaki viongozi wetu wa kidini wapewe mamilioni ya pesa na Rais wa nchi yetu. Rais anapata wapi pesa, mamilioni ya kugawa makanisni au misikitini?" - Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3240205
Soma: Pre GE2025 - Hizi ndizo zawadi, misaada na michango iliyotolewa na Rais Samia tangu aingie Ikulu. Ni maandalizi ya Urais 2025?
 
Tuoneshe zimewekwa shilingi ngapi kwenye miaka hii ya Urais wa Samia na matumizi yake yakoje?

Acheni kutetea wizi! Hizi ni pesa zinazopaswa kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanakuwa na maisha bora.
Hilo swali hata ukimuuliza CAG mwenyewe hajui na haruhusiwi kujua.
Hilo fungu ni halikaguliwi. Ina maana ht wewe hujui kama Lisu tu!
 
Tushike lipi tuache lipi? Kwa nini kuwe na matumizi ya fedha za walipakodi ambazo hayqkaguliwi?

Kama hayakaguliwi maana yake nini? Maana yake ni kwamba hiyo ni njia ya kuiba Pesa za Walipakodi ambapo ni dharau kubwa kwa walipa kodi wa Taifa hili

Huoni huo ni Ufisadi tena wa kutisha?
 
Nnachokishangaa hapa ni kuwa wewe na Lisu hamlijui hilo mpk leo! Hamjui kwamba kuna pesa haziruhusiwi kukaguliwa matumizi yake!
Mbona hili ni jambo la kawaida kwa serikali zote duniani
 
Nani kasema ni jambo la kawaida kwa Serikali zote?

Hivi unajua sehemu zingine duniani huko wananchi walivyo Serious za matumizi ya kodi zao?

Pia fedha zozote zile hata kama hazikaguliwi lazima zitengwe kwenye Bajeti kuu ya Serikali na ziwepo kwenye chati ya matumizi.

Kwa nini msituoneshe hizo pesa kwenyw mpango wa matumizi wa Serikali uliopitishwa na Bunge?
 
Rais wa nchi anayo bajeti maalumu ambayo anatumia kwa shughuli mbalimbali za kijamii. Wacha Rais, hata Mawaziri na Wakuu wa Mashirika ya umma na binafsi wanayo bajeti hiyo.

Fedha hizo anaweza akampa mwananchi yeyote ambaye ataona kuna haja. Hata viongozi wa dini ni sehemu ya wananchi ambao wanaweza kupewa fedha hizi. Kwa nini mnataka kuwatenga na Rais halafu mnasema watasimama na Chadema kwenye uchaguzi. Maneno hayo yanaweza kueleweka tu kwa watu wenye akili ndogo, kama anavyoonekana Lisu na wafuasi wake wachache
Hilo fungu la Rais unalosema huwa linatengwa kwa kazi za kusaidia jamii sio kusaidia makanisa.
Mfano Wakati Siku Kuu fedha huenda kusaidia watoto yatima au vituo vya wazee.
Na zile fedha zina ukomo wake...Sijui kama ndo Honoraria lkn haijasemwa kupelekwa kanisani au msikitini...Hiyo ni rushwa na matumiz mabaya ya fedha za mfuko wa Rais.
 
Nnachokishangaa hapa ni kuwa wewe na Lisu hamlijui hilo mpk leo! Hamjui kwamba kuna pesa haziruhusiwi kukaguliwa matumizi yake!
Mbona hili ni jambo la kawaida kwa serikali zote duniani
Ni Tz ndo kuna hizi fedha chafu.
Nchi zingine Rais atapewa baada kuondoka madarakani na atakua na mfuko maalum wa kusaidia jamii..(Foundation )
 
Hilo fungu la Rais unalosema huwa linatengwa kwa kazi za kusaidia jamii sio kusaidia makanisa.
Mfano Wakati Siku Kuu fedha huenda kusaidia watoto yatima au vituo vya wazee.
Na zile fedha zina ukomo wake...Sijui kama ndo Honoraria lkn haijasemwa kupelekwa kanisani au msikitini...Hiyo ni rushwa na matumiz mabaya ya fedha za mfuko wa Rais.
Hawana hoja zozote ni waongo tu.

Pesa zote za matumizi ya Serikali ni lazima zipitishwe kwenye Bajeti na kuna Jedwali na matumizi linaloidhinishwa na Bunge wakati wa kupitisha Bajeti hiyo.

Nimewauliza hapa walete hilo jedwali la matumizi watuoneshe ni wapi kuliluwa na hizo fedha zinazoonesha matumizi ya fedha za kununua magoli ya Simba, Yanga na Azam au za kuwapa Maaskofu na Masheikh hawajaleta hata huo uthibitisho.

Nyaraka za Bungeni hasa kwenye Bajeti ni Public Documents kwa nini hawaweki huo uthibitisho humu?
 
Chadema kura za viongozi wa dini wameshazikosa tayari kwa hili tamko la Lisu

..kuna maelfu ya viongozi wa dini hawajapata fedha za Mama Abduli.

..kwa mfano Shekhe Mkuu wa Arusha kapewa gari Range rover.

..Je, unadhani Mashekhe wa mikoa 30 iliyobaki Tanganyika hawahitaji Range rover? Je, lini watazipewa?
 
Back
Top Bottom