Pre GE2025 Lissu ahoji Rais anapata wapi pesa za kugawa kwa viongozi wa dini? kwa mshahara gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe ametumwa mara kadhaa kupeleka michango ya Rais Kwa viongozi wa dini akiwa kama Mwenyekiti wa Chadema
Kwa kutumwa Mbowe (kama unavyodai) hiyo inahalalisha haramu ya rushwa kwa viongozi wa dini kutoka kwa Rais?!
 
Ukishakuwa masikini huna akili unaona pesa za mwenzako anazitumia vibaya...
Basi muombeni Samia awachangie na nyie
 
Sitaki
Hiyo bajeti inapitishwa na nani na ni sh ngapi kwa muda gani?
Are you serious kwamba hujui kila mwaka bunge linapitisha fungu la Rais?
Mi nikidhani Lisu tu hajui kumbe hata wewe!
Kuna mwaka J. Mnyika alihoji bungeni matumizi ya hili fungu, akajibiwa na Hawa Ghasia kuwa kuna watoto wadogo wameingia bungeni juzi wanataka kujua ht visivyoruhusiwa na ikaishia hapo
 
Tuoneshe zimewekwa shilingi ngapi kwenye miaka hii ya Urais wa Samia na matumizi yake yakoje?

Acheni kutetea wizi! Hizi ni pesa zinazopaswa kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanakuwa na maisha bora.
 
Zingine anaenda kujenga Zanzibar zinachotwa tu hakuna namna
 
Kumekucha
 
Anachukua hazina then anagawa kama njugu pesa za walipa Kodi bila hata kuona aibu, Kwa kweli inasikitisha sana
 
Tuoneshe zimewekwa shilingi ngapi kwenye miaka hii ya Urais wa Samia na matumizi yake yakoje?

Acheni kutetea wizi! Hizi ni pesa zinazopaswa kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanakuwa na maisha bora.
Hilo swali hata ukimuuliza CAG mwenyewe hajui na haruhusiwi kujua.
Hilo fungu ni halikaguliwi. Ina maana ht wewe hujui kama Lisu tu!
 
Hilo swali hata ukimuuliza CAG mwenyewe hajui na haruhusiwi kujua.
Hilo fungu ni halikaguliwi. Ina maana ht wewe hujui kama Lisu tu!
Tushike lipi tuache lipi? Kwa nini kuwe na matumizi ya fedha za walipakodi ambazo hayqkaguliwi?

Kama hayakaguliwi maana yake nini? Maana yake ni kwamba hiyo ni njia ya kuiba Pesa za Walipakodi ambapo ni dharau kubwa kwa walipa kodi wa Taifa hili

Huoni huo ni Ufisadi tena wa kutisha?
 
Nnachokishangaa hapa ni kuwa wewe na Lisu hamlijui hilo mpk leo! Hamjui kwamba kuna pesa haziruhusiwi kukaguliwa matumizi yake!
Mbona hili ni jambo la kawaida kwa serikali zote duniani
 
Nnachokishangaa hapa ni kuwa wewe na Lisu hamlijui hilo mpk leo! Hamjui kwamba kuna pesa haziruhusiwi kukaguliwa matumizi yake!
Mbona hili ni jambo la kawaida kwa serikali zote duniani
Nani kasema ni jambo la kawaida kwa Serikali zote?

Hivi unajua sehemu zingine duniani huko wananchi walivyo Serious za matumizi ya kodi zao?

Pia fedha zozote zile hata kama hazikaguliwi lazima zitengwe kwenye Bajeti kuu ya Serikali na ziwepo kwenye chati ya matumizi.

Kwa nini msituoneshe hizo pesa kwenyw mpango wa matumizi wa Serikali uliopitishwa na Bunge?
 
Hilo fungu la Rais unalosema huwa linatengwa kwa kazi za kusaidia jamii sio kusaidia makanisa.
Mfano Wakati Siku Kuu fedha huenda kusaidia watoto yatima au vituo vya wazee.
Na zile fedha zina ukomo wake...Sijui kama ndo Honoraria lkn haijasemwa kupelekwa kanisani au msikitini...Hiyo ni rushwa na matumiz mabaya ya fedha za mfuko wa Rais.
 
Nnachokishangaa hapa ni kuwa wewe na Lisu hamlijui hilo mpk leo! Hamjui kwamba kuna pesa haziruhusiwi kukaguliwa matumizi yake!
Mbona hili ni jambo la kawaida kwa serikali zote duniani
Ni Tz ndo kuna hizi fedha chafu.
Nchi zingine Rais atapewa baada kuondoka madarakani na atakua na mfuko maalum wa kusaidia jamii..(Foundation )
 
Hawana hoja zozote ni waongo tu.

Pesa zote za matumizi ya Serikali ni lazima zipitishwe kwenye Bajeti na kuna Jedwali na matumizi linaloidhinishwa na Bunge wakati wa kupitisha Bajeti hiyo.

Nimewauliza hapa walete hilo jedwali la matumizi watuoneshe ni wapi kuliluwa na hizo fedha zinazoonesha matumizi ya fedha za kununua magoli ya Simba, Yanga na Azam au za kuwapa Maaskofu na Masheikh hawajaleta hata huo uthibitisho.

Nyaraka za Bungeni hasa kwenye Bajeti ni Public Documents kwa nini hawaweki huo uthibitisho humu?
 
Chadema kura za viongozi wa dini wameshazikosa tayari kwa hili tamko la Lisu

..kuna maelfu ya viongozi wa dini hawajapata fedha za Mama Abduli.

..kwa mfano Shekhe Mkuu wa Arusha kapewa gari Range rover.

..Je, unadhani Mashekhe wa mikoa 30 iliyobaki Tanganyika hawahitaji Range rover? Je, lini watazipewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…