Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Kaanza mapema sana, awe muangalifu na tume ya uchaguzi Tanzania wasije wakamuacha kati ya wagombea watakao teuliwa kugombea.

Muda wa kampeni bado.

Hajaanza kampeni bado.. haombi kura, anaongea kama mtia nia. Hao TCRA wamemchokoza wenyewe kukataa habari zake zisisemwe na vyombo vya habari.
 
Naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kidikiteta, lakini udikiteta wenyewe ni udikiteta wa kizalendo, a benevolent dictatorship, anafanya udikiteta kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

P

Ulishawekwa kando Mkuu. Siku uliyomuuliza lile swali Jiwe ndio siku uliyolikoroga. Na unamjua kwa visasi. Ilishaisha hiyo. So kuwa reasonable tu, huna cha kupoteza.
 
Hii haikuwa kampeni , ilikuwa malalamiko yake kwa yanayotendwa na TCRA
Vyovyote vile asubirie kwanza apitishwe na tume ya uchaguzi tarehe 25/8/20, baada ya hapo atayasema yote.

Kama kavumilia yote yaliyompata, anashindwa nini kuvumilia sasa.

Kila siku tunasema aache mihemko, muda wake bado kwasasa auvae u candidate aliouomba na kuupigania.

Wenzake umewaona wakifanya haya?! Kwanini wametulia au mnadhani wao wajinga sana.

Tujifunze kufuata taratibu, muda wa kampeni bado.
 
TCRA ilibidi ata wafungwe kwa unyanyasaji na kufutwa milele [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tume imesisitiza Mgombea mwenye sifa ndio atakayepitishwa! Nasisitiza mwenye sifa
 
Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake.

Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa ijieleze kwanini isiadhibiwe kutokana na kurusha alichoongea Lissu na BBC.

Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.

Lissu anadai malengo ya tume ya Nyalali ya kuondoa SHIHATA na kuleta TCRA yalilenga kuondoa ukiritimba baada ya Shihata kuonekana kuipendelea serikali, jambo ambalo bado halijatimia kwa vile TCRA wameendelea kutumika .

Binafsi naunga mkono TCRA Kufutiliwa mbali.
Ifutwe tu inatuumiza Sana sisi wanyonge

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hajaanza kampeni bado.. haombi kura, anaongea kama mtia nia. Hao TCRA wamemchokoza wenyewe kukataa habari zake zisisemwe na vyombo vya habari.
Sasa hivi anataka vyombo vya habari vya nini na kampeni hazijaruhusiwa?!

Mjifunze kumshauri vizuri na ukweli aambiwe, muda wa kampeni bado, mihemko ya nini?

Wakati mnatifuana na tume wenzenu watakuwa wanafanya kampeni, na mtakuja kukumbuka uzi huu muda uliisha pita.

Hao TCRA aachane nao, mbona habari za mikutano yake zinafika kila kona, radio na television zao mnataka za nini?!
 
Anaedai hana uhuru wa kusema, yukp Tanzania; hapo alipo kasema na kupitia YouTube kasikika.

Nadhani Tundu Lissu atupe vision yake anataka kutupeleka wapi Tanzania na sio kulalamika kila siku.

Watu kwa sasa wako huru kupata habari Nadhani kuliko nyakati zote.

Kama mainstream inaogopa, kuna various networks ambazo hata hao wanaolalama uhuru wa kusema kubinywa, wanatumia na kupata followers au ujumbe wao kufika.

So far kwa majigambo haya toka katika akidai katiba mpya siojaona jipya.

Kenya ambao tunawasifu kupata katiba mpya, ufisadi na kupiga hela kumeongezeka sana ukiwamo upigwaji wa hela zs Covid19.

Bila shaka JPM akashinda kwa kura nyingi ajabu. Na kama TL hatabadili ujumbe wake; akipata kura nyingi kuzidi za Mrema 1995; basi huu utakuwa muujiza.
sasa kama mna uhakika wa kupata kura nyingi hofu juu ya TL inatoka wapi?!.
kwann mnabinya vyombo vya habari visitoe taarifa zake...huoni kwamba wanamuhofia sana hadi kuzuia wananchi tusipate taarifa kumhusu yeye?!.
 
Naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kidikiteta, lakini udikiteta wenyewe ni udikiteta wa kizalendo, a benevolent dictatorship, anafanya udikiteta kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

P

Mkuu, njaa zimezidi ee!?
Yaani ukichukua jina lako "mayalla"
Sehemu ya "ya" ukiweka "lla" na "lla ikiwekwa kwenye "ya" basi tabia yako halisi ya sasa hasa kisiasa haitakuwa tofauti na jina jipya litakalopatikana baada ya kufanya mabadiliko ya hizo herufi!! In jpm's voice...!
 
Naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kidikiteta, lakini udikiteta wenyewe ni udikiteta wa kizalendo, a benevolent dictatorship, anafanya udikiteta kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

P
Hivi kuna udikteta wa kuleta maendeleo na usio wa kuleta maendeleo?
Unataka kusema Adolf Hitler alikua haleti maendeleo ujerumani? Alikua hajengi barabara?
Ko kutoupa Uhuru vyombo vya habari ndo udikteta wa maendeleo?
Mayala Jitafakari hata kama unataka uteuzi lakini usipende kuruhusu kutekwa akili yako.
 
Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.
Aisee...! Poleni sana wafuasi wake. Ndiyo mnaanza kujuta sasa kwa nini mlijichanganya. Sisi tunasonga mbele kuimarisha Tanzania katika nyanja zote.

Sasa anasema ataifuta TCRA. Akishaifuta TCRA ataweka mbadala upi kwenye kusimamia upatikanaji wa habari nchini? Au ndiyo ataweka Kurugezi ya Habari ya Chadema kama mbadala wa TCRA. Anaweza kufanya hivyo, maana ameanza kuubadili wimbo wetu wa Taifa!!! Hapa mwenye kuelewa na kuitakia mema Tanzania lazima amwangalie Lissu kwa jicho la 'kuchunga'.
 
kwa hoja hizi.....kichapo cha Mzee Lowassa kwa mgombea wa CCM 2015 kilikuwa cha mtoto!

Mgombea wa CCM kipindi hiki asichukulie poa....vijana tumemchoka,wazee hawataki kumsikia,watoto anaowadanganya kuwa wanapewa elimu bure ndio usiseme....namshauri mgombea wa CCM ajitoe tu....hana jipya la kuwaambia watanzania.....

NI MSHAMBA MNO!
 
Back
Top Bottom