Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

M
Mkuu maendeleo bila kutenda haki.
Kiongozi wa kweli ni yule atakaebadilisha uchumi wa watu wake na kuwapa Uhuru wa kujieleza ni hii huleta maendeleo endelevu.
KIPEWA UHURU HUO BILA MIPAKA WATANZANIA WANAJULIKANA WATAUTUMIA NDIVYOSIVYO ITAKUWA KERO KWA WATAWALA MNAJIJUA WENYEWE MLIVYO
 
Aisee...! Poleni sana wafuasi wake. Ndiyo mnaanza kujuta sasa kwa nini mlijichanganya. Sisi tunasonga mbele kuimarisha Tanzania katika nyanja zote.

Sasa anasema ataifuta TCRA. Akishaifuta TCRA ataweka mbadala upi kwenye kusimamia upatikanaji wa habari nchini? Au ndiyo ataweka Kurugezi ya Habari ya Chadema kama mbadala wa TCRA. Anaweza kufanya hivyo, maana ameanza kuubadili wimbo wetu wa Taifa!!! Hapa mwenye kuelewa na kuitakia mema Tanzania lazima amwangalie Lissu kwa jicho la 'kuchunga'.
Je Malengo ya kufuta Shihata yametimia ?
 
Haya maendeleo tunayosimangwa nayo ni haya ya kutoa ajira kwa wenye kadi za CCM?
Ajira za mipango, hupewi ajira mpaka uoneshe 'kadi ya kijani' (666). Inakera sana vijana hawana morale ya kusoma, maana hadi sectors binafsi kaziua.
 
Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake.

Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa ijieleze kwanini isiadhibiwe kutokana na kurusha alichoongea Lissu na BBC.

Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.

Lissu anadai malengo ya tume ya Nyalali ya kuondoa SHIHATA na kuleta TCRA yalilenga kuondoa ukiritimba baada ya Shihata kuonekana kuipendelea serikali, jambo ambalo bado halijatimia kwa vile TCRA wameendelea kutumika .

Binafsi naunga mkono TCRA Kufutiliwa mbali.

Ikifutwa TCRA ataleta nini? Au nchi itakuwa na "JUNGLE LAWS"?
 
niliwahi kumwambia mwanangu mmoja tukiwa seriously tunamjadili Magu. akasema mbona nampuuza sana wakati anafanya mambo makubwa? Nikamwambia kwangu yote ni hovyo maana anajijenga yeye badala ya kujenga na kuimarisha taasisi. Taasisi zimekuwa dhaifu kuliko wakati wowote. Nchi yenye taasisi weak ni kama baiskeli ya miti. Akifa yeye tunaanza upya
 
Naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kidikiteta, lakini udikiteta wenyewe ni udikiteta wa kizalendo, a benevolent dictatorship, anafanya udikiteta kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Kama udikteta ndio thawabu tunayopashwa kulipa ili tupate maendeleo afadhali tubaki maskini, hayo maendeleo yakae.

Post zingine humu zinatolewa na watu wanaonekana wamesoma lakini hawana akili kwani unaweza ukawa umesoma lkn hauna akili.
 
Vyovyote vile asubirie kwanza apitishwe na tume ya uchaguzi tarehe 25/8/20, baada ya hapo atayasema yote.

Kama kavumilia yote yaliyompata, anashindwa nini kuvumilia sasa.

Kila siku tunasema aache mihemko, muda wake bado kwasasa auvae u candidate aliouomba na kuupigania.

Wenzake umewaona wakifanya haya?! Kwanini wametulia au mnadhani wao wajinga sana.

Tujifunze kufuata taratibu, muda wa kampeni bado.
Hii siyo kampeni mkuu , haya ni malalamiko
 
baada ya kufutwa SHIHATA ililetwa nini ?
Aendelee kuota tu. Ila nina ushauri kwake, ajitahidi sana aboreshe Ofisi ya Makao Makuu Chadema pale Ufipa badala ya kufanyia vikao vya chama Mlimani City (matunda ya sera nzuri za CCM).
 
Sioni msaada wa TCRA apa nchini.. mimi mtu wa chini uku nahustle nao kuhusu laini(SimCard) yangu mara waifungie mara waniambie niihakiki na nimeihakiki, mara wairudishe..
 
Back
Top Bottom