Lissu akishinda tunatarajia CCM italazimika kuibua akiba yake ya makada wenye akili. Machawa nafasi yao inaweza kuwa hatarini

Lissu akishinda tunatarajia CCM italazimika kuibua akiba yake ya makada wenye akili. Machawa nafasi yao inaweza kuwa hatarini

Tupo salama wote!

Wakati CCM ipo Kimya ikiangalia yanayoendelea CHADEMA na mara kadhaa kwa Siri huenda ikijihusisha na mambo hayo kuyaingilia.

Ikiwa Mbowe atashinda hakuna mabadiliko yoyote ambayo CCM itafanya. Mbinu zitakazotumika zitakuwa zilezile walizotumia kwa Miaka 20 kwani Mbowe ndiye yuleyule wanayemjua na ambaye wanauzoefu wa Miaka 20 kujipigia kama punch bag

Ikiwa Lisu atashinda, inatarajiwa CCM kubadili baadhi ya Mbinu na mikakati na hii italeta mabadiliko ya Kisiasa kwa kiwango Fulani.

CCM itabidi ijipapasa kuibua Akiba na Kete zake zenye makada wenye uwezo unaoendana na LISU.

Tunatarajia, siasa za kiitikadi kurejea. Zile siasa maslahi au siasa biashara zinaweza kupotea kwa Kipindi hiki. Maana Lisu ataweka Safu ambayo inaitikadi ya CHADEMA Halisi hakuna CCM nayo itaweka makada wenye itikadi ya kiccm. Ile ya Nyerere
Hapa katikati vyama vyote Itikadi Zao zililegalega na Siasa ilikuwa kama Ajira au biashara Fulani hivi.

Machawa nafasi yao itatishwa kwa Sababu machawa ni matokeo ya siasa biashara. Wao wapo sio kwa kile wanachoamini kwenye chama husika Bali wpo kwaajili matumbo Yao.

Watu wengi wapenda mabadiliko waliopo pande zote. CCM, CHADEMA na vyama vingine wanaombea Lisu ashinde ili kubadili uelekeo WA siasa za nchi Zetu

Tupo!
Ndio maana Lucas Mwashambwa anahofu sana.
 
Ina maana hizo mbinu wataanza kuwafukuza wala Rushwa na majizi serikalini ama?
Sidhani kama Africa itakuja kubadilika maisha
Kuna nchi zimefanya rushwa kama moja ya katiba ya nchi na hata aje nani
Kuna watu mnaweza kumuona muokoa jahazi anakuja lakini mkumbuke rushwa bado ipo na watu hubadilika au kuwa dhaifu kwa mambo ya pesa
Kuna wengine hupitiwa kwa wanawake warembo na wengine kupitia ubia na hata matajiri wakubwa wana mbinu zao za kuwashawishi viongozi
Tusubiri tuone kama watamaliza rushwa na wizi
 
Hili bandiko lina lengo la kuwatisha kina Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable comte ....
Gentleman,
mimi pamoja na wachambuzi wataalamu wabobevu wa mambo ya siasa za Tanzania ulowatag,

hatuhusiki kwa namna yoyote na mambo ya ndani ya chadema ispokua tunafafanua, tunachambua na kuelezea mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea ndani ya chadema kadiri yanavyojitokeza kwa faidi ya wadau wa JF.

as professional political analysts in Tz, we have nothing to lose or gain as far as chadema elections is concerned, right?🐒
 
Akili mgando hizi kwa mtu unayeonekana ni intellectual siyo sawa hata kidogo.
Hana akili huyo!

Anajua mamlaka ya mwenyekiti ni yapi na ya kaimu ni yapi?

Ameisoma katiba ya Chadema na kufahamu mamlaka ya hao wawili ni yapi?

Mimi sina chama ila kuna watu wana reason kindezi sana. Sisi wengine ni wapenda haki.

Tatizo ni nini? Ni uchawa au ukosefu wa akili?

Akaangalie interview ya jana ya Salim Kikeke na Lissu. Lissu amejibu jawabu la huyo asiyetaka kufikiri dokta uchwara.
 
Back
Top Bottom