Lissu akiwa Sengerema apigilia msumari wa "akili matope" kwa Rais kuwapa DP World madaraka yake kama mdhamini wa ardhi

Lissu akiwa Sengerema apigilia msumari wa "akili matope" kwa Rais kuwapa DP World madaraka yake kama mdhamini wa ardhi

Masikini Crocodiletooth...Masikini Tanzania...in fact and to be truth, wow! Halafu ukute eti wewe ndio unapitia hivyo vipingele, utaelewa kitu kweli?

Na ukishafanya hivyo huna haki yoyote ile ya kumpa tena masharti kwani tayari wewe ni mtumwa. Kila hitaji lako lazima utatakiwa kuomba kibali.

Kwa uwezo wako kilugha, hata kama kipengele hicho kipo huwezi kukiona. In fact and to be truth imekuumbua uwezo wako...hebu epuka mijadala ya aina hii, ukimya wako pekee utakusetiri!

NB: Waliokupa likes labda ndio hao hao walituingiza katika huu mkataba wa hovyo.
Mkuu za Siku huyo ni kanjanja
 
Ni kuhusu kipengele cha mkataba kinachosema Rais akitaka kujenga chochote karibu na maeneo ya DP World kama vile hospitali karibia na bandari ya Isaka basi atatakiwa kwanza kuomba kibali cha DP World. Wakati Rais huwa ndio anaeombwa ardhi, sio yeye kuomba.

Tundu akauliza hii ni akili au matope? Wananchi wakaitikia "Matopeeeeeeee....."

Haya Waziri Nape, pitisheni kipira mkamate wananchi wote walioitikia matopeeeeeee!

Mweee mh lissu wapunguzie spana,ccm wanatafutana huko , mzee Wasira yupo uvunguni mwa kitanda, namshitaki tena kwako ebu mpige nyundo tena atoke uvunguni
 
Sasa wewe hapa unabwabwaja kitu gani, mbona hueleweki?

Hiyo lugha ya "in fact and to be truth" ni lugha gani hiyo. Ulilazimishwa kutumia lugha usiyoijua?

Kwanza haiongezi chochote cha maana katika uliyoandika baada ya maneno hayo.

"...rais kwenda kuomba kwa mwekezaji ili kutekeleza hata miradi ya watu wake..." Ni vipengele gani hivyo unavyozungumzia wewe. "Miradi ya watu wake". Watu wake ni akina nani hao, shemeji zake huyo rais?

Uandishi wa hovyo sana huu unaoonyesha upungufu mkubwa katika mfumo wa elimu yetu.
Nakushauli mngechutama tu na rais wako, maana mnazidi kuvuliwa nguo
 
Hii kandanda sijui itaishaje Ila inasikitisha Sana! kulitakiwa busara ndogo Sana toka CCM ili kuahirisha hii mechi,lakini wakaamua Ngoma iwekwe uwanjani ndio hasara zake hizo ni kukubaliana nazo tu hamna namna, nasikia mwingine anataka kumfirigisa mwambikusi!

Maajabu! wakati anawaambia Kila Leo amehesabu ghalama, wanaona la kumyumbisha kikazi ndio suruhisho kweli?

Hawaoni Kama wanatengeneza tatizo kubwa kisiasa then wanataka Tundu mwingine uwanjani? Kwani hawajui akikosa kazi atarudi uwanjani muda wote? Pole zao
Serikali ya CCM imepofushwa, haisikii la mnadi swala wala la mwazini, kuna jambo linakuja mbele nadhani si zuri kwa mstakabali wa hichi chama, Wananchi wamegoma kabisa kuelewa suala hili la bandari na bado SISIEM wamekomaza shingo, TUSUBIRI.
 
Masikini Crocodiletooth...Masikini Tanzania...in fact and to be truth, wow! Halafu ukute eti wewe ndio unapitia hivyo vipingele, utaelewa kitu kweli?

Na ukishafanya hivyo huna haki yoyote ile ya kumpa tena masharti kwani tayari wewe ni mtumwa. Kila hitaji lako lazima utatakiwa kuomba kibali.

Kwa uwezo wako kilugha, hata kama kipengele hicho kipo huwezi kukiona. In fact and to be truth imekuumbua uwezo wako...hebu epuka mijadala ya aina hii, ukimya wako pekee utakusetiri!

NB: Waliokupa likes labda ndio hao hao walituingiza katika huu mkataba wa hovyo.
NINGELIKIKOSEA KISWAHILI NINGESIKITIKA SANA,LAKINI KWA HII LUGHA YA WATU SIONI SHIDA.
 
Mwanzoni nilimlaumu sana Lissu.
Lakini nimetafakari sana haya maneno naona yana gonga kichwa!
Ila ccm mlichokifanya hapana! hapana! mbona wizi mmefanya sana hamridhiki?
 
Infact and to be truth,"angalieni tena upya baadhi ya vipingele,rais kwenda kuomba kwa mwekezaji ili kutekeleza hata miradi ya watu wake si sawa,endapo kama ni kweli kipo kipengele hicho Ndani ya mkataba"
Nadhani hata Shivji ulimsikia akisema "Rais amejipoka madaraka yake".
Hata suala la usalama wa anga maeneo yanayozunguka Bandari lazima Kwanza tumuulize Bwana Mkubwa DP World kama yuko tayari tuweke miundombinu ya kiusalama.
 
Mwanzoni nilimlaumu sana Lissu.
Lakini nimetafakari sana haya maneno naona yana gonga kichwa!
Ila ccm mlichokifanya hapana! hapana! mbona wizi mmefanya sana hamridhiki?
Yaani wewe Rais wa inchi umuombe muwekezeka ruhusa ndani ya ardhi yako? Magufuri asingefanya huu ujinga
 
Nakwambia kipindi hiki angekuwepo mch. Mtikila na ile bendera yake ya Tanganyika, pasingetosha.
 
kinachouma zaidi, DP WORLD wameingia mikataba na nchi nyingine nyingi duniani, zaidi ya hamsini, lakini wote wameingia mikataba ya akili, hakuna mkataba wa kijinga kama wa Tanganyika. walipokuja kwetu wameamua kuingia mkataba wa kijinga kwasababu walituona sisi wajinga na mamburura. wametudharau sana kuliko nchi zingine nyingi walizoingia nao mikataba, wameona Tanganyika ni kilaza. hivi kweli unataka kuniambia the same type of mkataba kama huu wameingia nao Waingereza? au nchi nyingine yeyote, au kwetu tu wameona mtelezo?
 
Hivi kampuni zote za nje zinazopewa tender nchini zina IGA kwenye kila tender? kwa nini hao DP world wanataka walindwe na IGA badala ya mkataba baina yao na TPA? hiyo IGA ni utapeli wa kiuwekezaji uliochagizwa na rushwa nono kwa walamba asali wanaosukumwa na ubinafsi kuliko maslahi mapana ya taifa.​
 
umeongea ya maana sana. plus hilo, najiuliza, aina ya terms za mkataba walizoingia nazo kwenye mataifa mengine ndio kama hizi walizoingia na sisi au wameona sisi mambumbumbu wakatuletea za aina hii? hii si dharau na matusi hii,wametuonaje yaani? wameona sisi mteremko kuliko waingereza walioingia nao na nchi zingine, wakatudharau na kuingia na sisi mkataba wa kijinga na bado kuna wasomi na wanaccm wanaupigia debe hadi kesho. kweli pesa tamu. zinaweza kukufanya ukawa kipofu kabisa.
 
Sisi wengine wenye akili huru tumemuelewa. Ningeshangaa sana kama na wewe mtumwa wa Waarabu ungemuelewa
EeeenHeeeee!

Wewe kweli ni "Mkojo" hasa!
Huoni ulivyopotea badala ya kuwa chooni unakuja kuchafua hali ya hewa bila kujua kilichoelezwa?
 
Infact and to be truth,"angalieni tena upya baadhi ya vipingele,rais kwenda kuomba kwa mwekezaji ili kutekeleza hata miradi ya watu wake si sawa,endapo kama ni kweli kipo kipengele hicho Ndani ya mkataba"
Mnang'ang'ana na lugha ngeni na hamuiwezi,hapa unawasiliana na waswahili wenzio,viingereza vya nini!?
 
Back
Top Bottom