Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 648
- 1,485
Kwa mujibu wa muongozo wa watia nia wa nafasi mbalimbali wa CHADEMA wa mwaka 2012, Mtiania kwa nafasi ya Urais anapaswa kutangaza nia yake katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja kabla ya tarehe ya Uchaguzi.
Muongozo huu uliandikwa ili kumdhibiti Zitto Kabwe ambaye mwaka 2010 wakati Dr Slaa anagombea Urais yeye akiwa Kigoma akatangaza kugombea Urais 2015. Sasa wakubwa wakaamua kumdhibiti mapema.
Mwaka 2013 Zitto akaingia kwenye mgogoro baada ya kunaswa kwa mkakati wa mabadiliko 2013 ulioandikwa na Mwigamba, Kitila na Waitara na mimi kwa mbali kidogo.
Sasa Mh. Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ametangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2017, 2018, 2019 na 2020 katika matamko yake mbalimbali na mikutano na waandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
Sasa kamati kuu hii ya CHADEMA ambayo iko chini ya Mbowe ambaye pia nia yake ya kuutaka Urais imeonekana kwa vitendo mara zaidi ya maneno itampitisha Lissu? Hawawezi kumpitisha. Nia wanayo na sababu wanayo
Nilisema kuwa mgogoro unaofuata CHADEMA sasa ni kati ya Mbowe na Lissu! Huu ndio utakuwa hatma ya Chama hicho au ufufuko wake. Muda utatuambia.
Mimi naamini Lissu atagombea kwa tiketi ya NCCR