didy muhenga
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 861
- 1,476
DJ niwekee ngoma ya Rema "hehe"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesema sahihi Mkuu, nadhani yeye pia ameshajijua.Lisu pale CDM ni Sawa na kondoo aliyezingirwa na mbwa mwitu, kila mmoja anatamani kumtafuna
lisu ni ukweli sio ufitini
lisu ni mfitini wallah
AhahaahahahKumbe wenje ni mpuuzi kiasi hicho.
Shida yake hajui, mipaka.Fitina ndio njia kuu za siasa, hujui tu hata hilo
It is too late to catch a moving truck 🤣Wakuu,
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara na 'mgombea' wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu amewashukia wale wote wanaodai kuwa miongoni ya watu wanaomuunga mkono katika kinyang'anyiro cha kutafuta nafasi hiyo ni wale ambao mara zote amekuwa akiwatuhumu kuwa wanajihusisha na vitendo vya rushwa ndani ya CHADEMA
Akizunguma na wanahabari kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam Desemba 18.2024 ikiwa ni muda mfupi baada ya kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa katika mchakato wa ndani wa uchaguzi unaoendelea Lissu amesema amekanusha vikali madai ya kuungwa mkono na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe: Nitatoa uamuzi wa kugombea Uenyekiti siku ya Jumamosi saa 5 asubuhi
Amesema miongoni mwa wale anaowatuhumu mara kwa mara kujihusisha na vitendo vya rushwa mmoja wapo ametangaza dhamira ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (ingawa Lissu hajabainisha kama mgombea huyo anatokea upande wa Tanzania Bara au Zanzibar), na kwamba mtu huyo ametangaza hadharani kuwa anamuunga mkono Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe katika mchakato huo (ingawa Mbowe mwenyewe ameahidi kutoa msimamo wake ndani ya saa 48)
Aidha, Lissu ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa mtu huyo (anayemtuhumu) ndiye aliyemfuata nyumbani kwake (Tegeta, Dar es Salaam) akiwa ameambatana na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja la 'Abdul' ambapo wawili hao walifika kumshawishi apokee rushwa, na kwamba walitumia nafasi hiyo kumueleza watu wengine ndani ya chama hicho waliofikiwa na 'Abdul' na 'kuchukua chao', lakini Lissu aliwakatalia
"Mtu aliyemleta Abdul nyumbani kwangu kuja kunihonga anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama, na amesema kwa maneno yake mwenyewe kuwa anamuunga Mwenyekiti (Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) mkono, sasa hao wanaosema niliowasema mimi (kuwa wanajihusisha na rushwa) na wananiunga mkono ni kina nani?, ninajuwa aliyemleta Abdul nyumbani kwangu anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama na amesema anamuunga mkono Mwenyekiti, maana yake mimi najuwa aliyeniambia amepewa hela na Abdul na aliyeniambia wengine waliyepewa hela na Abdul, na ndiye aliyemleta Abdul nyumbani kwangu na ndiye mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama, huyo ambaye mimi nimemsema na ananiunga mkono ni nani?" -Lissu
Taratibu mtaanza kuelewa sasa nyuzi za Pascal Mayalla juu kirusi kilichopo ndani ya chadema.Mbowe anaweza kuwa ni mmoja wa hao waliopewa hela na Abdul ndio maana Lissu anasita kuwataja. Lakini naamini iko siku atawataja.
Lissu alipigwa risasi na MboweIt is too late to catch a moving truck 🤣
atasema yote but it will not help him at all.
Political mistakes na blunders alizofanya Lisu ni pamoja na hiyo ya kuogopa kuwataja anao watuhumu kwa rushwa at first place.
saivi anaonekana anatapatapa tu kama mfa maji 🐒
Hata Mbowe ni mpuuzi sana, naona mwisho wa kuwadanganya Watanzania umewadiAKumbe wenje ni mpuuzi kiasi hicho.
Ninakuunga mkono, Mbowe amecheza na akili za Watanzania muda mrefu sanaTaratibu mtaanza kuelewa sasa nyuzi za Pascal Mayalla juu kirusi kilichopo ndani ya chadema.
Ndio mtaelewa kwamba sasa hata ile sign ya kwenye barua ya kuwaidhinisha kina Mdee kule bungeni haikufojiwa kama tulivyoambiwa.