PreGE2025 POTOSHI Lissu amesema wataandamana siku ya uchaguzi kuuzuia

PreGE2025 POTOSHI Lissu amesema wataandamana siku ya uchaguzi kuuzuia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya ‘No Reforms, No Election’ (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu ‘No Reforms, No Election.’

Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

“Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya kupiga kura tutaandamana, watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?” amehoji.
1744104006385.png
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), hivi karibuni amekuwa na ziara akifanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali ambapo awali alianzia kanda ya nyasa jijini Mbeya lengo kuu likiwa ni kueneza ajenda ya 'No Reforms, No Election' kwa wananchi juu uhitaji wa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.

Mnamo mwezi Aprili 7, 2025 Lissu alifanya mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza na kufafanua ajenda ya ‘No Reforms, No Election' kwa wananchi wilayani humo.

Madai

Kumekuwapo na taarifa iliyoripotiwa katika mitandao ya kijamii kuwa Lissu amesema wataandamana siku ya uchaguzi na kuuzuia

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck uliorejea hotuba ya Lissu ya Aprili 7, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani ya Masasi mkoani Mtwara, umebaini kuwa taarifa hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwani Lissu hakusema wataandamana siku ya uchaguzi kuuzuia usifanyike, bali alisema uchaguzi hautafanyika kama wananchi watakubaliana na msimamo wao kuzuia uchaguzi

Aidha alisisitiza kuwa Uchaguzi hautafanyika kwa kuwa Lissu amesema bali wananchi wakisema 'uchaguzi huu hautafanyika, hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya uchaguzi tutaandamana'

Katika hoja hiyo Lissu alianza kwa kusema "Nani anayataka kuendelea na mateso ya CCM mpaka Kiama? Ndio maana sisi CHADEMA tunasema, kama hawataki mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi, tuzuie uchaguzi usifanyike,"

"Uchaguzi hautafanyika kwa sababu Lissu amesema tu! Hautafanyika kama wananchi wa Masasi na Watanzania wote mkikubaliana na msimamo wetu na kusema: uchaguzi huu hautafanyika, hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, na siku ya kupiga kura tutaandamana. Watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?" amehoji.

View: https://www.youtube.com/live/1HYOTIwAb2M?t=6394s​
Back
Top Bottom