Lissu ameshamshinda Mbowe!!

Lissu ameshamshinda Mbowe!!

Ndio Lissu ameshamshinda Mbowe kwenye kuropokaropoka !
Lakini kwenye uongozi hamfikii hata nusu !
We unadhani kama Mwamba angepigwa kama risasi vile , Lissu angeweza kumpeleka Nairobi ???
Mwamba akili kubwa wewee !
 
Mimi napenda Lissu ashinde.Lakini naelewa mazingira ya kushinda Lissu ni magumu.Hapo uliposema wenyeviti wa kanda 7 tu hawawezi kuamua mwenyekiti ingeeleweka zaidi kama ungechambua wajumbe wote wa mkutano mkuu na namna wanavyoweza kuathiri na kuchagua mwenyekiti wa chama Taifa.Composition ya kamati kuu ni
i)wajumbe wote wa baraza kuu
(ii)Wenyeviti wa chama wilaya/majimbo
(ili)Makatibu wa chama wilaya/majimbo
(iv)Wabunge wa JMT
(v)Wajumbe 20 wa kuteuliwa
(vi)Mjumbe mmoja wa kuteuliwa kila wilaya

Ukiangalia kwa makini hii composition unaelewa kabisa kuwa huyo fisadi Mbowe ameshajiwekea mizizi kuanzia wilayani......Mfano hao wajumbe wa kuteuliwa kutoka kila wilaya unadhani sifa kuu yao ni ipi kama sio kuwa pro incumbent?Kuna wilaya ngapi?Bado hao 20 wa JMT.Hapo bado hujagusa turufu kuu ya incumbent ambayo ni baraza kuu.Kuna wabunge 19 wale ni wapiga kura pia...unadhani watamuacha Godfather wao?

Hivyo basi hoja yako namba moja yapaswa kugusa kura za hao wajumbe wote wa kamati kuu na si vinginevyo
Mkuu, ina maana na hawa Covid 19 wanapiga kura? Kwani wao ni wanachama wa CHADEMA? Tufahamishane!
 
Hii itakuwa ni scenario mpya kwa wapigakura hawa waliokataa kuwarudisha wenyeviti wa Kanda waliodumu kwa miaka mitano tu lakini wewe utegemee wapigakura haohao waje wakuchague wewe uliyekaa madarakani kwa miaka 20.

Sasa kwa utafiti huu wa kisayansi kabisa tayari Mbowe ameshapigwa kabla hata ya Uchaguzi.
Hili likitokea,manyumbu akili za nyumbu zitakuwa zimewatoka akili za binadamu zimewarudia。
P
 
Lissu ameshaenda ulaya.

Atashinda saa ngapi?
Hii sio dunia analogia boss. Dunia hii ya techology aliyeko New York yuko karibu kuliko aliyeko kwa mtogole. Ccm ndio bado wanaishi kinaanalogia, unakuta kiongozi anasema anakwenda kuongea na wananchi wake, lakini kiuhalisia unakuta haongei nao bali anawahutubia atakacho.
 
Miaka 21 na huna hata kijiji unasema unataka kuendelea kuongoza
Usichanganye uchu wa madaraka wa Mbowe, na chaguzi za kishenzi zinazoendelea hapa nchini. Tunajua udhaifu wa Mbowe ni upi, na ukhanithi wa kwenye chaguzi zetu ni upi. Usidhani hatujui kipi ni kipi.
 
Aibu kuu, mpinga ufisadi naye awa fisadi.

Lisu haihitajiki afanye kampeni Kama wajumbe Wana akili timamu.
Tetesi za ndani uchaguzi huenda usiwe Uhuru. Mjumbe akipiga kura atajipiga picha ili akitoka akapokee kitita Cha pesa sio chini ya milioni moja!!

Tunashauri wajumbe wakae nyuma ya mgombea ili tuwajue wajumbe ambao husema tupo pamoja kumbe wanafiki.

Tuache utani kumpigia MBOWE kwa Sasa ni kuua chadema
 
Hivi mbowe na watu wake huwa hawasomi mitandaoni aone jinsi asivyotakiwa kugombea tena? Anashupaza shingo huku anaona kabisa hatakiwi tena kuwa mwenyekiti. Kama si dikteta ni nani kung'ang'ania madaraka huku hatakiwi?
Kwani kura zinapigwa mitandaoni?
wapiga debe wamihemko ndio wanao taka lissu. Hawo wote huenda siwanachama.

wanachama ndio wanao taka Mbowe aendelee.
 
Kwakutumia Elimu yangu ya Sayansi ya siasa Leo natoa facts tatu (3 ) tu kuonesha tayari Lissu ni mshindi hata kabla ya kura,

1. Uchaguzi wowote ni namba mpaka sasa kundi linalomuunga mkono Mbowe ni tabaka la juu tu la Viongozi hasa wajumbe wa Kamati kuu kutoka Kanda ambao hesabu yao hawaizidi watu Saba (7 ),

Mbowe lazima atambue ni kosa kudhani Kwakuwa anaungwa mkono na wenyeviti wa Kanda automatically utaungwa mkono na walio chini yao jibu ni HAPANA,

Mbowe kwa utulivu kabisa lazima akumbuke hakuna Mwenyekiti yoyote wa Kanda anayemuunga mkono aliyechaguliwa kwa mara pili swali ni kwanini? Jibu Wapigakura hawa wanataka Uongozi mpya kuanzia chini mpaka juu kabisa.

Tujiuluze kwa polepole kabisa huyu Mbowe anayeomba kuchaguliwa kwa mara ya tano mfululizo na wajumbe wale wale waliokataa kurudisha Wenyeviti wa Kanda waliohudumu miaka mitano tu akiwemo Peter Msigwa,Kisayansi nikisema hata yeye hawatamchagua nakosea?
Jibu ni HAWATAMCHAGUA PIA.

Hii itakuwa ni scenario mpya kwa wapigakura hawa waliokataa kuwarudisha wenyeviti wa Kanda waliodumu kwa miaka mitano tu lakini wewe utegemee wapigakura haohao waje wakuchague wewe uliyekaa madarakani kwa miaka 20.

Sasa kwa utafiti huu wa kisayansi kabisa tayari Mbowe ameshapigwa kabla hata ya Uchaguzi.

2. Mbowe amepoteza imani kwa wapigakura wake hasa baada ya kusema maridhiano yamenunua Ofisi ya bilioni 1 kama Mafanikio wakati madhila wanayopitia wapigakura hawa ni makubwa nadhani kuliko kiasi chochote Cha fedha hivyo wapigakura hawezi kuchagua Ofisi na pesa ambazo hata haziwafikii watachagua zaidi hatma ya Uhai wao na hatma za wanaowaongoza ila kamwe hawezi kuchagua pesa na mali.

3. Kashfa za rushwa, Ufisadi na kulamba asali haya mambo ni mwiko na taboo kwa CHADEMA, Kwa tetesi zote hizi Mbowe haaminiki tena kwa wadau wa maendeleo wa CHADEMA wandani na nje ya nchi hivyo kumchagua Mbowe ni kufunga kabisa milango yote ya misaada kutoka kwa wafadhili na wahisani wa CHADEMA hivyo Mbowe tayari ameshapigwa kabla ya Kupigwa na kwa tetesi za yeye na team yake kuanza kugawa pesa kwa wajumbe ni kielelezo kingine namba 4 kwamba Mbowe huyu si yule wa miaka yote na utamaduni wa kuhongana si Utamaduni Wala msingi wa CHADEMA ya Mtei Wala Ile ya Bob Nyanga Makani.

×××××××

Naamini degree yako ya siasa ilisup mkuu
Jitahidi ujue inner circle za CDM
 
Back
Top Bottom