Pre GE2025 Lissu amwambia Balile "Maswali yako ni Nonsense"

Pre GE2025 Lissu amwambia Balile "Maswali yako ni Nonsense"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Balile ni kada wa ccm,
Serikali ilitanguliza kupeleka wahariri Dubai ili wakajifunze ufanisi wa wenzetu katika operation za bandari.
Hapo ni mapema sana kabla mambo ya DP world hayafahamika nchini.

Nakumbuka baada ya kurejea nchini, Balile aliandika article ndeefu sana kusifia technologia za wenzetu kwenye Gazeti la Jamhuri.

Wakati mjadala wa Dp world umetrend nchini.Balile hakufumbua mdomo wake kukoment chochote kama bosi wa wahariri.....nimeunganisha dots
 
Serikali ilitanguliza kupeleka wahariri Dubai ili wakajifunze ufanisi wa wenzetu katika operation za bandari.
Hapo ni mapema sana kabla mambo ya DP world hayafahamika nchini.

Nakumbuka baada ya kurejea nchini, Balile aliandika article ndeefu sana kusifia technologia za wenzetu kwenye Gazeti la Jamhuri.

Wakati mjadala wa Dp world umetrend nchini.Balile hakufumbua mdomo wake kukoment chochote kama bosi wa wahariri.....nimeunganisha dots
Hoja za DP zilikuwa za kisheria zaidi ambazo hawezi kuzidadavua hivyo aliamua kuufyata!
 
Ni kweli wahariri wa media za Tanzania wajifunze kuacha uchawa kwa maswali yasiyo na uhalisia ya yanayoendelea katika siasa za Tanzania

Al Jazeera Mehdi Hassan akimbana kiongozi wa walio wabunge wenye wa bunge la Jamhuri ya Kenya, hapa wanahabari nguli wa Tanzania wanaweza kujifunza ... badala ya kukata nonsense katika mijadala


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZSIA7ZB9i00
 
Balile na Paschal ni makada wa CCM waliojificha kwenye mwanvuli wa Uandishi wa habari, kuwashirikisha hao kwenye jambo la demokrasia na mabadiliko ni kupoteza muda wako tu.
Pascal Huwa anasimamia Haki,Labda kuogopa kuonekana hajui kusimamia Haki,Kwa kuwa kwenye Sheria nae Yuko vizuri!
 
Maswali ya hovyo ya Balile katika mkutano wa Chadema na wahariri wa vyombo vya habari yapelekea kuambiwa anauliza nonsense jambo ambalo limemkera sana na kuanza kutafuta kanuni za mkutano.

Balile ambaye ndiye alikuwa anaongoza mkutano huo alitumia muda mwingi kuvuruga mkutano badala ya kusikiliza hoja za Mh. Lissu.

Soma, Pia: Balile kutetea Serikali mkutano wa Waziri Mbarawa anathibitisha bahasha zimepita kwa Waandishi wa Habari?

Kutokana na Balile kuongoza vibaya mkutano huo umepelekea wahariri wengi kukosa muda wa kuuliza maswali.
View attachment 3255988
Zaidi ya miaka 12 wakati naanza kupita kwenye jukwaa hili, kulikua na misemo common sana humu dhidi ya Tasnia ya Habari na Wanahabari.

Mosi, Media( Tasnia ya Habari) ni mhimili wa nne.

Pili, Bahasha za kaki. Kwamba, waandishi wengi wanaishi kwa bahasha za kaki.

Kwa kusema hivyo, Alichokifanya Balile, kinadhihirisha kuwa, Tasnia ya habari si muhimili tena wa nne otherwise, muhimili huu unaharibiwa sana na bahasha za kaki .
 
Katika mjadala wa kisiasa unaoendelea kuhusu uchaguzi wa mwaka 2025, Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amejikuta kwenye wakati mgumu aliposhindwa kutetea hoja yake ya "No Reforms, No Elections" (Hakuna Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi).

Lissu, ambaye amekuwa mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, alipata wakati mgumu wakati wa mahojiano na vyombo vya habari alipoulizwa swali la msingi: "Ikiwa serikali haitafanya mabadiliko mnayoyataka, je, CHADEMA haitashiriki uchaguzi wa 2025?"

Ukwepaji wa Swali na Ukimya wa Lissu
Badala ya kutoa jibu thabiti linaloendana na msimamo wake wa muda mrefu, Lissu alikwepa swali hilo na kuanza kuzungumzia masuala mengine yasiyohusiana moja kwa moja na swali aliloulizwa. Hatimaye, aliamua kususia swali hilo kwa kukwepa kujibu moja kwa moja kama chama chao kitasusia uchaguzi au la.

Tabia hii ya ukwepaji wa maswali muhimu imeibua mjadala miongoni mwa wachambuzi wa siasa na wanaharakati wa demokrasia. Wengi wanaona kuwa kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections" ilikuwa zaidi ya mbinu ya kisiasa isiyo na mkakati wa utekelezaji.

Mabadiliko Yaliyo Fanyika na Ukweli wa Siasa
Licha ya madai ya Lissu na CHADEMA kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika, ukweli ni kwamba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mabadiliko kadhaa katika mifumo ya kisiasa na uchaguzi. Mfano ni kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara bila vikwazo, hatua ambayo imesifiwa hata na viongozi wa upinzani waliokuwa wakilalamikia zuio hilo katika awamu iliyopita.

Swali linalobaki ni: Je, CHADEMA iko tayari kususia uchaguzi wa 2025?
Kama msimamo wa Lissu unavyoonyesha, hakuna uhakika wowote wa kususia. Badala yake, inaonekana kauli mbiu hiyo ni mbinu ya kushinikiza bila dhamira halisi ya utekelezaji.

Kwa hali ilivyo sasa, upinzani unapaswa kutathmini upya mkakati wake na kuwa na msimamo thabiti unaoeleweka kwa wanachama na wafuasi wao badala ya kutumia vitisho visivyotekelezeka vya kususia uchaguzi. Wakati ukifika, ni wazi kuwa CHADEMA italazimika kushiriki katika uchaguzi, hata bila mabadiliko wanayoyataka, jambo linaloifanya kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections" kupoteza maana.
 

Attachments

  • 3bbb9350-6c8a-49b5-8fc1-067534c76a8e.mov
    1.7 MB
Yaan wewe ni Lucas mwashambwa.

Hizi Sheria za kihuni mlizobadilisha.

Anyway endeleeni kututawala paka mchoke
 
Hivi Balile bado una amini ulikuwa unauliza maswali ya maana?

Hilo nonsense lilikuwa jibu la kistaarabu sana! Wangekuwa wengine ungetukanwa kabisa.

Alafu umeshajifunza kuwa hakuna Sheria iliyo juu ya Katiba? Au ndo unajiliwaza kwa huu ujinga wako?😅😅
 
Mbona Makamu wake Heche alishasema hawatashiriki kama marekebisho yasipofanyika?

Au Bado utaratibu ni ule ule aliasisi Lissu kuwa Kila Kiongozi anaongea lake huko CHADEMA?
 
Back
Top Bottom