Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Akiwa mjini Tunduma, Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini, ameongea na maelfu ya wananchi.

Amezungumza kuhusu hali ya uminywaji wa Vyombo vya Habari nchini, watumishi wa umma kutopewa maslahi yao ipasavyo, kero za wafanyabiashara ndogondogo hususan vitambulisho vya wamachinga vya sh 20000, Viongozi wa dini ya waislamu walioko jela kinyume cha haki, uonevu dhidi ya vyama vya siasa, kero ya wafanyabiashara kubambikiziwa kodi na TRA na kusema kuwa watavikomesha hivyo october 28.

Na pia, akampiga kijembe Rais Magufuli kuwa badala ya kuhangaika kuweka bando la internet ili kuwatazama wapinzani kwenye WhatsApp, afungulie vyombo vya habari ili awaone kupitia vyombo rasmi vya habari.

Hapo Tunduma OCD wa sehemu hiyo alijaribu kuwazuia wananchi kwenda mkutanoni, lakini alishindwa kuwathibiti wananchi maana walikuwa ni wengi mno.

Kwa taarifa zaidi muone yeye mwenyewe Tundu Lissu.

 
Hoja ya kijinga Lowassa aitumwa ila waka huu ni kamiligado
Mamluki wenu Membe kashtukiwa mapemaa 😁😁😁
Sawa mkuu. Nakusihi. Tuwe watulivu siku ya kupiga kura. Lakini tuamini asiyekubali kushindwa si mshindani. Wote sisi ni watanzania na watakao chaguliwa ni watanzania wenzetu. Tuwe watulivu na tuyapokee matokeo kwa njia ya amani. Atakaye fanya uvunjifu wa amani, atakutana na wahusika wa hizo mambo.
 
Back
Top Bottom