Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Hivi magufuri akianza kampeni atadunganya nini? sababu anachorwa ile barabara.
 
Ndio ruzuku iko inafika mpk nyingine tunazificha ndani ya kofia.View attachment 1542578
Ayeeeeeeeee
Ef0HiCTWAAwH6Nh.jpg
 
Ndugu acha kumfananisha Lissu na lowassa huyu bwana ni mpinzani kweli,tena haogopi mtu,hatafuni maneno ni mkweli ni mwadilifu tofauti na lowassa aliyekuwa mwoga na mwenye doa kubwa la ufisadi,hoja tu ya ufisadi ilikuwa pigo kwa upinzani lakini watu kwa kuichoka ccm walimpa kura zaidi ya mil 6.

Ndugu huu mwaka ni tofauti lisu anauzika lisu anajiamini, ccm imechokwa na wakulima mf wa korosho,vijana hasa wahitimu vyuo, watumishi wa umma walionyanyasika miaka 5 bilakuongezwa mishahara na kudharirishwa ovyo, wafanyabiashara mpaka wengine wamejinyonga mf yule wa viroba Dodoma, ndugu ccm ijipange uchaguzi huu sio kama miaka mingine watu wanajitambua mtampinga lissu kwa hoja gani mtu makini na mwadilifu na pia yeye ni alama ya uonevu kwa kupigwa risasi za kutosha.

Pia tofauti na lowassa, lissu anakwambia hakuna kuibiwa kura.Ushauri wangu kwa chadema mwaka huu nendeni vijijini mjini tunajielewa tutawapa kura tu nendeni vijijini hata kwenye makao makuu ya kata mkaongezee tu kura ili waibe mpaka washindwe msijifurahishe na mafuriko ya mjini au gaweni timu vizuri,wengine wajikite mjini wengine vijijini.N.b mimi sina chama ila kura yangu kwa upinzani wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipimo kwamba watz wana akili timamu ni kuona kama watalichagua tena jinamizi ccm au watachagua uhuru wa kweli
 
Naona
Kuna watu wanajiandaa kuikimbia Nchi.
Naona.
Kuna binadamu wanafikiria kuishi uhamishoni,
Naiona Jera, namwona mtu Kifungoni.
Ni kilio na kusaga meno.
 
Lissu anajitahidi sana kuongea maneno ya kukera na kuudhi dhidi ya Rais Magufili, ...
...
Lakini ni muhimu wakati ukifika Lissu na umeshafika ni sasa aambiwe ukweli, wala msimdanganye hamna namna ataweza shinda uchaguzi huu. Hilo haliko, asiachiwe tu uwanja na kuangaliwa tu akiulaghai umma na mataifa mengine ya nje kuwa anakubalija na kesha shinda. ...

Kwangu mimi naona si sawa huyu aachiwe kuongea kila anachojisikia kuongea na kila anachotaka kuwaaminisha wale wanao msikiliza hata kama ni uongo na upotoshaji. Uongo ukaachwa kukanushwa na ukaendelea kuongelewa kwa kurudiwa rudiwa hugeuka na kuonekana ndio ukweli huo. Hivyo ni vizuri mbinu za kukabiliana na huyu anaye ongea kauli za kuandaa waasi watarajiwa akabiliwe mapema kabla ya kuanza kukumbuka shuka wakati kumesha kucha. Makosa haya yalifanyika awamu iliyopita kukatokea mapinduzi ya kutumia pambio la chama ingawa baadaye yalizimwa. Lissu si wakumchekea.

Hoja zako zinafikirisha na kufunua akili za WaTz kuhusu amani ya nchi hii. Wahenga walinena mdomo huumba na imeandikwa Mathayo 15:11 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.

Kwa angalizo lako naamini wamekusikia. Yawezekana Lissu ana agenda yake binafsi na si ya kuwa Rais wa nchi hii. Ni mtu kichaa anayeweza kutamka maneno kama ya Lissu kuomba ridhaa ya uongozi wa nchi.

Angalizo langu, muda mwafaka wa kudhibiti lengo lake haujafika kwa sababu hadi sasa ni mteule wa CHADEMA kama mgombea Urais. Kwa kuwa bado hajateuliwa na Tume ya Uchaguzi kama mgombea, yuko huru kutumia haki yake Kikatiba kuomba udhamini.

Labda cha kujiuliza ni je, jinsi anayotumia kuomba udhamini ni halali? WaTz wa sasa naamini wanajua pumba na mchele ukifikishwa mezani (yaani wakati wa kampeni kama atateuliwa na Tume ya Uchaguzi).
 
Akiwa mjini Tunduma, Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini, ameongea na maelfu ya wananchi.

Amezungumza kuhusu hali ya uminywaji wa Vyombo vya Habari nchini, watumishi wa umma kutopewa maslahi yao ipasavyo, kero za wafanyabiashara ndogondogo hususan vitambulisho vya wamachinga vya sh 20000, Viongozi wa dini ya waislamu walioko jela kinyume cha haki, uonevu dhidi ya vyama vya siasa, kero ya wafanyabiashara kubambikiziwa kodi na TRA na kusema kuwa watavikomesha hivyo october 28.

Na pia, akampiga kijembe Rais Magufuli kuwa badala ya kuhangaika kuweka bando la internet ili kuwatazama wapinzani kwenye WhatsApp, afungulie vyombo vya habari ili awaone kupitia vyombo rasmi vya habari.

Hapo Tunduma OCD wa sehemu hiyo alijaribu kuwazuia wananchi kwenda mkutanoni, lakini alishindwa kuwathibiti wananchi maana walikuwa ni wengi mno.

Kwa taarifa zaidi muone yeye mwenyewe Tundu Lissu.

Ili wananchi wasio elewa kinachoendelea Tanzania, Lissu asifanye mjadala wa hadhara na Rais Magufuli, ambaye siyo saizi yake, bali afanye na huyu hapa
 
Back
Top Bottom