Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Lissu hawezi kamwe kushinda uchaguzi Mwenye kiti CHADEMA hapo januari 2025, licha ya uchaguzi kuwa wa wazi. Sababu ni zifuatazo:
1) Sasa hivi, hii imekuwa ni vita kati ya CHADEMA kanda moja tu (asilia- Mbowe) na CHADEMA Tanzania iliyobaki (Lissu). Haitatokea kwa mazingira Lissu alivyojipambanua na kueleza kinaga ubaga matatizo ya ndani ya CHADEMA na yakawaingia wanachadema Tanzania, eti ashinde.
2) CHADEMA asilia itatumia nguvu zote - Ushawishi, uwezo wa pochi, ahadi, Uzee na Propaganda kuanzia tar 10/1 mpaka 20/1. Mambo yote yatamalizwa katika siku hizi 10, Mchezo utakuwa umekwisha. Wajumbe wa kutosha anaowaamini Lissu, watalainishwa na kumgeuka Lissu. Mlango kwa mlango, jimbo kwa jimbo.
3) Hao anaowaamini Lissu na kupendekeza wawemo badala ya wazee wa chama, wakiwemo viongozi wa dini, atashangaa kuona, hao wote watamgeuka kwa kile kinachoitwa maslahi mapana ya chama/nchi.
4) Tar 21/1 uchaguzi utakuwa huru, haki na wa wazi kwa asilimia 150%, ili kuwahakikishia wanachadema, team Lissu na watanzania wote kuwa Lissu kashindwa kihalali: Vyombo vya habari vyote maarufu vitakuwepo na kamera zao mwanzo mwisho mpaka matokeo. Hata BBC, DW n.k vitakuwepo
Lissu ajiandae kisaikolojia baada ya kushindwa uchaguzi wa 21/1, kwani hapo ndio kwa mara ya kwanza ataelewa kuwa hiki ni chama cha kikanda, kikitetea maslahi ya kanda na kina malengo ambayo Lissu hayajui.