Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Moja ya taarifa kubwa iliyotikisa vyombo vya habari mwaka huu ilikuwa ni kukamatwa kwa Rais wa Venezuela, bwana Nicolás Maduro na vikosi vya Marekani tarehe 3 Januari 2026, huko Caracas, Venezuela, katika operesheni ya kijeshi iliyoitwa Operation Absolute Resolve.
Ingawa tarehe 5 Januari 2026, Maduro alifikishwa katika mahakama ya shirikisho Manhattan, ambako alishtakiwa kwa mashtaka ya narcoterrorism na cocaine trafficking; kauli na matendo ya Marekani yanaashiria kitu kingine tofauti kabisa ambacho ni mafuta.
Venezuela ina akiba kubwa sana ya mafuta duniani. Kwa miaka mingi Marekani ilikuwa soko muhimu sana la mafuta yake. Lakini kadiri mahusiano kati ya Washington na serikali za Hugo Chávez na baadaye Nicolás Maduro yalivyozidi kuwa mabaya, Venezuela ilizidi kuelekeza mahusiano yake ya kiuchumi na kisiasa kuelekea China na Russia.
China haikuwa mnunuzi wa kawaida tu. Iliikopesha Venezuela mabilioni ya dola, huku sehemu ya madeni hayo ikilipwa kupitia mafuta. Kufikia Aprili 2019, China ilikuwa inapokea takribani mapipa 337,000 kwa siku—karibu theluthi moja ya mauzo yote ya mafuta ya Venezuela wakati huo—na kampuni ya serikali ya China, CNPC, ilikuwa miongoni mwa wateja wakubwa wa PDVSA.
Mwaka 2019 utawala wa Donald Trump uliweka vikwazo vikali dhidi ya kampuni ya taifa ya mafuta, PDVSA, ukiwa na lengo la kuikatia serikali ya Maduro chanzo chake kikuu cha mapato.
Matokeo yake Marekani ilipoacha kununua mafuta ya Venezuela, China ikawa mnunuzi namba moja wa mafuta hayo. Kufikia 2025, China ilikuwa imekuwa destination kubwa mno ya mafuta ya Venezuela: takribani mapipa 642,000 kwa siku, au 75% ya exports zake kwa wastani, zilikwenda China.
Katika kipindi chote cha mvutano na serikali ya Venezuela, Marekani ilishirikiana na wapinzani wa serikali ya Venezuela, ili kuiangusha serikali hiyo kwa njia za kidemokrasia. Hata hivyo katika uchaguzi mkuu Mei 20, 2018, bado Maduro alimshinda Henri Falcón kwa kupata asilimia 67.8%.
Januari 23, 2019, Juan Guaidó, alijitangaza na akajiapishwa kuwa Rais wa Venezuela, kwa madai kwamba uchaguzi wa 2018 haukuwa huru na haki na Marekani ya Trump ikamtambua rasmi siku hiyo kama Rais wa Mpito wa Venezuela, jaribio ambalo lilishindwa kumuangusha Maduro.
Baadaye María Corina Machado akaibuka kama mmoja wa wapinzani wakubwa wa Maduro na alikuwa amejenga matarajio makubwa kwamba Marekani—hasa Donald Trump—angekuwa mshirika muhimu katika kuleta mabadiliko Venezuela.
Alimsifu Trump sana na hata akamkabidhi medali yake ya Nobel Peace Prize kama ishara ya kutambua mchango wake.
Marekani walipoona njia za kidemokrasia haziwapi matokeo wanayoyataka, wakaona isiwe tabu, Januari 3, 2026, wakatuma vikosi vyao nchini Venezuela na kumkamata Maduro.
Baada ya kuondolewa kwa Maduro, Delcy Rodríguez, aliyekuwa makamu wa rais wa Maduro, akawa Rais wa Venezuela na mara moja akatangaza yupo tayari kufanya kazi na Washington, na Washington nayo ikaitambua serikali ya mpito ya Delcy Rodríguez.
Rais Trump akaelekeza mfumo wa mafuta wa Venezuela kuelekea Marekani na makampuni yanayohusiana nayo. Makampuni ya kimarekani sasa yanaingia katika makubaliano makubwa ya mafuta na yameanza kusaini mikataba ya miradi mipya chini ya serikali hiyo.
Jambo la kushangaza Machado sasa amekuwa akihoji uwazi na masharti ya baadhi ya mikataba hiyo ya mafuta inayoendelea kusainiwa. Hapo ndipo vyama vya upinzani duniani kote vinapaswa kujifunza. Mataifa ya nje yapo kwaajili ya maslahi yao, sio demokrasia. Kesho yanaweza kufanya biashara na mpinzani wako kama mpinzani huyo atakuwa na arrangement bora zaidi kwake.
Hapa ndipo mfano wa Venezuela unapotupa lens nzuri ya kulitazama sakata la makinikia la mwaka 2017.
Rais John Pombe Magufuli alisema kwa msingi kwamba “Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini, lakini je, Watanzania wanapata sehemu inayostahili ya utajiri huo?”
Akaizuia export ya makinikia. Akaanzisha uchunguzi. Akaweka kampuni za madini chini ya pressure kubwa.
Hatimaye mgogoro huo uliingia katika negotiation mpya na Barrick na kuzaa mfumo mpya wa ushirikiano uliotoa Tanzania, miongoni mwa mambo mengine, 16% free-carried interest na settlement ya dola milioni 300.
Lakini Tundu Lissu alikuwa miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa namna Magufuli alivyoshughulikia suala hilo . Alionya kuhusu mikataba iliyokuwa tayari imesainiwa, sheria za kimataifa za uwekezaji, arbitration na uwezekano wa Tanzania kushitakiwa na kulipa fidia kubwa. Pia alipinga baadhi ya hesabu kubwa zilizotolewa kuhusu thamani ya madini yaliyokuwa kwenye makinikia.
Swali kubwa likabaki; Je, hofu ya mabeberu inapaswa kuwa veto juu ya maslahi ya Taifa? Hapo ndipo hoja ya Magufuli ilipopata nguvu.
Ikiwa kila mara nchi maskini itaambiwa:
“Msiguse mkataba huu, mtashitakiwa.”
“Msibadilishe sheria, wawekezaji watakimbia.”
“Msizuie export, international arbitration itawamaliza.”
basi swali linakuwa: Uhuru wa nchi hiyo uko wapi?
Kama nchi haiwezi hata kuhoji masharti ambayo rasilimali zake zinachimbwa kwa sababu inaogopa reaction ya corporations na foreign powers, sovereignty yake inaweza kubaki zaidi kwenye bendera kuliko kwenye uchumi.
Tundu Lissu amekuwa akiamini sana katika kushirikiana na mataifa ya nje kuing'oa CCM madarakani. Lakini wameshindwa kung'amua somo kubwa kutoka kwenye mapinduzi dhidi ya Maduro wa Venezuela
Wawekezaji wana maslahi yao. China ina maslahi yake. Marekani ina maslahi yake. Russia ina maslahi yake. Na hata taasisi za kimataifa zina mifumo na interests zinazoweza kutofautiana na za nchi yako.
Katika siasa za kimataifa, ukimkabidhi mwingine jukumu la kulinda maslahi yako, siku moja unaweza kushangaa kumuona amekaa mezani akifanya biashara na yule uliyedhani ni adui yenu wa pamoja.
Taifa lenye busara halijengi sera yake juu ya urafiki wa mataifa makubwa. Linajenga uwezo wa kujadiliana nayo.