Lissu ana somo la kujifunza kutoka kwa María Corina Machado wa Venezuela

 
Kwenye hili hata Lissu mwenyewe amewahi kukiri kwamba JPM alijitahidi. Shida ni kwamba alisubiri JPM afe ndio ampe maua yake

..Na Jpm alijaribu kumuua TL.

..sasa TL angekufa angemsifiaje Jpm?

..unaona jinsi Jpm alivyokuwa mjinga na hayawani?

NB:

..Jpm alisubiri mpaka awe rais ndipo atetee madini na rasilimali.

..TL ametetea rasimali tangu akiwa kijana mdogo bila ulinzi wa serikali au mtu yeyote.

..Na kipindi chote TL amepambana na makampuni toka nchi za mabeberu.
 
Lisu pia alipinga miswada ya sheria zinazosimamia ubinafsishaji wa rasilimali zisipelekwe bungeni kwa hati ya dharula. Kwani udharura huo unasababisha tupigwe.
Ndio, hati ya dharura kupitisha document ya page 100 za kisheria bila kusoma ni hatari kwa maslahi ya taifa. Maana haikutoa muda kwa wadau kutoa maoni, wabunge kuisoma na kupata ushauri wa kisheria kabla ya kuchangia.
 
Kwenye hili hata Lissu mwenyewe amewahi kukiri kwamba JPM alijitahidi. Shida ni kwamba alisubiri JPM afe ndio ampe maua yake
Lissu hakupinga JPM kupambania rasilimali alipinga MBINU, mfano alitaka mikataba iwekwe wazi bungeni, sheria zisipitishwe kwa dharura, mafisadi ya madini yakamatwe cha ajabu mpaka leo hakuna wezi wa madini walifikishwa kortini, hakuna mkataba uliwekwa wazi na in fact tumeshalipa zaidi ya Trilion 1 kwenye kesi za madai.

Kama JPM angesikiliza kuna ujinga ungeisha
 

Wewe ni mpumbavu kama wapumbavu
 
Maneno meeeengii. Unamaliza Miti tu
 
Kwenye hili hata Lissu mwenyewe amewahi kukiri kwamba JPM alijitahidi. Shida ni kwamba alisubiri JPM afe ndio ampe maua yake
Wakati Lisu anapambana na hiyo mikataba mibovu, Magufuli aliwahi kumpa maua yake, au yeye alikuwa anasubiri kupewa maua yake tu?

Kwenye mikataba ya madini kuna namna propaganda za ushindani wa kisiasa zilitumika kuhadaa umma. Lisu alikuwa wazi kuwa tuliingia mikataba ya kipuuzi, na walioingia ni viongozi wa ccm. Hakuna popote Lisu aliwahi kuingia hiyo mikataba. Lisu alisema kuna namna ya kudeal na hiyo mikataba ya kimataifa, na sio kwa kiki za kukamata makinikia. Kwa bahati mbaya Magufuli alipambana kwa nguvu kwenye hiyo mikataba, na sio kwa akili. Na Magufuli hakutaka cdm wapate sifa bali alitaka aoneka ni yeye tu na ccm ndio wamepambania hiyo mikataba. Matokeo yake tumelipishwa fidia kwa kuvunja mikataba ile mingi, hadi serekali imeamua kulipa kwa Siri kuficha aibu ile. na wanajua wakilipa kwa uwazi Lisu ataibuka shujaa.
 
Yaani katika watu watakaoleta mabadiliko nchi hii ni Lisu. Na ukitaka kujua Lisu ni zaidi, tazama kati ya Magufuli na Lisu nani yuko hai. Hakuna chochote wazungu wanachokitaka hapa nchini watakikosa kwa ccm hadi wamtegemee Lisu. Hizo propaganda za wazungu mtawaokota watu wa vijijini wasiojua lolote.
 
Kwenye hili hata Lissu mwenyewe amewahi kukiri kwamba JPM alijitahidi. Shida ni kwamba alisubiri JPM afe ndio ampe maua yake
Lissu ni mzee wa percent anaweza kumtetea hata muuaji ,mtu uwe na akili kama anavyodanganya misekule yake halafu hata alichogundua wala kuleta impact zaidi ni kijakazi wa Wazungu ...Huyo jamaa akipewa nchi lazima alipe fadhila ,familia yake inalelewa huko na yeye mwenyewe alienda kutolewa huko.


Kiufupi, hao wanasiasa ni wajanja sana ,mtaji wao ni ujinga wa watu...Mimi nina quotes za huyo jamaa kipind fulani alikuwa anamkosa sana Magufuli alipobana utoroshaji wa madini, Magufuli alitaka madini na makinikia yafanyiwe clearance kwenda nje na taasisi za serikali ili kupata thamani yake halisi katika kulipia kodi ,hilo jamaa likaanza kusema Magufuli hataki private wafanye kazi za clearance.

Uongozi wa sasa ,umetoa ile mandate imepelekwa kwa private kila siku madini yanatoroshwa ..Lissu alikuwa anadai hiyo taasisi iliyokuwa inashughulika na kuondosha hizo shehena za madini na nyara za serikali ni mali ya Magufuli wakati ilianza mwaka 2017 kisheria kabisa.
 

..hata wewe unamtetea muuaji Baba Jesca, na muuaji Mama Abduli.
 
..traitors ni ma-ccm unaowatetea.

..TL katetea rasilimali miaka yote, na wanaompinga, na waliojaribu kumuua, ni Ccm.
Nchi yetu tuachie kibaraka ,Mungu anatulinda nyie wafanya fujo muondoke ,vurugu tu kama mambwa.!
 
Na hapa ndio unakuta Iran inajadiliana na U.S kwa kutumia kalamu ya ballistic missiles,.....huku walokole wa Bongo wakiishia kusema Iran ni magaidi
 
Nchi yetu tuachie kibaraka ,Mungu anatulinda nyie wafanya fujo muondoke ,vurugu tu kama mambwa.!

..wanaoleta shida Tanzania ni mahayawani waliokuwa wakitumwa na Baba Jesca, na sasa Mama Abduli, kuteka, kutesa, na kupoteza, ndugu zetu.
 
Kwa yaliyotokea oct 29 ingekuwa maslahi ya Mabeberu yako hatarini mpka leo hii tusingekua hapa tulipo ukiona wamekaa kimya au wanaongelea mbali basi ujue mambo yao yanaenda …Hata uwe dikteta wa namna gani kama unawa-favour hawana shida na wewe , ingekua ni waumini wa demokrasia kama wanavyojinasibu M-7, Kagame wote wasingekuwepo hao ndio Mabeberu win-win approach ndio mtindo wao.
 
..wanaoleta shida Tanzania ni mahayawani waliokuwa wakitumwa na Baba Jesca, na sasa Mama Abduli, kuteka, kutesa, na kupoteza, ndugu zetu.
😅😅 Wafuate sasa! kuna level utaishia kubweka kama mbwa ,dogo jaribu kujua limit yako sio shobo dundo kibao.
 
Ukiwaeleza watu mambo haya wanakimbilia kutukana badala ya kujibu hoja. Mataifa ya nje hayana interest yoyote na demokrasia, huwa wanaitumia demokrasia kama silaha ya kufanikisha agenda zao za kupora rasilimali za nchi masikini.
 
Ukiwaeleza watu mambo haya wanakimbilia kutukana badalq ya kujibu hoja. Mataifa ya nje hayana interest yoyote na demokrasia, huwa wanaitumia demokrasia kama silaha ya kufanikisha agenda zao za kupora rasilimali za nchi masikini.

..kweli kabisa.

..na kwasababu Ccm ni madalali wazuri wa rasilimali za Tanzania wanamageuzi tusitegemee msaada wowote toka kwa mabeberu, au taifa lolote la nje.

..Mabeberu hawasaidii upinzani kwasababu wana hakika mema na vinono wanavyopata toka kwa Ccm, hawawezi kupata toka kwa wapinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…