Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Tundu Lissu afahamishwe katika kushika dola umoja ni muhimu zaidi kuliko hata sera, uhalisia na ukweli. Pamoja na yote anayofanya lazima ajue lugha ya ukali anayotumia kwa CCM na serikali haifai na haiwezi kudumisha umoja ndani ya chama chake, anapaswa kuipooza. CHADEMA hakijawahi kushika dola kama CCM hivyo hakiwezi kuwa na matatizo mengi na makubwa ya kimfumo na kimaslahi kama chama tawala CCM. Ukweli ni kwamba kuelekea 2025 hakuna chama kingine mbadala cha upinzani kui challenge CCM madarakani.