Lissu anahujumiwa, CHADEMA imeuzwa

Ogopa watu ambao Akili zao huwa zinashikiliwa na mtu mwingine !! 😅😅
 
Anzisheni chama chenu kama mnaona Lissu anahujimiwa .Mtakapokuwa mmeanzisha chama chenu Lissu mumpe uwenyekiti ili apate jukwaa huru la kuendelea kuporomosha MATUSI
 
weka clip angalau moja tuone hiyo tofauti! Nilisema mnapakazia kuwakosanisha , mmefeli right from the morning
 
 
Eti na Wewe ni binadamu..#
 
Mkuu kila mtu huwa ana hisia, ila ni vyema kuzidhibiti ili mtu aweze kupata heshima ama kutokukosea watu wengine. Mathalani mtu akiwa na njaa haimaanishi anapaswa kula chochote kile akionacho mbele ya macho yake, hali kadhalika huwa hivyo pia akiwa na kiu, hamu ya kufanya mapenzi, usingizi, n.k.

Hisia za kiunaharakati zina matamanio yake pia, bali hupaswa kuthibitiwa pia. Ratiba ya kiongozi yeyote yule wa CDM huratibiwa na makao makuu, kwa hiyo suala la matumizi ya muda, vitu na watu hutegemeana mahitaji ya rasilimali husika. Pamoja na hisia zako zote hizo na madai yako ya kuwa karibu na chama hiki, wewe unapaswa kujali ujumbe unaotolewa kwa umma kuhusu umuhimu wa uwepo katiba mpya.

Kutaka kuaminisha watu kuwa kuna mgogoro ambao unafukuta ndani ya CDM, ama upendeleo katika matumizi ya ruzuku, hizo sasa ndizo hisia zako wewe binafsi. CDM ilikuwa kifungoni kwa miaka 6 pasipo kupewa haki yake ya kikatiba na kisheria ili kijitangaze, kiuze sera zake, na hata kutafuta wanachama wapya.

Sasa CDM kinafanya hivyo nchi nzima, lakini mtu kama wewe unakuja na andiko lenye kubeba ujumbe wenye hisia hasi zenye kila dalili ya kutaka kudhoofisha jitihada hizi. Suala la kuwa hisia hasi kama hizi katika jitihada zinazofanyika hivi sasa, zinalifanya andiko lako kuweza kupambanuliwa kuwa upo upande wa mahasimu wa CDM.
 
Wewe unayejua pls tujuze walichozungumza
 
Hilo nimeliona hasa la mikutano ya lissu kutopewa kpaumbele na viongoz wa chadema ni ajabu kuona pages za viongoz zmejaa pcha na video za mikutano ya mbowe and hakuna za lissu. Hayo mengne ya lissu kujtegemea wewe n jitu liongo sn sn.
 
Kuna mambo umeandika, ndiyo ukweli na ndiyo uhalisia, LAKINI conclusion yako siyo SAHIHI.

Nadhani kuna kitu hukielewi. Kwenye mapambano ni lazima kuwepo wa kazi na mbinu, lakini lengo hubakia ni moja.

Haiwezekani Mbowe aongee kitu hicho hicho, Lisu kitu hicho hicho, Mnyika hicho hicho na Heche kitu hicho hicho.

Hata tu kwenye muziki, ili muziki uwe mzuri ni lazima wawepo wenye sauti za kupaa, sauti za kati na sauti za chini.

Kuna wakati Kikwete aliposhambuliwa kwa nini anawaweka wazee kwenye Serikali yake, aliwajibu kwa kusema, 'wapo watu wanasema niwaondoa wazee wote kwenye Serikali, haiwezekani. Ukikwaweka vijana pekee yao kila sehemu, nchi italipuka hii. Wazee ni grisi.

Lisu kuendesha mikutano katika hali ya ufukara, ndiyo uhalisia wenyewe. Chama ni kikubwa sana lakini resources ni kidogo sana. Sasa hivi kuna mikutano inayoendelea nchi nzima, mingi haitangazwi, na yote inagharamiwa na watu binafsi. Wiki iliyopita tu niliombwa mchango, nikawachangia, na nadhani ni hali ya nchi nzima.

Lisu mwaka 2020 aliendesha mikutano yake katika hali hiyo hiyo ya umaskini. Ilishindikana kupata hata mabango, lakini kutokana na picha tulizokuwa tunaziona, hakupungukiwa watu.

La muhimu sana ulilolisema, ni wananchi kuchangia gharama za mikutano hii maana katiba ndiyo mustakabali wa kila mwananchi, ni mstakabali wa Taifa zima, na siyo CHADEMA pekee.
 
Hizi zote ni hisia.

Btw, Mbowe na Lissu nao ni watu kama wewe wanahitaji furaha na maendeleo pia.
Hao watu wameteswa sana na hizi siasa...kama ni kweli wanakula acha wale.
Hii dunia tunaishi mara moja tu.
Ukimjua Freeman alikotoka ukiambiwa alikuwa anachoma nywele na kuuza NGADA utasema anasimgiziwa! Lakini huo ndio ukweli mtupu.
 
Ndio maana sie wengine tulishawapuuza hawa kina Mbowe tokea 2015.

Lakini kwa Lissu hiyo ni karma inafanya kazi. Dr. LISSU alipokataa mambo ya kisalitiana kwa vipande vya fedga wao walimuita mamluki na Lissu akamshambulia mno.

Wamemalizana na watu walioona wabaya wao leo wameanza wao kwa wao.

Ukiangalia maneno anayoongea Lisu na maneno ya Mbowe unaona kabisa hakuna connection kati yao. Kwa sasa ni kama wanaviziana.

Yawezekana Mbowe kaamua kuvamia mikutano ya Lissu ili kupangua kauli za Lissu ambazo kwa sasa watu wengi wanategemea kusikia kutoka upinzani.
 
Thibitisha ni uongo. Mimi nimeandika ukweli
Hapa ndio unaona umecheza mind game la hatari, inaonekana ww ni mzee, maana wazee wengi ndio wanaamini kwenye propaganda za kichovu hivi.

Tuchukulie uliyosema kwenye post namba moja ni kweli. Hata kama ni kweli, hilo kwetu ndio afya ya chama wetu kutofautiana, ukiona kwenye taasisi watu hawatofautiani, jua kuna walioacha kufikiri. CDM haiba ujinga huo wa kiccm.
 
Thibitisha ni uongo. Mimi nimeandika ukweli
Ukweli haupatikani kwa kusema kuwa, 'nimeandika ukweli'.

Wewe kushindwa kujenga nyumba nzuri ya kuishi familia yako, ukaamua kupanga, siyo uthibitisho kuwa umeuza familia. Yaani Lisu kutembelea gari la kukodi ndiyo uthibitisho kuwa ameuza chama? Yaani Mbowe kuelezea mazuri ya Samia kukuza demokrasia ndiyo kuuza chama? Kwani ni uwongo kuwa ni Rais Samia ndiye aliyekubali kurudishwa kwa haki ya kikatiba ya kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa? Kwani ni uwongo kuwa ni Rais Samia ndiye aliyetoa maelekezo kwa DPP kuwa afute kesi ya uwongo dhidi ya Mbowe iliyokuwa imetengenezwa na akina Siro, Diwani, Muganga na kundi lao lile la kishetani la kuwabambikia watu kesi? Utambue kuwa ni Siro na Diwani waliomdanganya Samia kuwa kulikuwa na kesi na ushahidi mzito dhidi ya Mbowe, Rais akaamini, kumve ulikuwa upuuzi mtupu. Na ndiyo sababu akaamua kuondokana nao.
 
Mfanyabiashara ni mfanyabiashara tu haijalishi yuko wapi na anafanya nini.

All in all ni kijana wa Saigon.
 
Uongo utakusaidia nini?

Wanyukane hivyo kisha Lisu atumie hela yake kujilipia gari la kukodi na mbowe atumie helkopta kisa CHADEMA? Sababu ya ku-fake ni nini hasa?

Yaani hamuelewani ila mlengo wenu ni mmoja?

Itoshe kusema we mpumbavu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…