Lissu anahujumiwa, CHADEMA imeuzwa

Dah!
Huu ni "Mkakati" uliosukwa kwenye maridhiano?
Mbowe anapata 'booster' ya Samia kuwadhibiti akina Lissu ndani ya CHADEMA?

Hadi hapa nilipofikia kwenye andiko lako, dhana hii sina njia ya kuipinga; pamoja na kwamba ndani ya andiko lenyewe naona kuna udhaifu wa aina fulani kwa upande unaoutetea..

Ngoja niendelee kukusoma.
 
Mkuu 'TETRACYCLINE', haya uliyoandika huku chini hayahusiani kabisa na mada yenyewe. Wewe ni 'Team' Nani, Mbowe?

Hayo ya uraia na mengine ya binafsi' tuyajadili kwingine. Hapa tuijadili hii dhana aliyoleta huyu 'Mwingereza'.
 
Nimemaliza kukusoma mkuu 'Mwingereza'.

Sasa naomba tu jibu, toka kwako, au kwa yeyote mwanachama wa CHADEMA aliye na jibu:

Je, CHADEMA kama chama, kinasemaje kuhusu hali hii iliyopo? Msimamo wa chama ni upi? Ule wa Mbowe, au ule wa Makamu wa Mwenyekiti, Lissu?

Chama hakiwezi kuwa katikati ya hawa wawili, ni lazima kiwe upande kinakosimamia kama chama.

Mkanganyiko huu hauwezi kuachwa uendelee kuwepo ndani ya chama.

Nihitimishe: Ulichosema kuhusu Mwenyekiti Mbowe, hilo sina mashaka nalo toka zamani sana; kinachonistua ni hili ulilozungumzia hapa kuhusu Lissu, na katika hali ya kushangaza sana kutambua kwamba hali kama hiyo inaweza kuwepo ndani ya chama hiki bila ya kutafutiwa jibu haraka.
Mbinu ya Mbowe na Samia kuwalaza akili wanaCHADEMA hadi dakika za majeruhi, hili ninaliona.

Mbowe ni mtu mwenye njia zake za kufanya mambo. Sasa naamini hata wale COVID -19 ni matokeo ya kazi ya mikono yake, kama ilivyokuwa kwa Lowassa.
 
Tundu lisu anatafuta nafasi yeyote ile ya kumuweka mbowe pembeni lakini akashindwa. inakuwaje anaongea kuwa jamaa alilamba asali? afu mbona kama hawapo pamoja? yaani mbowe anatuhumiwa kuhongwa asali.
 

..Wakoloni, kwa mfano, Waingereza, hawakuwa wakatili kama hawa watawala wetu wa Ccm.

..Nakupa challenge. Umewahi kusoma mahali popote kama mkutano wa Tanu wa kupinga ukoloni umeshambuliwa kwa mabomu, risasi, au washawasha?

..Umewahi kusoma au kusikia Mwalimu Nyerere au kiongozi wa Tanu kukamatwa, kupigwa, au kudhalilishwa, na vyombo vya dola vya Wakoloni wa Kiingereza?

..Mimi sikubaliani na mfano ulioutoa unaoonyesha kwamba Ccm wana afadhali ktk kukabiliana nao kuliko wakoloni, haswa Waingereza.

..Mimi nasimama ktk hoja yangu kwamba Mbowe kumsifia Samia kwa kufungua milango ya kufanya siasa hakuondoi ukweli kwamba Ccm ni mbovu na imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi.
 
Ombi langu kwenu wadau: Msaidieni Lissu kifedha, hali na mali ili aweze kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ufisadi unaoendelea, umuhimu wa katiba Mpya, Pamoja na Tume huru ya uchaguzi kwa wananchi.
Watu wakitaka kuchanga wapeleke wapi?

Ni vizuri umetoa mwanga wa mwanzo kuhusu hali iliyovyo huko ndani ya CHADEMA.

Ni muhimu sana sasa chama kitoke mbele na msimamo wake ujulikane kinaelekea wapi.
 
Samia hamfanyii mtu yeyote fadhira, hadi watu walazimike kutoa shukrani, ni wajibu wake kuheshimu sheria zilizopo.

Mbowe anakuwa mbinafsi na kusahau dhamira ya CHAMA alichokiongoza.
 
Tunasimama na Lissu, alipo tupo
 
Samia hamfanyii mtu yeyote fadhira, hadi watu walazimike kutoa shukrani, ni wajibu wake kuheshimu sheria zilizopo.

Mbowe anakuwa mbinafsi na kusahau dhamira ya CHAMA alichokiongoza.

..Chadema ktk mikutano mbalimbali wameeleza kwamba kuzuia mikutano ya hadhara ilikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na katiba.

..Wako viongozi ambao wamekwenda mbali na kusema Samia alipaswa kuomba RADHI wakati akitengua zuia haramu la mikutano ya vyama.

..Magufuli alipokufa alikua ameacha viongozi na wanachama wa Chadema zaidi ya 400 ktk mahabusu na magereza mbalimbali hapa nchini.

..Mazungumzo kati ya Chadema na Ccm yamewezesha kuachiliwa huru kwa mahabusu na wafungwa wa Magufuli.

..Hakuna namna Mbowe au kiongozi yeyote wa Chadema anaweza kuongelea suala hilo bila kuonekana anamsifia au anamshukuru Rais Samia.

..Mbowe kumsifia au kumshukuru Samia hakuondoi au kupunguza matatizo na kero za wananchi. Zaidi, haimaanishi kwamba Mbowe anakubaliana na sera na maamuzi yote yanayofanywa na Samia au Ccm.

..Majuzi nimesoma Mbowe akinukuliwa kusema kwamba itakuwa ni makosa makubwa kuingia ktk uchaguzi mkuu wa 2025 bila Katiba mpya na Tume huru.

..Msimamo huo ulipotamkwa na Lissu kuna baadhi waliandika post ktk jukwaa letu kwamba kuna kutofautiana baina ya viongozi wakuu wa Chadema.

..Kwa kifupi nadhani kuna jitihada kubwa hapa Jamii Forum kupotosha ukweli kuhusu Chadema, na kufifisha credibility ya viongozi wake.

..Ccm wameishiwa hoja, pia wameishiwa mbinu za kutatua matatizo ya nchi yetu. Kukabiliana na hali hiyo wameamua kuwekeza ktk kuchafua vyama mbadala na viongozi wake.
 
..Mbowe kumsifia au kumshukuru Samia hakuondoi au kupunguza matatizo na kero za wananchi. Zaidi, haimaanishi kwamba Mbowe anakubaliana na sera na maamuzi yote yanayofanywa na Samia au Ccm.
Hili ndilo jibu.

Sidhani kuwa kuna mtu yeyote mwenye akili timamu ataacha kushukuru, hata kama Samia alipaswa kufanya alivyofanya.

Lakini Mbowe anaonyesha waziwazi kwamba ni zaidi ya shukrani za aina hiyo.
Mbowe amekwisha, na asiimalize CHADEMA kwa kwisha kwake.

Urafiki wa Samia na Mbowe usiingilie shughuli za CHADEMA.
 

..Zaidi ya kumshukuru Samia, au kueleza jinsi alivyofutiwa kesi ya ugaidi, Mbowe amefanya jambo gani in favor of Ccm na Samia, and against Chadema?
 
Hizi zote ni hisia.

Btw, Mbowe na Lissu nao ni watu kama wewe wanahitaji furaha na maendeleo pia.
Hao watu wameteswa sana na hizi siasa...kama ni kweli wanakula acha wale.
Hii dunia tunaishi mara moja tu.
Mbowe akila Sawa ni binadamu watu wengine wakila ni mafisadi ukabila umewajaa mno
 
Naam hakika umeelezea Kwa kadiri unavyowajuwa ...we penyeza rupia
 

Itapendeza kama ungeweza kuthibitisha kuwa wewe siyo Kamanda Aliyechoka

Unaonekana kuwa na hasira kali dhidi ya Mbowe.

Ulichoandika siyo ukosoaji. Wewe unaonekana kuwa ni mtu wa chuk binafsi. Chuki hazijengi ndugu.

Wewe na kina Joni, msajili, CCM, Ayubu au jiwe na nduguze baba mmoja mama mmoja!
 
Baada ya CD ya CHADEMA ni chama cha Wachaga sasa mmehamia kwa Lissu Vs Mbowe. Nyie ni Wapumbavu
Hawajafanikiwa kuisambaratisha kama walivyofanikiwa kwa NCCR mageuzi na CUF, na sababu ni uimara wa Mbowe sasa wanatatarika.
Naunga mkono hoja ni wapumbavu
 
Nasimamia maneno yangu. Kwamba, maridhiano ni ya Mbowe, Samia na CCM

Viongozi wote wa Chadema nilioongea nao, hawataki kabisa maridhiano wakiamini ni ujanja wa wa CCM kupoteza muda
Umeongea na nani? Kama nani?
Rest be assured kuwa Tanzania haitorudi nyuma kwenye siasa za ukatili na kuuana, visasi na dhulma mlizozoea nyie wapumbavu wa CCM
 


Hii sehemu tu ndo imeharibu andiko lako :

"Kama alivyofanya miaka yote, 2015 aliuza chama kwa Lowassa. 2025 Mimi na wewe hatujui yeye na Samia wamepanga nini"

Kama ni miaka yote, ina maana asingeshtakiwa kwa ugaidi....

Peleka utapeli wako wa ccm..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…