Lissu anahujumiwa, CHADEMA imeuzwa

Upumbavu at its best, kwamba kwa Mbowe kukubali maridhiano amelambishwa asali unaorhibitisha, kwamba kwa Lissu aliyeshambuliwa akiwa kwenye majukumu ya kitaifa, aliyekataliwa kutibiwa na serikali ingawa ni haki yake, akaishi uhamishoni kama mkimbizi, akapewa uraia na familia yake baada kunyimwa haki zake za kuishi na kutibiwa na stahiki zake.

Kuwa hana uchungu na nchi hii kwa kupata haki ya kuishi kwa amani uhamishoni, yeye ambae hata kurudi kwake aliomba kuhakikishiwa usalama wake. Ila waliotaka kuutoa uhai wake, wakamnyima stahiki zake ndio wenye uchungu na nchi hii na yeye kurudi na kutumia haki yake kufanya siasa amelambishwa asali, uko vizuri upstairs kweli?

Kwamba Mbowe aliyefilisiwa na shetani Magufuli, na Lissu aliyetaka kuuliwa na shetani Magufuli wametajirishwa kitambo?

Hii yote ili wasiaminiwe? CCM mmefika kiwango cha juu cha unafiki or rather kiwango cha juu cha upumbavu
 
Siasa ina mbinu nyingi, umewahi kuona wawindaji wanavyomkimbiza mnyama, kila mmoja huenda upande wake
 
Kama mtakuja na cheap propaganda zenye dhamira ovu, mkatengeneza uzushi wa zaidi ya upumbavu bila uthibitisho dhidi ya watu waliokuwa wahanga wakubwa wa siasa mbovu za ukatili na kuuana kwa kiwango cha kutisha mkategemea watu watajiingiza kwenye kusifia huo upuuzi mtakuwa mmepotea.

Hoja yenye dhamira nzuri iliyojengwa kwa hoja jadidi zenye uthibitisho zitajibiwa kwa weledi so uzushi na majungu, hayo yatajibiwa accordingly. Kwanifoolish questions deserves foolish answers so is foolish comments
 
Uko very biased, mahaba yako both ways. Yako kwa wale wasiopenda kuona chama cha upinzani kimesimama imara ambako huzungumzii sadly ndio upande ulioko

Tunakumbuka hila zilizosambaratisha NCCR mageuzi ilipokuwa na nguvu. Tunakumbuka hila zilizosambaratisha CUF ilipokuwa na nguvu, na sasa tumeona viongozi wa CHADEMA wakinunuliwa kwenda kuunga mkono juhudi.

Tumeona walioshambuliwa na kuuawa na majaribio ya kuuliwa, waliobambikiwa kesi na kufungwa magerezani kwa kesi za kutengeneza ambao wengi wameachiliwa baada ya Mbowe kukubali kukaa na kuzungumza na nchi inaenda mbele sasa.

You are the one who is soft minded kutulazimisha tuzipokee cheap propaganda kama hizi, hebu tupe proof ya Lissu kutumia pesa zake za mfukoni kwenye mikutano ya chama? Ukishindwa na wewe ni mmoja wao
 
..Zaidi ya kumshukuru Samia, au kueleza jinsi alivyofutiwa kesi ya ugaidi, Mbowe amefanya jambo gani in favor of Ccm na Samia, and against Chadema?
Hili ni swali makini nisilopenda kulijibu kwa pupa. Nipe muda nilitafakari kwa kina ili nipate jibu linalolingana na uzito wa swali.

Siyo lazima, "Mbowe afanye jambo 'against' CHADEMA" ndipo ionekane kuwa anafifisha juhudi za chama kufikia malengo yaliyotegemewa, ya kuiondoa CCM madarakani.

Mbowe anaweza kuridhika kwa kuahidiwa nafasi yeye na chama chake ndani ya serikali, ambayo bado itakuwa chini ya CCM; yale yale ya Kenya tuliyokuwa tunayazungumzia humu JF hivi karibuni.
 

..adui wa mabadiliko sio Mbowe.

..adui wa mabadiliko ni hawa wanaleta propaganda dhidi ya Chadema.

..kuna juhudi kubwa zinafanyika ili tusifuatilie na kusikia ELIMU inayotolewa na Chadema ktk mikutano yao na wananchi.

..kila Chadema wakianza mikutano kunaibuka post nyingi zenye lengo la kufifisha hoja wanazozipeleka kwa wananchi.

..jana tulijadili helikopta ya Mbowe. Leo tunajadili jukwaa la Lissu. Ccm hawataki tujadili Katiba au Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Mkuu 'Joka', sina tofauti yoyote kuhusu hilo kundi linalofanya hizo juhudi humu JF na kwingineko. Binafsi kelele hizo hazini'influence' mtizamo wangu katika maswala haya ya siasa za nchini mwetu humu.

Mimi ninawasoma wahusika wenyewe, akina Mbowe, Lissu , Samia na wengineo na kufikia utambuzi ninaouona kutokana na wao, siyo haya makundi ya wapiga kelele pembeni.
 

..lakini hapa hatujadili hoja za Mbowe, Lissu, Ruge, etc wanazozitoa ktk mikutano yao.

..tunajadili mambo madogo madogo ya kutupotezea muda tusijadili KATIBA MPYA.

..mimi nataka nisikie CCM wanataka nini ktk katiba mpya, ili tuchanganye na hoja za wengine na kufikia muafaka wa Kitaifa.
 
..jana tulijadili helikopta ya Mbowe. Leo tunajadili jukwaa la Lissu. Ccm hawataki tujadili Katiba au Tume Huru ya Uchaguzi.
Hizi zinaweza kuwa ni ishara muhimu, ambazo hata kama ni njia za kpotezea lengo, lakini kama zipo haziwezi kupuuzwa.
 
Hii naifanya sehemu ya jibu langu kuhusu swali lako ambalo bado ninalitafakari kama nilivyoeleza hapo juu.

Kama Mbowe, Lissu, Ruge wanazo ajenda ambazo zinatakiwa wananchi ziwafikie na wazielewe ipasavyo, hivi ni jukumu la nani kuhakikisha agenda hizo zinawafikia wananchi?

Mbowe anaposhindwa kwa sababu anazozijua mwenyewe kufikisha hizo ajenda kwa wananchi kwa , pengine kuogopa asionekane kutokuwa na shukrani kwa fadhila alizofanyiwa, watu wamlaumu nani?

Mbona huko nyuma ajenda za namna hiyo zilikuwa hazina shida kufika zinakotakiwa kufika?

Kwa hiyo, inawezekana kuna kitu kilichomtokea Mbowe, asiweze kufikisha ajenda zake 'more effectively' huko anakotaka kuzifikisha. Ni wajibu wake sasa kuangalia kama mtindo wake huu mpya ndio sahihi au la.

Tafadhali, naomba usinielewe kwamba nataka awasilishe mambo yake na chama chake kwa kutukana, au lugha chafu. Hapana.
 
mimi nataka nisikie CCM wanataka nini ktk katiba mpya, ili tuchanganye na hoja za wengine na kufikia muafaka wa Kitaifa.
Dah!
'Joka' Bhwanah!

Kuna nyakati huwa tunachimbuana akili ili tufikie kwenye hitimisho moja ambalo wewe na mimi mara nyingi tupo pamoja.

Lilwe swali lako lililonitoa jasho leo, kila tunapojadili naona tunapata jibu sahihi juu ya swali hilo.
Kuhusu ni kitu gani anachofanya Mbowe, ambacho kinaonekana anaisaidia CCM, au anaikandamiza CHADEMA (sikunakili 'verbatum).

Hebu usome tena huo mstari niliounyanyua hapo juu kutoka kwenye bandiko lako.

Binafsi sikuwahi hata siku moja kumsikia Mbowe katika mikutano yake kabla ya "maridhiano" akitumia lugha ya kuudhi kwa yeyote, iwe kwa CCM au viongozi wake, hata wakati ule wa Magufuli, alipokuwa akisulubiwa, sikuwahi hata siku moja kusikia Mbowe akitumia lugha chafu popote; lakini alieleweka vizuri kabisa, hata alipokuwa akidai Katiba Mpya.

Sasa huyu Mbowe, baada ya "maridhiano" mbona ni kama Mbowe mwingine?

Na hawa wapiga kelele wa pembeni waliojazana humu kupoteza lengo; Mbowe hawaoni? Je, hizi zikiwa ni mbinu zinazotumiwa na hao hao alioingia nao "maridhiano" haoni kwamba zinafifisha juhudi zake kama hawezi kupitisha ujumbe wake ukasikika?
Kwa mfano: Lile swala alilolizungumzia Lissu, kuhusu mabango yaliyoenezwa kila kona za miji yetu kuhusu maridhiano, hizi nazo tuziite kelele za watu wa pembeni, au ni mbinu mahsusi zilizolenga matokeo maalum? Kuyasemea haya nayo inampa taabu sana Mbowe asionekane kuwa anakiuka makubaliano ya maridhiano?

Mbowe kabadilika sana, siyo rahisi tena kuficha mabadiliko hayo wanayoyaona wananchi.
 
Mkuu kabla sijasoma hili porojo reefu nilishaandika humu kuwa Chadema wamepoteana lakini chama chao kinaelekea kufa kabisa kabisa, Tanzania hakuna upinzani wenye nguv tangia enzi za Maalim Seif, mbowe tokea alivyotoka jela break ya kwanza akatua Ikulu tayari kwa wenye kujua walielewa thamani ya mbowe sasa itakuwa wapi

Na hata huyo Tundu Lissu alimpokea mama samia Belgium bila ya hata ushauri na wenzake na walichoongea wanakijua wao, kwa vile hadi leo Lissu hakuuambia umma juu ya walichoongea.

Tundu Lissu hawezi tena kuwa mwanasiasa kama alivyokuwa kabla sasa toka apate yale matatizo na kuangukia belgium huko ndio kwenye maisha yake na hawezi kukaa tena Tz hata kwa dakika 5 anataka kurudi, anarud Tz kuzugazuga tu lakini hana tena morali ya kisiasa na kuwasaidia watanzania ambao wanahitaji mabadiliko

Chadema ilipasuka vipande vipande kwa tamaa za hela tokea kina kafulila sijuwi na nasari, waitara, silinde na genge looote hadi kumfikia kina halima mdee na sasa mbowe naye ameingia mahali hapo hapo ambapo haikuwa matarajio ya wote kwa kiongozi aliyekuwa anaonekana kuwa na msimamo kama mbowe. Huko Tanzania Bara hela ndio inayoongea siasa imeuliwa kabisa.

Tundu Lissu ata alipokosa urais hakupita hata jimbo moja la uchaguzi kutoa shukurani au kusema moja mbili tatu alikimbilia ubalozi akatimkia zake belgium hata hakuweka online conference meeting kusema chochote ni vile shida yake ilikuwa ni urais tu na yalipotokea yale yaliyotokea akawaacha Watanzania sasa amehamia video za mtandaoni na clips za youtube zitamsaidia nini mtanzania aliye kijijini ata network hana
 
Thibitisha ni uongo. Mimi nimeandika ukweli
Ukweli wa lissu anahujumiwa uko wapi?.Hivi lissu unavyomuona ni aina ya binadamu wakuhujumiwa kiasi ambacho hadi wewe ujue alafu akae kimya,huyo lissu unayemuongelea sio huyu tunayemfahamu.Siku mambo yakiparaganyika Chadema wao wenyewe ndio watakaotoa taarifa sio mtu mwingine wakuja na stori za kuunga unga.
 
Kama chadema imekufa kwa huu uji ga ulioandika hapa basi wewe ndo umeoza kabisa.
 
Kama chadema imekufa kwa huu uji ga ulioandika hapa basi wewe ndo umeoza kabisa.
poleni sana, chadema wakinyooshewa mkono tu ni kama wanawake malaya kwa hela hawaangalii nyuma yao kuna nani viongozi wao wote wamepuruchuka kwenda upande ule
 
Lissu yupo pamoja na Mnyika, Catherine Ruge, na Kaimu M'kiti wa Bawacha yule mama. Kwahiyo wote hao wanatumia hela zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…