Uchaguzi 2020 Lissu aonya juu ya mkakati wa nia ovu ya kumuengua baada ya watawala kupagawa kwa kimbunga chake mikoani, asema hilo halitofanikiwa

Yaani Lissu anacheza na maneno tu. Anayageuza geuza as if anaongea na wapumbavu. Sheria gani imesema mtu akikiuka sheria ya maadili mpaka afungwe. Atuambie kilichomfukuzisha ubunge ni nini? Rufaa yake aliyokata mahakamani alishinda? Kama hakushinda ina maana maamuzi yanabaki kama yalivyo. Wanachotaka hawa Chadema ni vurugu tu hiyo ndo ajenda yao. Lakini wanajua fika mgombea wao hana sifa za kuchaguliwa kuwa Rais.
 
Mipango yenye akili ni kushawishi umma ukupe kura kwa ridhaa yake siyo kwa kufanya uhuni wa kuzuia washindani wako asiingie uwanjani kushindana!
Kila kitu kina sheria na utaratibu wake. Kwanini mtu uvunje utaratibu kwa makusudi anatafuta nn? Mbona wengine wanaomba wadhamini kimya kimya hawafanyi mikutano ya hadhara. Sema tu Serikali imeshashtukia mpango wa Lissu aliokuja nao, ndo maana imeamua tu kumkalia kimya.
 
Sio busara kumuengua Tundu Antipas Lissu, aachwe tu kwani hajafikia viwango vya kumshinda Jpm
 
This time wamekula ya chuya
 
Ha ha jamaa ana akili sana..kweli unaanzaje kampeni wakati hujateuliwa?
Sheria ilimaanisha baada ya kuteuliwa na chama chako usianze kampeni kabla Tume haijakupitisha.Lissu anacheza na akili zenu ambazo siku zote hazitaki kufikiri.
 
Magufuli anazidi kujiaibisha.

Aache atashinda tu Jpm atashinda anaogopa nini??
 
Ukitafuta wadhamini unatakiwa kuhutubia Mkutano wa hadhara na kutoa ahadi
Ndio maana anahutubia kwenye ofsi za chama tu. Na analifahamu hilo. Sasa kupata wadhamini miambili wenye kadi kila mkoa unadhani hao unakutana nao wapi?? Kuna wenye kadi na wasio na kadi wote watakufata.

Nyie si mmefanya mambo mazuri kwa watanzania?? Sasa woga wa nini?
 
CCM watakaa kumjadili Lissu badala ya kujadili watia nia wao watakuja kushtuka muda wa kuchukuwa fomu NEC ushapita!
Yaani mwaka huu kuna kuna Bundi huko CCM. Wagombea wao hadi sasa hawajui hatima yao. Na muda unazidi kuyoyoma. Hii hali ilikuwa ikiwakuta wapinzani miaka ya nyuma. This time kibao kimebadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…