Lissu asema hajalipwa stahiki zake kama Spika Ndugai anavyoliambia Bunge

Lissu asema hajalipwa stahiki zake kama Spika Ndugai anavyoliambia Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Ndugai-na-Lissu-620x308.jpg

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amedai kuwa bado hajalipwa ‘gratuity’ (bahkshishi) yake ambayo ni asilimia 40 ya mshahara wake, tofauti na kile kinachoelezwa bungeni.

Lissu amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kulieleza kuwa Lissu ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, hadai chochote na kwamba ameshalipwa madai yake yote.

Vile vile, alidokeza kuwa mwanasiasa huyo anadaiwa Sh. milioni 70 ya mikopo aliyokopa benki. Akizungumza na Nipashe akiwa nchini Ubeligiji, alihoji: “Niliuliza swali dogo tu, je, nimelipwa kiinua mgongo changu ambacho ni sawa na asilimia 40 ya mishahara yangu?”

“Hayo ya mikopo yangu ya benki yana uhusiano gani na madai yangu ya ‘gratuity’, hakuna uhusiano hapo,” alisema.

Juzi Spika wa bunge, Ndugai, alieleza kuhusu fedha ambazo Bunge limemlipa Lissu ikiwamo posho mbalimbali na mishahara zaidi ya Sh. milioni 500 na kusema kuwa kwa sasa hana madai yoyote anayodai Bunge isipokuwa yeye (Lissu) ndiye anayedaiwa mikopo aliyodai kupitia bunge hilo inayofikia Sh. milioni 70 ambayo bado hajalipa.

“Lissu anapenda sana kuzungumza mambo yake mbele ya jamii, mimi nadhani si busara tena anachokizungumza hakina ukweli ni vyema angepiga hesabu vizuri,“ alisema Spika Ndugai.

Tangu kuvuliwa ubunge kwa kiongozi huyo wa Chadema, pamekuwa na mvutano kati yake na Bunge kuhusiana na madai mbalimbali ambayo aliyaibua Lissu ikiwamo mishahara, posho na fedha za matibabu wakati mwanasiasa huyo akidai kuwa ni haki yake kulipwa madai hayo Spika wa Bunge, amekuwa akisisitiza kuwa hakuna anachokidai katika bunge hilo.

Lissu alipigwa risasi 32 kati yake tano zilimpata mwilini Septemba 7, 2017, alipelekwa jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu na baadaye nchini Ubeligiji ambako amekuwapo hadi sasa.
 
Ninachojua Lissu anadai pesa yake sio kwa sababu ana njaa ila ni kwa sababu anapenda wakati wote haki itendeke.
Hiyo ni njaa Boss! Tusidanganyane hapa! Sijawahi sikia akizungumzia aliyowafanyia wapiga kura wake kama ilivyo ktk ajira yake. Badala yake kila siku ni kudai pesa! Haki yake sawa na je, haki ya wananchi ametimiza nini?
 
Ninachojua Lissu anadai pesa yake sio kwa sababu ana njaa ila ni kwa sababu anapenda wakati wote haki itendeke.

Tatizo lenu mmeshikiwa akiri na T Lisu, huyo lisu mwanzo alisema kalipwa pesa mpaka mwezi wa tano, lakini Spika akasema amemlipa mpaka mwezi wa sita, sasa ulitakiwa kujua kweli kalipwa mpaka mwezi wa sita?, cha pili huyo Lisu atalipwaje stahiki za ustaafu wakati wabunge wote wanalipwa mwezi wa sita? Ana u special gani mpaka alipwe kabla ya mwisho wa vipindi? Aache uongo, spika kasema kila mtu atalipwa mwezi wa sita kwa hiyo huyo lisu anatakiwa asubili mwezi wa sita asipolipwa nado azungumze, sasa kila anachosema mnapanua midomo bila kujiuliza kama kasema ukweli, kweli kazi mnayo.
 
..amefukuzwa Ubunge hivyo Spika alitakiwa kumlipa mafao yake bila kuchelewa, na kama anadaiwa akwate ktk mafao.

..kumfukuza bila kumlipa mafao ni muendelezo wa MATESO ya Spika dhidi ya Tundu Lissu.
 
Hivi huyu lissu ana uchungu kweli kuhusu shida za wananchi wa jimboni kwake na ajisikii aibu kuchukua pesa ambazo hajazifanyia kazi?
 
Back
Top Bottom