Lissu asema hajalipwa stahiki zake kama Spika Ndugai anavyoliambia Bunge

Hiyo ni njaa Boss! Tusidanganyane hapa! Sijawahi sikia akizungumzia aliyowafanyia wapiga kura wake kama ilivyo ktk ajira yake. Badala yake kila siku ni kudai pesa! Haki yake sawa na je, haki ya wananchi ametimiza nini?
Kwa hoja hizi za kijinga mkaqmua kumshona risasi zote zile??

Basi hela anazodai si zenu, ni za wananchi, kwanini mnamnyima haki yake????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamanda mchanigieni huyu mnyoa kiduku.
Nilifika Brussels nikaona unyoaji huo ni common kwa vijana wa kongo wanaoishi kati ya jiji, wakicheza muziki. Tatizo nilipoona mbunge wa jimbo Tz, siku chache baada ya kwenda Ubelgiji, naye ananyoa kama wao! Nikajua ni aina ya watu tunaowaona hawana substance. Wakiishi na mvuta bangi, siku chache wanavuta. Wakiishi na mcheza disco, nao hawalali. Wakiishi na mpiga pombe, nao wanaingia.
 
Kwa hoja hizi za kijinga mkaqmua kumshona risasi zote zile??

Basi hela anazodai si zenu, ni za wananchi, kwanini mnamnyima haki yake????

Sent using Jamii Forums mobile app
Risasi, risasi, kila siku risasi! Kuna watu wameuwawa na tulishasahu, itakuwa risasi 32? Kwa kuwa alipigwa risasi nyingi ndo adeke kila siku? Kila leo ni hadithi zake ili asisahaulike. Mwambieni shujaa arudi, woga umetoka wapi?
Kuna watu munasubili Lisu arudi utadhani Yesu. Lisu ni nani hadi awadanganye kurudi kwake.
 
Hivi ukivuliwa ubunge bado unalipwa kinua mgongo? Hapa sielewi naomba msaada wanaJF?
 
Umeelewa hoja inayoongelewa hapa.
 
Heeee, kuna Bakhshishi kumbe yaani acha Mshahara ya mamillioni, Posho laki 3 kila.kikao bado Mbunge anakula Bakhshishi ya asilimia 40?

Halafu kama akimaliza muda wake mpaka mwisho kuna malipo ya Kustaafu mpaka kufa!!! Jamani, jamani mimi naanzisha MUSWADA wa Wananchi dhidi ya vyama vyoote vya Siasa nchini. Hawa ndio wananalifilisi Taifa..
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amedai kuwa bado hajalipwa ‘gratuity’ (bahkshishi) yake ambayo ni asilimia 40 ya mshahara wake, tofauti na kile kinachoelezwa bungeni.
ALIPWE ASILIPWE HIYO mada huu sio wakati wake tafadhalini. HAPA TUNA WASWASI NA PANDEMIC YA COVID NYIE MNALETA HABARI ZA MTU BINAFSI!!!!

ACHENI KWANZA JAMAA SISI TUNA MAWAZO VICHWANI KUHUSU ITAKUWAJE GONJWA LINATUNYEMELEA, SASA MKILETA MAMBO YA MTU HAJALIPWA MNALETA MADA YA KINYUME NA MUELEKEO WA WABONGO KWA SASA.
 
Tatizo lenu mmeshikiwa akiri na T Lisu, huyo lisu mwanzo alisema kalipwa pesa mpaka mwezi wa tano, lakini Spika akasema amemlipa mpaka mwezi wa sit
Hapa kinachoongelewa sio Mshahara bali ni bahashishi na marupurupu
 
Hiyo ni njaa Boss! Tusidanganyane hapa! Sijawahi sikia akizungumzia aliyowafanyia wapiga kura wake kama ilivyo ktk ajira yake. Badala yake kila siku ni kudai pesa! Haki yake sawa na je, haki ya wananchi ametimiza nini?

Kuna popote Lisu amekusanya hela ya mpiga kura wake ili kumletea maendeleo? Kazi ya mbunge ni kuwa muwakilishi wa wananchi bungeni, kuisimamia serikali na kuishauri, pamoja na kutunga sheria. Ukitaka mbunge awaletee wananchi maendeleo, hela zisainiwe na mbunge.
 

Asubiri mpaka mwezi wa sita kwani yeye ni mbunge tena?
 

Hili sio jukwaa la afya, hili ni jukwaa la siasa, hoja zilizopo humu ni za kisiasa. Hizo za ugonjwa zina majukwaa yake.
 
Ukisoma vizuri bila mukali wa kumshabikia Lissu, utaelewa ulivyokwenda chaka. Message yangu hakuna inaposema Lissu apeleke pesa kwa wananchi wa jimbo lake. Nimeandika haki ya wananchi wake alitimiza? Naona unakuja na wazo la pesa tuuu!

Huyu ni mtu hovyo tu! Kila alipokwenda ni keleleee! Leo hii TLS ipo na rais mwenye elimu kubwa kuliko yake lakini hatusikii kelele za kizembe kama za kwake na yule bibi wa Zbar. Mtu anayetafuta uadui kila wakati hafanikiwi. Anaishia kutumika na kuitwa shujaa wakati wenzake wanafaidi.
btw., hajasindikizwa kurudi nchini?
 
Asubiri mpaka mwezi wa sita kwani yeye ni mbunge tena?

Wote walio hama vyama na kukosa nafasi wanasubili final mwezi wa sita ndio mwisho wa kila mtu kupata ulichopanda
 
Hapa kinachoongelewa sio Mshahara bali ni bahashishi na marupurupu

Yeye ataombaje marupurupu wakati muda ni mwezi wa sita? Kumbuka kauli yake alisema kalipwa mpakamwezi wa tano na spika kasema aklipwa mpaka mwezi wa sita, sasa abishe kama hajalipwa mwezi wa sita?
 

Haki ya wananchi wake ni kuwawakilisha huko bungeni, jukumu hilo alilitekeleza vyema mpaka aliposhambuliwa na mabaradhuli wenye kiburi cha madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…