- Source #1
- View Source #1
LISSU KWENYE UKURASA WAKE WA X (TWITTER) AMENENA MAZITO ASEMA HATA AKIBAKI MWENYEWE CHADEMA ITASONGA.
Hayo yamekuja mara baada ya viongozi mbalimbali wa Kanda wa CHADEMA kujiuzulu kwa madai ya Chama chao (CHADEMA) kukosa Muelekeo na Kwenda kujiunga na ACT wazalendo ili kuongeza nguvu kwenye chama chenye nia ya mabadiriko ya kweli sio kwa Sasa CHADEMA imejifia kifo cha asili sema viongozi taifa hawataki kusema ukweli.
Hayo yamekuja mara baada ya viongozi mbalimbali wa Kanda wa CHADEMA kujiuzulu kwa madai ya Chama chao (CHADEMA) kukosa Muelekeo na Kwenda kujiunga na ACT wazalendo ili kuongeza nguvu kwenye chama chenye nia ya mabadiriko ya kweli sio kwa Sasa CHADEMA imejifia kifo cha asili sema viongozi taifa hawataki kusema ukweli.
- Tunachokijua
- Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano kwa baadhi ya wana CHADEMA, mathalani tarehe Februari 18, 2025 mmoja wa makada wa chama hicho, Lembrus Mchome aliwasilisha pingamizi la kupinga uteuzi wa viongozi watendaji wa juu wa sekretarieti na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho uliofanywa na Mwenyekiti Tundu Lissu Januari 22, 2025 akidai kuwa umekiuka katiba ya chama hicho.
Ambapo baada ya taarifa hiyo katibu mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika alieleza kuhusu madai hayo kupitia ukurasa wake wa X aliandika.
"Kuna mkakati wa kuhamisha mwelekeo kutoka #NoReformsNoElection . Maamuzi ya Baraza Kuu @ChademaTz ya tarehe 22 Januari 2025 ni halali kwa kuwa Mkutano ulikuwa na wajumbe halali 234 kati ya 412 sawa na asilimia 56.8 kwa mujibu wa Katiba ibara ya 6.2.2.
Kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e) na hakukuwa na agenda ya uchaguzi.
Nakala ya barua tajwa kupelekwa kwa Msajili kunaashiria nia ovu iliyoko nyuma ya pazia."
Madai
Kumekuwapo picha inayoonekana kuwa chanzo chake ni mtandao wa X, ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuonesha kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Lissu amechapisha akieleza kuhusu vuguvugu linaloendelea Chadema likiongozwa na Boniface Jacob. Inaonesha pia akieleza kuwa yeye ni “One Man army” na amewataka watu wajifunze kwa Ntobi.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia kwa njia ya mtandao ikiwemo kupitia ukurasa wa X zamani Tweeter wa Tundu Lissu na kubaini kuwa screenshot hiyo si ya kweli. Aidha aina ya mwandiko (font) uliotumika katika screenshot hiyo si unaotumika na mtandao wa X na badala yake ni ya kuhaririwa.
Madai yanayoonekana katika taarifa hiyo kuwa Lissu ameandika atawashughulikia wananchama hao kama ilivyokuwa kwa Ntobi siyo sahihi. Emmanuel Ntobi alikuwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga ambaye alivuliwa nafasi hiyo na kamati tendaji ya chama hiko kutokana na utovu wa nidhamu wakati wa kampeni kipindi ambacho Lissu alikuwa mgombea tu na si mwenyekiti. Tazama hapa
Chadema pia haijatoa taaarifa yoyote kuhusu kuwepo kwa viongozi wa kanda wa chama hiko wanaotaka kujiuzulu.