Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu Tundu Antiphas Lissu amesifu zoezi zima la upigaji kura lilivyoenda muda mfupi baada ya kupiga kura majira ya Saa 8 na nusu mchana kwenye Kituo cha Kijiji cha Mtewa Kilichopo kata ya Ntutu Wilayani Ikungi, Singida.
Tundu Lissu amesema "Nimetoka Dar es Salaam ili kuja kupiga kura mahali ambapo nilikuwa Mbunge kwa vipindi viwili, mahali ambapo nina marafiki wengi na hawa ni watu wangu kwahiyo nilitaka nije niwe pamoja na watu wangu kwenye zoezi hili muhimu katika nchi yetu. Zoezi limekwenda vizuri, nafikiri kwa jinsi nilivyoona utaratibu umekwenda vyema sana."