Acha kuwa "BIASED", tumia elimu yako kihaki na weledi.
CCM wameitia "DOA" nchi yetu, doa lisilofichika wala kufutika milele. Nchi hii imeshuhudia "WIZI na UONEVU" katika chaguzi nyingi sana, ila huu wa 2020 ni umevuka mipaka. Tumejenga "MAADUI" wengi sana wa mataifa yenye nguvu tokea 2015 mpaka sasa, na hatujaonesha dalili wala juhudi za kutuliza hii hali, bali tumeongeza uadui wa raia.
1) Mawasiliano kuminywa - Kwa hili tujindae kuwekewa vikwazo na nchi nyingi sana duniani.
2) Watu kuuliwa - Zanzibar tumeshuhudia watu wamepigwa risasi na askari polisi.
3) Watu kutekwa - Tumeshuhudia viongozi wakitumia plate number ya UNITED NATIONS kufanyia uhalifu. Hii ni kuichafua UN na KUIDHIHAKI.
4) Kura za wizi - Tumeshuhudia Kawe/Kigoma/Zanzibar kura za wizi zikikamatwa na raia.
CCM lazima itajitangaza kushinda kwa kishindo (Kama wewe ulivyoandika), na watajiapisha kwa mabavu kuanzia Urais/Ubunge/Udiwani. Ila madhara yake unayajua vizuri sana kwa nchi yetu yatakayotufika.
1) Dunia itatoa tamko la "KUTOKUMTAMBUA RAIS NA SERIKALI YA TANZANIA.
2) Dunia itatoa tamko la "UCHAGUZI HAUKUA WA HAKI" na urudiwe.
3) Dunia itatuwekea "VIKWAZO" vya kiuchumi.
NB Tanzania tunategemea "UTALII" kupata fedha za kigeni na kuchangia kwa asilimia nyingi kwenye budget yetu. Wakitupiga pini kwa kuzuia watalii hapa tu, wametumaliza na nchi inaanguka vibaya.
#CCM mnaiga kwa Zimbabwe, ila mnajifanya mmeshau walichokipata.
Mtu mmoja analiangusha taifa, na nyinyi mmekalia "UONGO NA UNAFIKI" kusifia visivyo sifika, ili mpate kazi/ajira. Njaa mbaya sana.