Lissu ataka kukutana na Mashahidi wake watatu kabla ya kuendelea na kesi

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Katika hatua ya kuendelea kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mhe. Tundu Lissu, Mahakama Kuu imeendelea na hatua ya re-examination ya shahidi wa upande wa utetezi, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.

Baada ya Jaji Ndunguru kumweleza Mhe. Lissu kuwa bado ana mashahidi watatu na kwamba mahakama ilitarajia upande wa utetezi kuwasilisha final submissions siku ya Ijumaa, Mhe. Lissu alisema bado anahitaji muda wa kukutana na mashahidi wake hao ili kupanga mkakati wa kesi.

«“Kwanza hao mashahidi wangu nahitaji kuonana nao ili tupange mkakati wa kesi yetu.”»

Mashahidi hao watatu waliotajwa na Mhe. Lissu ni:

1. IGP Camillius Wambura – Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
2.
2. CDF Jenerali Jacob John Mkunda – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania.
3.
3. DCI Ramadhan Kingai – Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Kauli hiyo ilizua vicheko ndani ya ukumbi wa mahakama, huku Mhe. Lissu akisisitiza kwamba anahitaji kukutana na mashahidi wake kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata za kesi.

Awali, Jaji Ndunguru alimwambia Mhe. Lissu kwamba mahakama inaamini atakuwa na maswali machache katika hatua ya re-examination ya John Heche.

Mhe. Lissu, kwa upande wake, alijibu kwa utani:

«“Niko tayari Waheshimiwa Majaji, ila inategemea na speed ya nyie kuandika pia, maana mimi ndiye niko gerezani kule, sio Sheraton Hotel.”

Kesi inaendelea huku Mhe. Lissu akiendelea na re-examination ya shahidi John Heche, kabla ya upande wa utetezi kuendelea na mashahidi wake watatu waliobaki.
 
Hao ni hostile witnesses. Wanaweza kuitwa mahakamani kwa summons. Je wanaweza kulazimishwa kukutana na Lissu
uwezi wasema ni hostile witnesses wakati bado hawaja panda kizimbani ili ku establish element za hostile witnesses .
Apa patamu tuweza kwenda kupata precedent kadhaa ikiwa waki shindwa ku obey summons za mahakama inabidi wawe delt kama mashahidi wengine wasio na vyeo wala majina walio shindwa kutii.
 
Insha Allah
 
Kwenye maisha penda kuwa fanyia watu unachopenda kizuri au kibaya Utajua mwenywe

Ila usisahau kuwaweka watu kwenye kona ya kujipigania maisha.. Utafeli tu

Mode viumbe duniani ukiruka mstari tu utakutana na kitu usichotarajia

Paka ni mpole ukimuelewa na akakuelewa ila ukimkaza kwa kona kona ataishi na wewe vizuri tu

NB: tusipende kupeleka wapendwa wetu kwa kona matokeo hutoyapenda
 
Wakikaidi wito wa mahakama; hiyo ni faida kwa mshtakiwa.

Kwa hiyo itabidi watokee mbele ya mahakama kutoa ushahidi.

Na hili la kusema 'hostile witness' limetoka wapi hata kabla hawasikia maswali wanayotakiwa kujibu!
Kama wapo walioshinikizwa kufanya maamuzi ambayo walikuwa hawayaafiki; hii itakuwa fursa ya kujielea.
 
Ila TL 😂😂😂🙌🙌🙌🙌
 
Mashahidi hao kesho wanatakiwa wawepo ndani ya mahakama, hawatakiwi kumuhangaisha mshitakiwa wao.
 
Na hiyo ndio sababu mchaga kaita press conference kesho Ili watu watoke kwenye focus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…