Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu wakati akitangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema CHADEMA haina budi kurudisha utaratibu wa ukomo wa Madaraka kwani utaondoa uwezekano wa Viongozi kung'angania madaraka na kuandaa Viongozi wapya, kupatikana kwa mawazo mapya na itapunguza upambe na uchawa ulioshamiri pale kiongozi anang'ang'ania madaraka pale ambapo hakuna ukomo wa madaraka
Ili kutekeleza majukumu yanayodaiwa na mazingira ya sasa ya mapambano ya kidemokrasia CHADEMA inatakiwa kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ambapo kwanza ni Katiba ya Chama hicho, ambapo amesema Chama kimekuwa kikubwa na hakuna hofu ya kukosa uongozi katika nafasi mbalimbali za chama hivyo chama kinahitaji kurudisha ukomo wa mataraka kama ilivyokuwa mwanzo
Aidha, akizungumzia ukomo madaraka katika nafasi za Ubunge na Udiwani. Lissu amesema "Ukomo wa madaraka unahitajika pia katika suala nyeti la Ubunge na Udiwani wa Viti Malaamu." Amesema mchakato na namna ya kuwapata Wabunge wa Viti Maalumu umeleta mgawanyiko katika chama hicho ambapo mara baada ya uchaguzi wa 2020 ilibidi CHADEMA iwafukuze wanachama karibu Viongozi waandamizi wote wa BAWACHA waliorubuniwa ili kupewa nafasi za Viti Maalumu.
PIA SOMA
- LIVE - Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA