Kuna tetesi za chini kwa chini kwamba Mh. Tundu Lissu anaweza kuzuiliwa kugombea Urais. Zengwe linapikwa na watu waleeee, ili Lissu akose sifa za kugombea kama ilivyokuwa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kuna wasiwasi mkubwa sana, kule ndani kwamba Mh. Lissu akiruhusiwa kugombea urais, atampa wakati mgumu bwana yule na huenda akashinda kitu ambacho wengi wenye maslahi binafsi kwenye utawala huu hawakubaliani nacho.
Habari ndio hiyo
Ungechimba kidogo na kunusa hadi hilo unaloliita "zengwe" lenyewe na kisha kuja na critical analysis....
By the way, observation yangu mimi Kitaturu inanipa scenarios ya "mizengwe" ya aina mbili tu inayoweza kumsumbua Tundu Lissu kwa kiwango kidogo sana lakini ikiwa na hasara zaidi kwa wanaotaka kuifanya kuliko washindani wao kuelekea uchaguzi mkuu hapo oktoba, 2020;
1. MOSI, NI ZENGWE LA KISHERIA juu ya kesi mbalimbali zilizoko mahakamani zinazomkabili
Hata hivyo kizingiti hiki ni chepesi na kinachoweza kurukika kwa urahisi kabisa kwa uthibitisho na ushahidi madhubuti kabisa kwa sababu;
å Tundu Lissu kwa takribani miaka miwili na ushee, alikuwa mgonjwa tena ugonjwa wa kufisha. Ushahidi ni nyaraka za kitabibu na picha, sauti nk
å Watasema na ofcoz ndivyo wahafidhina hawa wanavyodai kuwa alishapona muda kitambo lakini hakutaka kurejea nyumbani aendelee na kesi zake. Hii inatuleta kwenye hoja ya usalama. Hili ni jukumu la kikatiba la serikali kupitia Police Force kulinda usalama wa raia na mali zao. Tundu Lissu ni raia wa Tanzania mwenye haki hii pia under very special circumstances....
Bahati njema kumbe serikali kupitia Jeshi la polisi walishaandikiwa mpaka barua kuhusu kumhakikishia jamaa usalama wake ili arudi nchini, lakini hawakujibu lolote...
Pili Ubelgiji alipo TL ina uhusiano wa kibalozi na TZ.....
Kwa ishu ya kimahakama, tujiuluze, je mahakama ilishawahi kumtumia wito TL kumtaka kuja mahakamani Tanzania kwa mashtaka/kesi yoyote?
Kwa ishu ya kumhoji juu ya shambulio lake mwaka 2017...
Je, TZ si mwanachama wa Interpol? Hatujaini mikataba mbalimbali ya kimataifa ya mashirikiano juu ya mambo haya?
Polisi walishindwa nini kutumia mtandao wa polisi kimataifa (Interpol) na ubalozi wa TZ Ubelgiji kutengeneza utaratibu wa kumhoji na kupata maelezo yake na kuwa sehemu ya uchunguzi wao kama wako serious kweli kulichunguza swala hili?..
2. ZENGWE LA KUMUUA KABISA NA KUMMALIZA.
Hii ni hatari zaidi kwao na hili likifanyika damu yake itawatafuna wengi sana wa watawala hawa wa sasa milele na vizazi vyao...
Yaani wasije kujaribu kabisa kumdhibiti huyu jamaa kwa njia hii maana hawatafanikiwa zaidi sana wote watakaoandaa mpango huu, watakufa naye hakika...
Kwa kufupi sana ni kuwa, hili zengwe ni almost IMPOSSIBLE MISSION with so much a negative impacts kwao kuliko mlengwa hakika halitafanikiwa....!!
Zengwe wanaloweza kufanikiwa ni moja tu. Kumwacha Tundu Lissu aendelee na shughuli zake, atumie uhuru na haki zake za kikatiba kugombea huu URAIS wa JMT na CCM na mwisho was siku ifanye mchezo wake was miaka yote. Yaani imwibie kura zake na kumpa Magufuli, na kumtangaza mshindi kwa nguvu kisha tuone itakuwaje....
Wakifanikiwa hili ni heri yao. Lakini mwaka huu ni very unique na kuna dalili zote muhimu kuwa CCM this time inaweza kulala chali ndembendembe ktk hali ambayo hata wao wanaCCM hawataamini kabisa...!!