JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
LISSU: NIMEANDIKA BARUA YA KUTIA NIA KUWANIA URAIS WA NCHI KUPITIA CHADEMA
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema ameshaandika barua ya kutia nia ya kuwania nafasi ya Mkamu wa Rais wa CHADEMA nafasi anayoishikilia kwa sasa pamoja na nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia chama chake.
Amesema hayo alipohojiwa na Kituo cha Crown FM, Agosti 16, 2024, ameongeza kuwa “CHADEMA hakuna mkanganyiko, ni joto la uchaguzi, hizo ni kelele za kawaida kabisa, nimeshawasilisha barua mbili wala hakuna cha kuficha.”
LISSU: CCM WAMENICHANGIA, WAMEPELEKA BENKI, SHIDA IKO WAPI?
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), #TunduLissu amekiri kuwa risiti ya Benki inayoonesha fedha zilizochangwa na Wanachama wa CCM kwa ajili ya kumnunulia gari, vina jina lake na Namba ya Akaunti yake ya benki.
Amesisitiza kuwa wakati wanaomba achangiwe kupata gari hawakuweka masharti ya watu wa kuwachangia, amesema hayo alipohojiwa na Kituo cha Crown FM, Agosti 16, 2024, na kusisitiza kuwa amechangiwa na Wana-CCM wengi anaowafahamu na ambao hawafahamu.