Kwani mkurugenzi wa NEC kwa mujibu wa katiba anapaswa kuwa na sifa gani? Nauliza tu,I know magu ana phD ya kuokota watu majalalani
Tume inaundwa na Wajumbe saba (7), miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au
Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni
mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu
anayetoka sehemu ya pili ya Muungano. Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2)
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Kifungu cha
4(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka miongoni mwa Wanachama wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) na Wajumbe wengine
wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia na
kuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri
ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume.