Mungu Ibariki Tanzania!
Eee Mungu eeh, Ibariki Tanzania! Njoo huku!
CCM must go!
Pamoja na kuwa mkataba unawapa nyenzo na mamlaka Kampuni ya watu binafsi kuilazimisha Serikali ya Tanzania kufanya maamuzi magumu kama ya 'kuwataarifu' kuhusu hatua zezote zile Serikali itakayochukua, yaani....
Tanzania itaijulisha DPW juu ya fursa zozote zilizopo, na zitakazokuwepo sasa na baadae.
Basi,sasa Wananchi nao kwa sauti moja, watoe na kuitaarifu CCM, kuwa nao, Wananchi watafanya maamuzi magumu na kuwapa taarifa kuwa CCM hawatachagilika hapo baadae.
Sasa, kwa muktadha huo, itakuwa sahihi kwa Wananchi wote waendelee kudumisha amani na utulivu, umoja na mshikamano, kwa kulinda Katiba.....na maadili na utamaduni zetu na rasilimali zetu kuwajulisha chama cha mapinduzi, kuwa fursa zezote zile walizobakiwa nazo na fursa zezote zile zitakazo kuwepo hapo baadae, kuwa, itawa taarifu Umma/Wananchi, kuwa ifikapo Tarehe itakayotangazwa na uwepo wa Uchaguzi, kuwa, kama Chama kilichopo madarakani, kuwa, kitatota taarifa kuwa Chama kipigiwe kura iwapo tu, kilisharudisha Mkataba bungeni ujadiliwe kwa mapana na marefu, kwamba, kimeondoa vipengele tajwa na tata katika mkataba unaojadiliwa na mijadala yote nchini, na kuwa pia,kitaondoa wingu, jinamizi, laana , shetani, tandabuli la na hofu, waliouleta na kwa, manufaa ya Nchi na Wananchi wake, kuwa, limerudisha matumaini na matamanio ya wananchi kwa Serikali yake, kuwa, kinyume na hayo, kuwa, Mkataba wake na Wananchi utakoma kwa njia ya Kura.
Kwamba, Wananchi watapiga kura yao na kuwaondoa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuchagiza mkataba hovyo kutokea Nchini kutoka madarakani.
Chagua kwa Uangalifu na Umakini mkubwa 2025.
Amani ikutandae