Uchaguzi 2020 Lissu baada ya kuiteka ngome ya Kanda ya Ziwa, una kazi moja tu ya kuiteka Dar es Salaam umalize biashara hii mapema

Uchaguzi 2020 Lissu baada ya kuiteka ngome ya Kanda ya Ziwa, una kazi moja tu ya kuiteka Dar es Salaam umalize biashara hii mapema

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
No doubt Ngome ya kisiasa ya raisi Magufuli ya Kanda ya Ziwa imetikiswa sana na mashambulizi ya kampeni ya Lissu

Hii kanda ndiyo iliyokuwa muhimu sana kumsaidia Magufuli kubalance nguvu za upinzani katika kanda ya kaskazini na miji mikubwa ya Dar na Mbeya, huku akitegemea mikoa loyal kwa CCM kama Dodoma kuendelea kuisapoti CCM.

Hata hivyo equations za kisiasa nchini zimeshabidirika, hata huko kwenye kanda ya Ziwe Magufuli ametikiswa

Sasa ndugu Lissu una shughuli kubwa sana mbele yako, nayo ni kuiweka Dar es salaam katika himaya yako!

DAR ES SALAAM BADO IMELALA.

Katika uchaguzi wa nchi yetu, Dar es salaam ndiyo donge nono. Ndiyo mji wenye kura nyingi kuliko mji wowote!

Kwa hivi sasa Dar es salaam ina wakazi zaidi ya milioni tano, hakuna mji wenye idadi kubwa ya watu kiasi hicho. Kwa hiyo inahitajika mkakati maalum wa kuunyakua mkoa huo kisiasa.

Kwa nini Dar es salaam imelala au kupumbazwa kisiasa?

1. Dar es salaam ndiye muathitika mkuu wa propaganda za Serikali ya awamu ya tano

Dar es salaam ndiyo mlaji(consumer) mkuu wa taarifa mbalimbali za habari zikiwemo za TBC na magazeti. hii ni kwa sababu vyombo hivi vimejikita zaidi Dar kwa sababu ndipo kwenye uchumi mkubwa zaidi. Sasa kwa miska hii mitano vyombo hivi vimegeuka kuwa mouthpiece ya propaganda za serikali ya Magufuli, kwa hiyo wananchi wa Dar ambao ni consumers wakuu wa habari nchini wamelishwa propaganda kali za kuwapumbaza, kwa hiyo kisiasa hawajielewi wako confused.

2. Ni Jiji lenye hofu

Kutokana na matendo ya kidhalimu na uonevu na ubabe ya Makonda, mtu aliyekuwa akiyafanya huku haguswi na mtu yoyote na tena anakingiwa kifua, Dar es salaam iliingiwa na hofu ya kuwa active kisiasa, Vijiwe vya Kahawa vikaogopa kuisema serikali, Watu wakahofia kutekwa na kupotezwa. Kwa hiyo mji ambao ulikuwa active sana kisiasa kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma leo hii umelala doro mno kisiasa sababu ya hofu.

3. Kukatishwa tamaa na serikali baada ya chaguzi za marudio

Chaguzi za Marudio za Kinondoni na Ukonga ambazo wananchi wa Dar walikuwa bado na mwamko wa kushiriki siasa, zilishuhudia uporaji na unajisi mkubwa wa mchakato wa uchaguzi, matendo haya yaliwademoralize (kuwavunja moyo) watu wa Dar es salaam na kuanza kupoteza imani katika siasa

4. Kushindwa kwa Lowasa mwaka 2015

Kama kuna miji ndani ya nchi yetu iliyompokea Lowasa kwa mikono miwili, na kama kuna mikoa iliikataa CCM kwa mikono miwili ni Dar. Dar iliweka moyo wake mkubwa katika mabadiriko mwaka 2015, Kitendo cha hilo jambo kutofanikiwa pia kiliinyong'onyesha sana Dar na kuanza kuwapa wananchi wasiwasi wa kuwa labda haiwezekani kuitoa CCM Madarakani

5. Miradi anayojenga Magufuli Dar

Hizi Flyover, Barabara etc wananchi wa Dar zinamake sense kwao kwa sababu huu ndo mji wao, kwa hiyo hii miradi kisiasa inamuongezea Magufuli credit kwa wakazi wa Dar

6. Kutowasumbua wamachinga

Dar ndo mji wenye machinga wengi zaidi, pamoja na kile kitambulisho cha magumashi cha 20000, Wamachinga wameweza kufanya shughuli zao kwa uhuru mkubwa hapa Dar, hilo pia limemuongezea Magufuli credit kwa kundi hili la mkoa wa Dar

7. Kutokuweka Lockdown kipindi cha Korona

Kama kuna kitu kinampa Magufuli credit katika mkoa wa Dar ni kutokuweka Lockdown watu kipindi cha Korona, Kama ingewekwa Lockdown muathirika wa kwanza wangekuwa watu wa Dar, kwa hiyo rating ya Magufuli iko juu ajabu kwrenye ishu ya kutoweka Lock down Dar

8. Kupungua kwa vitendo vya ujambazi Dar

Kabla ya Magufuli hajaingia Madarakani, hali ya ujambazi Dar iliuwa inatisha, zilikuwa hazipiti siku tatu unasikia tukio, Sasa hivi uwongo mbaya hali ni nafuu sana

NAMNA YA KUMSHINDA MAGUFULI DAR

1. Endelea kupiga Spana ishu ya Maslahi ya watumishi wa Umma

Dar ni mji wenye watumishi wa umma wengi zaidi kuliko mkoa wowote nchini, ni lazima kuendelea kulishawishi kundi hili kuwa Serikali ya Magufuli haikuwa rafiki yao

2. Kundi la Wafanyabiashara na Wajasiriamali

Kundi hili nalo ni kubwa, ndiyo wanaomiliki biashara mbalimbali, wengi biashara zao zimeathirika sana. Inahitajika sana Lissu akija Dar aje na majibu ya madhila yao, aeleze kwa plan zilizo detailed namna atakavyowasaidia, asije na statement za jumla jumla aje na plan detailed

3. Kundi la Influencers (washawishi)

Hili ni kundi mtambuka, ni kundi linalohusu waleta ugali nyumbani wakiwemo wafanyakazi, wafanyabiashara, wasomi hawa ni muhimu sana kuwashawishi na kuwaomba wawe mabalozi wakubwa wa kuinflunce watu walio kwenye himaya zao za ushawishi wakuunge mkono

4. Dar Ilishuhudia matendo ya kikatili ya kuwavunjia watu nyumba

Hili suala liliumiza wakazi wengi wa Dar, Wahanga na wasio wahanga, Lissu akija Dar alizungumze hili kwa nguvu sana kila mahali ili kuonyesha ubaya wa serikali hii

5. Kuwavutia wamachinga

Lissu akija Dar aendelee kupigilia spana kitambulisho cha wamachinga, na aje na idea za kuwarahisishia wamachinga kufanya biashara zao. Yaani hapa aje na plan kubwa ya kuwashawishi Wamachinga namna ataavyowarahisishia biashara.

6. Lissu akija Dar lazima afanye mikutano mingi zaidi ili kuamsha ari

Dar inahitaji dedicated time, Lissu akija Dar asiishie kufanya mikutano miwili mitatu Dar, Dar inahitaji mikutano kila mahali ili kurejesha morali ya umma

7. Lissu akija Dar awakumbushe watu gharama za miamala ya fedha ya MPESA, TiGo Pesa etc Gharama za data vifurushi n. k

Huu mkoa ndo consumer mkuu wa huduma hizo nchini, Tangu wapandishe makato ya vifurushi hivyo Wakazi wa Dar wamekuwa ni waathirika wakubwa wa makato hayo kwa sababu Dar ndo mji mtumiaji mkubwa zaidi wa huduma hizo.

8. Ajira kwa vijana na Makato ya Loansboard

Dar ndo kimbilio la vijana nchi nzima kutafuta maisha mazuri, kiwango cha ukosefu wa ajira kinatisha, Lissu inabidi aendelee kuahidi kupunguza makato Loansboard kutoka 15% hadi 3% na aje na plan iliyo detailed ya kuinua kiwango cha ajira nchini

9. Uonevu wa Matrafiki

Kama kuna Idara serikali ya Magufuli iliharibu ni kwenye kuigeuza Trafiki kama wakusanya kodi kwa kisingizio cha makosa ya barabarani, Yaani badala ya hili suala kuwa reasonable, jeshi la polisi likaanza kujisifu kulusanya mapato kwa kisingizio cha makosa ya barabarani. Watu wametozwa hela sana na matrafiki, Bodaboda na bajaji wamekamuliwa sana hela zao. Kama kuna zawadi ya bure ya kisiasa Magufuli amewapa wapinzani kwenye sahani ni hili suala. Tena alisema zile elfu tanotano wanazochukua matrafiki ni hela za kung'arisha viatu, Lissu akiitumia hasira hii ya wamiliki wa vyombo vya moto ataweza kugeuza tide ya Dar kuwa upande wake

10. Lissu akija Dar amgeuze Bashite kuwa punching bag yake

Makonda ni unpopular sana hapa Dar, Timu ya kampeni ya Lissu itafute skendo kubwa za Bashite na jinsi Magufuli alivyomkingia kifua kisha aonyeshe ni namna gani Magufuli alivyo na double standard kwenye utawala wake, Hili litaclick vizuri sana kwa wananchi

11. Lissu aje na plan ya kuendelea kuthibiti ujambazi Dar

Aeleze kinagaubaga yeye atafanyaje kuendelea kuboresha usalama Dar, kama ni kuinstall CCTV Cameras kila barabara muhimu aseme, lakini kiukweli mkoa wa Dar umepata ahueni kubwa sana katika suala hili la ujambazi Dar, Lissu inabidi aje na counter argument katika hili suala kama anataka kumnyang'anya Magufuli point katika hili suala

12. Kupanda gharama za bidhaa muhimu.

Sasa hivi bei ya sukari iko juu kuliko mwaka 2015, Gharama za ujenzi ziko juu, Simenti imepanda bei sana, Uwezekano wa watu wa Dar kujenga ndani ya awamu hii umeshuka sana.
Vijana waliokuwa wanajajiri katika sekta ya ujenzi, ikiwemo mafundi mbalimbali, wauza tofali sasa hivi wana hali ngumu jijini Dar. Naamini hii point ni muhimu sana kuwashawishi wakazi wa Dar wakuunge mkono.

Kwa hali ya Kisiasa inavyokwenda
Ni dhahiri hali ya kisiasa ya Magufuli kwa sasa siyo nzuri, Lissu ajitahidi aiweke Dar kibindoni the rest will be history
 
Dar karibu kila mtu anamiliki smartphone hivyo kinachoendelea wanajua vizuri sana.

Kingine ni kuwa,mikoani kumewafumbua macho watu wa Dar na kuwaondolea uoga uliokuwepo mwanzoni na kuwatia morari na pia sera anazoendelea nazo Lissu mikoani zinaendelea kuwateka wakazi wa Dar mfano habari ya kikokotoo.

Hata Magu Dar hana mvuto na hiyo miradi sio sababu kwani hata mwaka 2015 wakati wa JK Dar ilikuwa inazindua mradi wa mabasi ya mwendokasi kipindi cha kampeni ila bado Halmashauri zote ziliangukua mikononi mwa upinzani.

Sema pia Dar imekuwa sio active sana kisiasa na hii ni kutokana na siasa za kununua wapinzani na chaguzi kuvurugwa ila sio kama Magu anakubalika.
 
Watanzania hawa hawa au wameteremshwa wengine kutoka mbinguni
Uwa wanajaa sana kwenye mikutano ya wapinzani
Wanasukuma mbaka magari
Wanavua mashati tumbo wazi
Wanajipaka rangi mwili mzima
Tatizo sasa kwenye kupiga kura,,
Ilo ni tatizo la miaka nenda rudi ,,

Wale wauza vitumbua ,wasuka ukili vibarazani, vibabu na vibibi awavui mashati wala awasukumi magari ya wagombea kazi yao ni moja tu kupiga kura ( basi
Wala awasikilizi sera
Tunatumia nguvu kubwa miezi yote 2 mfululizo wao simple tu ndumbwi ..
 
Mkuu Missile ushauri mzuri, ila sina hakika kama Lissu/Wanaomzunguka huwa wanatembelea JF na kuona maoni/Ushauri. Kwa kuongezea watu walikata tamaa ya kupiga kura kwasababu ya mizengwe ya kwenye chaguzi S/mitaa na hasa ule wa 2015.

Hapa T. A. Lissu anapaswa kuwajaza morari wa kupiga kura na namna zitaonesha umuhimu wa wao kupiga kura tofauti na chaguzi nyingine. Hamasa ya kuwafanya watu wakapige kura ni muhimu sana kwa sasa. Mimi na uhakika kwa DSM watu wengi watampigia kura hata wale wa chama cha mapinduzi.
 
Sawa ila Mkuu,nakuhakikishia kuwa tangu Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingine uanze Dar Ni ngome ya Upinzani.1995 majimbo yote kasoro Ukonga tu yalienda Upinzani NCCR wakati huo iko juu.uchaguzi ukarudiwa CCM wakafanya ya Jecha.
Ilibaki kuwa hivyo hata Leo Lissu ana kazi ndogo Sana DSM.
Hofu yangu Ilikua nyumbani tu,lakini nimeshangaa huko Ni Kama kumsukuma mlevi tu, namaana Lakezone.
Lisu Rais kwa ballot box,piga ua.
Sioni Kama Kuna watu wanamhitaji Magufuli kwa hisia Kali,sioni.
 
Mleta mada uko vizuri unanikumbusha enzi zile za Critical analysis. Mlevi mmoja kule twita anasema " Revolution wont be televised" or "Altenative views wont be aired"

Lakini mbona Tunisia Mohamed Bouaziz alipojipiga moto hadharani dunia nzima ilionyesha kwenye TV na ndio ikawa mwisho wa mababeru wa kiarabu kutawala Nchi za kiarabu
 
Poleni sana,sana tena sana! Baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ...ndio mtajua kumbe hamjui....
 
Sawa ila Mkuu,nakuhakikishia kuwa tangu Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingine uanze Dar Ni ngome ya Upinzani.1995 majimbo yote kasoro Ukonga tu yalienda Upinzani NCCR wakati huo iko juu.uchaguzi ukarudiwa CCM wakafanya ya Jecha.
Ilibaki kuwa hivyo hata Leo Lissu ana kazi ndogo Sana DSM.
Hofu yangu Ilikua nyumbani tu,lakini nimeshangaa huko Ni Kama kumsukuma mlevi tu, namaana Lakezone.
Lisu Rais kwa ballot box,piga ua.
Sioni Kama Kuna watu wanamhitaji Magufuli kwa hisia Kali,sioni.

Huenda Dar ni dormant volcano inayohitaji pressure kidogo tu ilipuke. Lissu akija Dar afanye kazi hii, likitokea hilo itakuwa ni mtafutano katika camp ya CCM
 
No doubt Ngome ya kisiasa ya raisi Magufuli ya Kanda ya Ziwa imetikiswa sana na mashambulizi ya kampeni ya Lissu

Hii kanda ndiyo iliyokuwa muhimu sana kumsaidia Magufuli kubalance nguvu za upinzani katika kanda ya kaskazini na miji mikubwa ya Dar na Mbeya, huku akitegemea mikoa loyal kwa CCM kama Dodoma kuendelea kuisapoti CCM.

Hata hivyo equations za kisiasa nchini zimeshabidirika, hata huko kwenye kanda ya Ziwe Magufuli ametikiswa

Sasa ndugu Lissu una shughuli kubwa sana mbele yako, nayo ni kuiweka Dar es salaam katika himaya yako!

DAR ES SALAAM BADO IMELALA.

Katika uchaguzi wa nchi yetu, Dar es salaam ndiyo donge nono. Ndiyo mji wenye kura nyingi kuliko mji wowote!

Kwa hivi sasa Dar es salaam ina wakazi zaidi ya milioni tano, hakuna mji wenye idadi kubwa ya watu kiasi hicho. Kwa hiyo inahitajika mkakati maalum wa kuunyakua mkoa huo kisiasa.

Kwa nini Dar es salaam imelala au kupumbazwa kisiasa?

1. Dar es salaam ndiye muathitika mkuu wa propaganda za Serikali ya awamu ya tano

Dar es salaam ndiyo mlaji(consumer) mkuu wa taarifa mbalimbali za habari zikiwemo za TBC na magazeti. hii ni kwa sababu vyombo hivi vimejikita zaidi Dar kwa sababu ndipo kwenye uchumi mkubwa zaidi. Sasa kwa miska hii mitano vyombo hivi vimegeuka kuwa mouthpiece ya propaganda za serikali ya Magufuli, kwa hiyo wananchi wa Dar ambao ni consumers wakuu wa habari nchini wamelishwa propaganda kali za kuwapumbaza, kwa hiyo kisiasa hawajielewi wako confused.

2. Ni Jiji lenye hofu
Kutokana na matendo ya kidhalimu na uonevu na ubabe ya Makonda, mtu aliyekuwa akiyafanya huku haguswi na mtu yoyote na tena anakingiwa kifua, Dar es salaam iliingiwa na hofu ya kuwa active kisiasa, Vijiwe vya Kahawa vikaogopa kuisema serikali, Watu wakahofia kutekwa na kupotezwa. Kwa hiyo mji ambao ulikuwa active sana kisiasa kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma leo hii umelala doro mno kisiasa sababu ya hofu.

3. Kukatishwa tamaa na serikali baada ya chaguzi za marudio
Chaguzi za Marudio za Kinondoni na Ukonga ambazo wananchi wa Dar walikuwa bado na mwamko wa kushiriki siasa, zilishuhudia uporaji na unajisi mkubwa wa mchakato wa uchaguzi, matendo haya yaliwademoralize (kuwavunja moyo) watu wa Dar es salaam na kuanza kupoteza imani katika siasa

4. Kushindwa kwa Lowasa mwaka 2015
Kama kuna miji ndani ya nchi yetu iliyompokea Lowasa kwa mikono miwili, na kama kuna mikoa iliikataa CCM kwa mikono miwili ni Dar. Dar iliweka moyo wake mkubwa katika mabadiriko mwaka 2015, Kitendo cha hilo jambo kutofanikiwa pia kiliinyong'onyesha sana Dar na kuanza kuwapa wananchi wasiwasi wa kuwa labda haiwezekani kuitoa CCM Madarakani

5. Miradi anayojenga Magufuli Dar
Hizi Flyover, Barabara etc wananchi wa Dar zinamake sense kwao kwa sababu huu ndo mji wao, kwa hiyo hii miradi kisiasa inamuongezea Magufuli credit kwa wakazi wa Dar

6. Kutowasumbua wamachinga
Dar ndo mji wenye machinga wengi zaidi, pamoja na kile kitambulisho cha magumashi cha 20000, Wamachinga wameweza ufanya shughuli zao kwa uhuru mkubwa hapa Dar, hilo pia limemuongezea Magufuli credit kwa kundi hili la mkoa wa Dar

7. Kutokuweka Locdown kipindi cha Korona
Kama kuna kitu kinampa Magufuli credit katika mkoa wa Dar ni kutokuweka Lovkdown watu kipindi cha Korona, Kama ingewekwa Lockdown muathirika wa kwanza wangekuwa watu wa Dar, kwa hiyo rating ya Magufuli iko juu ajabu kwrenye ishu ya kutoweka Lock down Dar

8. Kupungua kwa vitendo vya ujambazi Dar
Kabla ya Magufuli hajaingia Madarakani, hali ya ujambazi Dar iliuwa inatisha, zilikuwa hazipiti siku tatu unasikia tukio, Sasa hivi uwongo mbaya hali ni nafuu sana

NAMNA YA KUMSHINDA MAGUFULI DAR

1. Endelea kupiga Spana ishu ya Maslahi ya watumishi wa Umma

Dar ni mji wenye watumishi wa umma wengi zaidi kuliko mkoa wowote nchini, ni lazima kuendelea kulishawishi kundi hili kuwa Serikali ya Magufuli haikuwa rafiki yao

2. Kundi la Wafanyabiashara na Wajasiriamali
Kundi hili nalo ni kubwa, ndiyo wanaomiliki biashara mbalimbali, wengi biashara zao zieathirika sana. Inahitajika sana Lissu akija Dar aje na majibu ya madhila yao, aeleze kwa plan zilizo detaiked namna atakavyowasaidia, asije na statement za jumla jumla aje na plan detailed

3. Kundi la Influencers (washawishi)
Hili ni kundi mtambuka, ni kundi linalohusu waleta ugali nyumbani wakiwemo wafanyakazi, wafanyabiashara, wasomi hawa ni muhimu sana kuwashawishi na kuwaomba wawe mabalozi wakubwa wa kuinflunce watu walio kwenye himaya zao za ushawishi wakuunge mkono

4. Dar Ilishuhudia matendo kikatili ya kuwavunjia watu nyumba
Hili suala liliumiza wakazi wengi wa Dar, Wahanga na wasio wahanga, Lissu akija Dar alizungumze hili kwa nguvu saa kila mahali ili kuonyesha ubaya wa serikali hii

5. Kuwavutia wamachinga
Lissu akija Dar aendelee kupigilia spana kitambulisho cha wamachinga, Ia aje na idea za kuwarahisishia wamachinga kufanya biashara zao. Yaani hapa aje na plan kubwa ya kuwashawishi Wamachinga namna ataavyowarahisishia biashara.

6. Lissu akija Dar lazima afanye mikutano mingi zaidi ili kuamsha ari
Dar inahitaji dedicated time, Lissu akija Dar asiishie kufanya mikutano miwili mitatu Dar, Dar inahitaji mikutano kila mahali ili kurejesha morali ya umma

7. Lissu akija Dar awakumbushe watu gharama za miamala ya fedha ya MPESA, TiGo Pesa etc Gharama za data vifurushi n. k
Huu mkoa ndo consumer mkuu wa huduma hizo nchini, Tangu wapandishe makato ya vifurushi hivyo Wakazi wa Dar wamekuwa ni waathirika wakubwa wa makato hayo kwa sababu Dar ndo mji mtumiaji mkubwa zaidi wa hufuma hizo.

8. Ajira kwa vijana na Makato ya Loansboard
Dar ndo kimbilio cha vijana nchi nzima kutafuta maisha mazuri, kiwango cha ukosefu wa ajira kinatisha, Lissu inabidi aendelee kuahidi kupunguza makato Loansboard kutoka 15% hadi 3% na ia aje na plan iliyo detailed ya kuinua kiwango cha ajira nchini

9. Uonevu wa Matrafiki
Kama kuna Idara serikali ya Magufuli iliharibu ni kwenye kuigeuza Trafiki kama wakusanya kodi kwa kisingizio cha makosa ya barabarani, Yaani badala ya hili suala kuwa reasonable jeshi la polisi likaanza kujisifu kulusanya mapato kwa kisingizio cha makosa ya barabarani. Watu wametozwa hela sana na matrafiki, Bodaboda na bajaji wamekamuliwa sana hela zao. Kama kuna zawadi ya bure ya kisiasa Magufuli amewapa wapinzani kwenye sahani ni hili suala. Tena alisema zile elfu tanotano wanazochukua matrafiki ni hela za kung'arisha viatu, Lissu akiitumia hasira hii ya wamiliki wa vyombo vya moto ataweza kugeuza tide ya Dar kuwa upande wake

10. Lissu akija Dar amgeuze Bashite kuwa punching bag yake
Makonda ni unpopular sana hapa Dar, Timu ya kampeni ya Lissu itafute skendo kubwa za Bashite na jinsi Magufuli alivyomkingia kifua kisha aonyeshe ni namna gani Magufuli alivyo na double standard kwenye utawala wake, Hili litaclick vizuri sana kwa wananchi

11. Lissu aje na plan ya kuendelea kuthibiti ujambazi Dar
Aeleze kinagaubaga yeye atafanyaje kyendelea kuboresha usalama Dar, kama ni kuinstall CCTV Cameras kila barabara muhimu aseme, lakini kiukweli mkoa wa Dar umepata ahueni kubwa sana katika suala hili la ujambazi Dar, Lissu inabidi aje na counter argument katika hili suala kama anataka kumnyang'anya Magufuli point kstia hili suala

Kwa hali ya Kisiasa inavyokwenda
Ni dhahiri hali ya kisiasa ya Magufuli kwa sasa siyo nzuri, Lissu ajitahidi aiweke Dar kibindoni the rest will be history
Nina uhakika Lissu akishuka Dar sasa patatetemeka kwani wakati ule watu walikuwa bado hawajahamasika sasa watu hadi vijinini wamepata mwamko.
 
Dar es salaam inatakiwa majimbo kama kigamboni,ukonga,ubungo,segerea hayapewa kipaumbele sana .inatakiwa afanye kata kwa kata watu dar wanashindia mihogo kwa ajili ya ugumu wa maisha hili aliseme waziwazi na atoe mifano hai pia gharama za matibabu aoneshe jinsi muhimbili inavyokataa kutoa maiti hadi pesa ilipwe
 
Nina uhakika Lissu akishuka Dar sasa patatetemeka kwani wakati ule watu walikuwa bado hawajahamasika sasa watu hadi vijinini wamepata mwamko.
Kwa ufupi ni kwamba watu wa MIKOANI ndio wameleta hamasa kwenye KUUSAKA UHURU WA KWELI 2020.

Mungu atie Barka Kwenye Ukombozi huu na awafanye Jamaa Washindwe na Waregee kabisaa
 
Poleni sana,sana tena sana! Baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ...ndio mtajua kumbe hamjui....
Tunajua apo ndio ukomo wa akili zako lakini nakuambia unaweza kufanya jambo kubwa na jema zaidi ya hapo.

Pole sana team ya kuabudu ndio mnakwenda hiyo!
 
Hyo number 8 ni kero na janga Sana haya Mambo ya Loan board ni msiba wa wengi asilisahau hilo
 
Back
Top Bottom