Uchaguzi 2020 Lissu baada ya kuiteka ngome ya Kanda ya Ziwa, una kazi moja tu ya kuiteka Dar es Salaam umalize biashara hii mapema


Tushamsukumia ushauri huu..

@CHADEMA
 
Hyo number 8 ni kero na janga Sana haya Mambo ya Loan board ni msiba wa wengi asilisahau hilo

Loansboard ni tatizo, ile retention fee ya 6% na makato ya 15% ni msumari mzito wa umasikini katika shingo ya walalahoi.
 

Robo ya wapiga kula hipo kanda ya ziwa mfano wasukuma ndio kabila kubwa tanzania hata ukiingia kwenye wikipedia.ukiweza kupata kanda ya ziwa uko kwengine unateleza
 
Sasa hivi kuna kazi mbili au tatu tu anazotakiwa kuziwekea mkazo Tundu Lissu na chama chake, wakishirikiana na wote kwenye upinzani walio na msimamo.

Mambo hayo mhimu ni kama yafuatayo, katika mpangilio huo huo wa umhimu, ukianza na mhimu zaidi.

1. Kutafuta mbinu na njia za kuhakikisha watu wengi sana wanajitokeza kwenda kupiga kura hiyo tarehe 28. Asisitize katika mikutano yake yote umhimu wa kwenda kupiga kura.

2. Kuhakikisha kura zote zitakazopigwa haziharibiwi na mtu yeyote. CHADEMA na wenzao watafute kila njia ya kuhakikisha kuwa kila mbinu itakayotumika kuvuruga kura inadhibitiwa, na hata kama haiwezi kuzuiwa lakini ushahidi wa wazi na usiotiliwa shaka wa kuvurugwa kura wanao na wanaweza kuutumia kudai haki zao.

3. Lissu aendelee na ratiba yake bila kujali Dar au kwingine kokote. Kama Dar wanajiweka ujinga, basi ujinga wao utaondolewa na waTanzania walio wengi, ambao wapo vijijini. Hata hivyo Dar hawawezi kuwa vilaza kama anavyotaka kutuaminisha mleta mada hii.

4. Mambo yanayoelekea kuleta vurugu kwenye uchaguzi huu, Tundu Lissu na Vyama vyote vya upinzani wayatambue. Hii inaonekana ni mbinu ya kuokoa jahazi linalozama. Asikubali kuingia kwenye mitego ya hila ili kuvuruga kasi yake anayojizolea kwa wananchi.

CCM sasa hivi wapo radhi kutumia mbinu yoyote kuwavuruga wapinzani, hasa Tundu Lissu. Watamtafutia kila mtego wamnase, au kumlazimisha avuruge kasi yake.

5. Jumuia za kimataifa ni lazima waendelee kujulishwa yote yanayotokea kwenye kampeni hizi na mbinu zote zinazotumika kuharibu uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…