Mkuu, inaonyesha ya kuwa wewe unaishi kwa mazoea na unaamini sera za CCM tu ndizo hasa zinapaswa kufuatwa. Fikra zako zipo ndani ya kasha, kwa kuwa huwezi kuona chochote kile chema nje ya kasha, yaani madhaifu ya watawala wa chama chako.
Viongozi wa CCM hawana sera zenye mvuto kwa wananchi, ndiyo maana wanajificha ktk maendeleo ya vitu, ijapokuwa hawatoi taarifa sahihi kuhusu kukua kwa deni la taifa na matumizi ya kodi za Watanzania kuendana na hayo mambo ya kawaida kufanywa na serikali yoyote makini hapa duniani.
Kuwa ndani ya kasha la fikra hakuta badilisha watu makini na wenye sera mbadala kuweka bayana mapungufu ya sera za CCM. Mtizamo wa jumla kuhusu maendeleo yenye tija kwa watu ndiyo kitu Watanzania wanahitaji kukisikia.
Makundi tofauti ya kisekta yameumizwa na hata kyathirika sana na sera mbovu za CCM kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Sera hizo hizo mbovu bado kwa mara nyingine tena zinazidi kukumbatiwa na watawala, na zikipingwa hadharani zinaonekana kuwa ni matusi.
Waache wananchi wasikilize sera mbadala hata kama makada wa chama tawala mnaamini kuwa si sera. Wananchi ndiyo wenye uamuzi kwa kile ambacho wanalishwa kupitia kunadiwa kwa ilani tofauti za vyama ktk nyakati hizi za kampeni za uchaguzi.