Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?
Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?
Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?
Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].
Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?
Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.
N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.