Lissu haelewi maana ya ‘Jeshi la Akiba’?

Lissu haelewi maana ya ‘Jeshi la Akiba’?

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
32,246
Reaction score
31,176

IMG_20200903_042901_257.jpg
IMG_20200903_042924_543.jpg
 
Majeshi yanaundwa na Katiba ya nchi na sheria. Huwezi tu kuamka ukaanza kujiita wewe ni jeshi.

Kama hilo jeshi la akiba halipo kwa mujibu wa sheria, basi ni jeshi batili na haramu (kama jeshi la wasiojulikana? hehehe).

Kuwepo kwake ni swala moja, lakini uhalali wake ni swala la pili.

Lipo ndio, lakini je, lipo kwa mujibu wa sheria ipi?
 
Majeshi yanaundwa na Katiba ya nchi na sheria. Huwezi tu kuamka ukaanza kujiita wewe ni jeshi.

Kama hilo jeshi la akiba halipo kwa mujibu wa sheria, basi ni jeshi batili na haramu.

Kuwepo kwake ni swala moja, lakini uhalali wake ni swala la pili.

Lipo ndio, lakini je, lipo kwa mujibu wa sheria ipi?

Si kila kitu kinandikwa kwenye sheria...jeshi la akiba ni kamandi ya jeshi la wananchi wa tanzania ambapo majeshi mengine ni majeshi ya nchi kavu,majini na anga.

Kukuthibitishi hilo ndo maana mkuu wake ni afisa wa jwtz na linasimamiwa na jwtz na linapewa mafunzo na jwtz. Na vitambulisho vyao vinasainiwa na afisa wa JWTZ.

Sawa sawa na kusema leo jeshi la wanamaji limeanzishwa na sheria ipi...hitimisho jeshi la akiba ni moja ya kamandi ya jwtz na inasimamiwa na jwtz na linasimamiwa na sheria iliyoanzisha JWTZ na si jeshi linalojitegemea.
Jeshi kamili ni moja tu nchini tanzania kwa maana ambalo litasimamia na kutoa maelekezo na kupiganisha vita ktk uwanja wa medani,mengine ni majeshi usu na mengine ni kampuni za ulinzi na vingine ni vikundi vya jamii vya ulinzi kwa kuzingatia muktadha wa maana ya neno jeshi tafsiri ni nyingi kutokana na ain ya ujumbe unaotaka kuupeleka kwa jamii.
 
Ukweli ni kwamba kumezuka majeshi mengi ya ajabu ajabu...

Kuna moja nimesikia sijui wanaliita jeshi la magufuli? Vijana wa magufuli?

Lingine jeshi la ccm? wale wanaovaa manguo ya kijani na mabuti makubwa.

Kuna kikosi kazi cha bashite (as he then was).

Hivi vikosi vya ajabu ajabu ni vikosi haramu na ni chanzo kikubwa cha ghasia.

Majeshi ya kihuni huni ni hatari kwa mustakabali wa amani ya nchi. Yapigwe vita na yeyote mwenye akili timamu.
 
Ukweli ni kwamba, KILA KITU kinaandikwa kwenye sheria.

Na ukweli ni kwamba, majeshi yote HALALI ya nchi yanatambulika na Katiba ya nchi.

Kama kuna jeshi lolote halitambuliki kwenye Katiba ya nchi, ujue hilo ni JESHI HARAMU NA BATILI.
...."Mafunzo ya wanamgambo yalianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mgambo ya 1963 ya kulipatia jeshi raia wa Tanzania, wakulima na wafanyakazi waliotayari kulinda nchi yao kama moja ya sehemu za JWTZ. Azma ya Wanamgambo ni kujenga moyo wa uwajibikaji na kujivunia taifa kwa wananchi kwa kuwakaribisha wananchi kutoa mchango wao katika ulinzi wa nchi."
Tovuti Kuu ya Serikali.
 
Huyu alielewa kwa nini JKT kwa mujibu wa sheria alipewa force number?
Kwahyo na mie ile force [emoji648], ndo nimekua mjeshi?
Tatizo sio kuwepo kwa jeshi hilo, Bali uhalali wake.

Hebu kua muelewa bas khaaah
 
...."Mafunzo ya wanamgambo yalianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mgambo ya 1963 ya kulipatia jeshi raia wa Tanzania, wakulima na wafanyakazi waliotayari kulinda nchi yao kama moja ya sehemu za JWTZ. Azma ya Wanamgambo ni kujenga moyo wa uwajibikaji na kujivunia taifa kwa wananchi kwa kuwakaribisha wananchi kutoa mchango wao katika ulinzi wa nchi."
Tovuti Kuu ya Serikali.
Sheria ya mgambo ilishafutwa.

Ipo sheria mpya ya " jeshi la polisi na huduma za ziada".

Hata kwenye sheria ya JWTZ sijaona hilo jeshi la akiba.

Traditionally, tunaweza kuwa na kitu kinachoitwa jeshi la akiba, lakini sidhani kama ni jeshi rasmi.
 
Back
Top Bottom