Si kila kitu kinandikwa kwenye sheria...jeshi la akiba ni kamandi ya jeshi la wananchi wa tanzania ambapo majeshi mengine ni majeshi ya nchi kavu,majini na anga.
Kukuthibitishi hilo ndo maana mkuu wake ni afisa wa jwtz na linasimamiwa na jwtz na linapewa mafunzo na jwtz. Na vitambulisho vyao vinasainiwa na afisa wa JWTZ.
Sawa sawa na kusema leo jeshi la wanamaji limewnzishwa na sheria ipi...hitimisho jeshi la akiba ni moja ya kamandi ya jwtz na inasimamiwa na jwtz na linasimamiwa na sheria iliyoanzisha JWTZ
Wanapofanya kazi za ulinzi wa watu na Mali zao hawaitwi Jeshi la akiba.
Ndio maana wakishahitimu mafunzo wakati wa amani wanakua chini ya polisi na vijini wanafanya kazi za polisi mpaka kukamata. Lakini sio Jeshi la akiba na hawawi chini ya Jeshi la wananchi wakati wa amani isipokua wakati wa vita tuu.
Lisu ni Genius wa sheria tukubali wala tusimshauri vibaya Mgombea uraisi wa CCm ambaye ndiye amiri Jeshi mkuu.
Haya majeshi yakitumiwa kisiasa yataleta matatizo sana. Hakuna atakayekua salama.
Kumbuka wao nao wanahitaji kuishi kwa amani na watanzania wenzao wa vyama vya upinzani kwenye nchi yao. Japo CCM wanataka kutawala tu bila kufuata sheria kwa sababu tu wamefanikiwa kuwateka baadhi ya idara za umma kuwa Mali yao kupitia ahadi za vyeo vya kisiasa.
Kwa nini awamu hii ya tano inayomaliza muda wake imetumia muda mwingi kuwapandikiza makada wa CCM kwenye vyombp vya dola na sheria ili kuhakikisha kuwa wapinzani kwa mamilioni yao wote wanaitwa wahalifu na wanashughulikiwa kama wahalifu japo wapo kisheria?
Je, hali hiyo ya chama tawala na Serikali yake kutumia fedha na ahadi za vyeo kuwaumiza washindani wao italiunganisha taifa na kulifanya moja au italigawa taifa na kuwapa askari wa majeshi yetu shida kubwa ya kuweka mambo Sawa kwa sababu tu kuna wachache wamehongwa vyeo na ndugu au marafiki zao?
Rushwa kubwa sasa kwa CCM imebaki kwenye ahadi za vyeo na madaraka mana huko kuna ulaji na kila mtu anaokoa tumbo lake.
Ndio maana Mungu alimponya Lisu na kuondoa Korona Tanzania ili uchaguzi ufanyike kwa haki tupate viongozi watenda haki wasiojenga ukabila na udini na ubaguzi wa kivyama na kuwanyima Watanzania haki ya kuchagua viongozi wao wanaowataka.