Lissu hashauriki; Walishindwa Jaji Warioba na Raila Odinga kuhusu NRNE


Wewe ama ni mwongo mkubwa au ni miongoni mwa wauaji, au ulipata taarifa zisizo sahihi.

Warioba na huyo jaji wa Kenya walikubaliana na Lisu kuwa tuna sheria mbaya za uchaguzi, na hatuna tume huru ya uchaguzi. Walichoshauri ni kuwa kwasababu muda ni mfupi, badala ya kutaka ipatikane katiba mpya kama alivyokuwa anataka Lisu, kabla ya uchaguzi, kufanyike tu mabadiliko muhimu ya sheria ili kuweza kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Jambo ambalo Lisu alionekana kuwa tayari kuridhia. Ushauri huo huo ndio uliotolewa na Baraza la Maaskofu Wakatoliki. Tatizo kubwa lilikuwa kwa yule mama Muuaji, Chama Cha Mauji na mamluki wao, ambao walikataa kata kata kuwa hawapo tayari kufanya mabadiliko yoyote, wakaamua kuwafanya washauri, Mzee Warioba na TEC, kuwa maadui.

Wakafanya shambulio dhidi ya katibu wa TEC kutaka kumwua, wakaendelea kuwateka, kuwaua na kuwabambikia kesi wote waliokuwa wanashauri uwepo wa uchaguzi huru na wa haki.
 
Na lilikuwa jambo jema sana. Kauli za Lissu ndiyo zimepelekea watu kuuawa 29/10

Awali nilidhani una akili timamu, kumbe ni miongoni mwa yale mahayawani yaliyoondolewa akili na ibilisi shetani.
Mungu Baba laana yako ikawe dhidi ya hawa wauaji wafuasi wa ibilisi wanaojiona ni washindi baada ya kuwaua wanadamu wenzao kama wanyama. Tunaomba daima ukawaoneshe wao na familia zao kuwa wewe ni Bwana wa haki.
 
Sawa, msimamo mzuri
 
Nyinyi mnaotaka maridhiano mbona hamsimamii maridhiano wenyewe. Ni miaka mingi sana kila baada ya uchaguzi mnataka maridhiano kwa maneno kivita mnashindwa. Sasa bakini hivyo kwanini kulazimisha watu wengine.
 
Sio rahisi kufanya mabadiliko ya katiba kabla ya 2030 sababu itawakaanga haohao waliopo madarakani.
 
Mbona kikwete alikataa ushauri wa Warioba na nchi aliiongoza au ni kwa Lisu tu akikataa ushauri hafai. Samia mwenyewe amekataa ushauri wa Warioba lakini ndio Rais wa nchi na mnamsifia!
 
Muasisi wa NRNE ni Mbowe 2021 na ikapitishwa katika mkutano mkuu December 2024 .

Lissu alisimamia kilichopitishwa na mkutano mkuu ambacho ndio kilikua msimamo wa chama na aliwaambia katika mkutano wake wa kwanza 2025 kama wanafikiri anatania basi wajue hatanii atasimamia maamuzi ya kamati kuu na kama kamati kuu iliamua basi yeye kazi yake ni kusimamia kile kamati kuu imepitisha.

Utaendaje kwenye uchaguzi wakati wagombea wako wanaenguliwa eti hawajajaza fomu vizuri halafu wa CCM wote wanapita wote kwa madai eti wa CHADEMA hawajui kusoma vizuri huu si upuuzi wa karne?

Unaendaje kwenye kinachoitwa uchaguzi na anayesimamia ni mteule wa executive na kapewa maelekezo hata ukishinda atangazwe wa kutoka kwa anayeteua.

Ukianza kuleta mifano ya Odinga nitakueleza vingi na utofauti na ubora wa siasa za Kenya kwa upinzani kutokana na katiba yao bora.

Leo hii Gachagua angekua Tanzania angekua ameshauwawa , amekimbia nchi au kuzuiwa kufanya mkutano popote.

Lakini Kenya hiyo hiyo Gachagua ameunda chama kipya na hakina hata miaka 2 kimeshinda uchaguzi wa ubunge Ol Kalau kule .

Mimi ninaunga mkono NRNE na namuunga mkono TAL aliyesema ataisimamia hii ni kwa watu timamu tu ndio tunaweza kuelewa umuhimu wa reforms za kiuchaguzi zinavyoweza kuisaidia nchi isitumbukie katika machafuko.
 
Hii laana ya mwendawazimu wewe inaishia humu humu JF. Hamuwezi kuchoma miundombinu ya umma mkachekewa eti mnadai Katiba!!
 
Nyinyi mnaotaka maridhiano mbona hamsimamii maridhiano wenyewe. Ni miaka mingi sana kila baada ya uchaguzi mnataka maridhiano kwa maneno kivita mnashindwa. Sasa bakini hivyo kwanini kulazimisha watu wengine.
Hii siyo mada ya maridhiano bali inaonyesha jinsi Lissu alivyopasua kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…