Lissu: Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni/Mungu ni wao

Lissu: Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni/Mungu ni wao

Ikiwa ni kweli Lissu alifanya mambo hayo yote, kwa nia ya kweli, bila kujitukuza mwenyewe, kwa maslahi ya Watanzania na taifa hili. Bila kuingiza matamanio yake, bila kutumwa na mabeberu, bila kuwa na hila yoyote mbaya dhidi ya taifa hili/lake.
Kwamba Lisu aliamua kutetea Haki bila kutegemea Faida, sio ili awe Rais au ili apate cheo chochote au faida yake mwenyewe bali faida yake alitaka kuona Haki katika taifa hili. Kuona kwa macho yake kizazi bora katika taifa hili kabla ya kuingia mavumbini. Ikiwa hayo ni kweli yote. Basi Ufalme wa Mungu ni wake.
1. Mkuu, inaelekea humjui vizuri lisu. Lisu alivyo mbinafsi hawezi kufanya kitu chochote bila manufaa yake binafsi. Au umesahau kuwa wakati tunapambana na mabeberu ili tuongeze manufaa ya uchimbaji wa madini yetu yeye alikuwa upande/mtetezi wa mabeberu? Upendo wa taifa hapo unatoka wapi?
2. Hawezi kuuona Ufalme wa mbinguni bila kuukana ushoga. Hiyo mbingu ya kuingia mashoga ni mbingu gani? Ushoga ni chukizo kwa Mungu. Sonoma na Gomora ziliangamizwa kwa moto sababu ya ushoga. Acha kumpa kichwa, mhimize atubu
 
Back
Top Bottom