Jaribu kuwa mkweli kidogo mkuu 'Croco.'Kilimo ni ajira!, sijaona kipindi ambacho banks zipo friendly kama wakati huu wa awamu ya sita.
Naomba niseme kwamba leo nakusoma vizuri zaidi kuliko siku za nyuma. Leo umetulia kidogo na maandishi yako yanaonekana kuwa ya msingi sana.
Sasa niambie, mwananchi kule kijijini ataanzia wapi kwenda kutafuta mkopo Benki; na inawezekana kabisa hajawahi hata siku moja kuingia Benki!
Usilete utani mkuu, haya ni mambo muhimu sana.
Serikali imefanya juhudi zipi kuwapanga hawa watu ili waweze kupata mikopo ya Benki. Imewapa 'guarantee' huko Benki ili kuhakikisha Benki ziondoe mashaka juu ya wananchi hawa?