Tetesi: Lissu kugombea ubunge Singida 2025

Tetesi: Lissu kugombea ubunge Singida 2025

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Taharuki na matumbo joto kwa wanasiasa wabunge wa majimbo ya SINGIDA baada ya tetesi hizi kusambaa kama bush fire 🔥...

Ameamua kubadili gia angani mapema, baada ya kutathimini kwa kina, kujiridhisha na kuthibitisha kwamba, mazingira ya chama chake si rafiki na hayampi matumaini, hamasa, wala sapoti ya dhati kuwania nafasi ya uongozi wa juu wa chama wala kipaumbele cha kuwania nafasi ya uongozi wa wa juu serikali, yaani Urais... mnyetishaji alidokeza.

Lakini pia hali ya kisiasa nchini ilivyoelemea upande moja hasa wa chama Tawala na na kudhihirika bayana kwamba, anaetazamiwa kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama Tawala, anauungwa mkono hata na vyama vya kisiasa vya upinzani na kwa hivyo ushindi kwake ni wa wazi hata kama tutasingizia kuibiwa, itakua ni vichekesho kumshinda yule mama mnyetishaji aliendelea kutiririka.

Kwa kiasi kikubwa sana, hii imemkatisha tamaa na, imedhoofisha jitihada na harakati zake za kutaka kuleta na kuchochea mabadiliko nchini, kupitia nafasi ya juu ya uongozi wa nchi, na kwahivyo ameamua kukita kambi SINGIDA, baada ya kukosekana hamasa kwenye siasa za kitaifa, hasa kutoka upande wa upinzani ikiwemo chama chake cha Chadema ambacho kina viashiria vyote vya mgawanyiko miongoni mwao.

Mpango sasa ni kutafuta Jimbo SINGIDA kwajili ya 2025, na ndio maana umeona karibu mwezi mzima tupo hapa. kama mwenyekiti Taifa anajua hili au hajui hilo nadhani siwezi kusema, wao ni viongozi inawezekana wanawasiliana mara kwa mara.
mnyetishaji alidokeza.

Kwa hakika kiongozi huyo ni gineaus anae jua kusoma vizuri sana, upepo wa kisiasa, alama za nyakati na mazingira ya kufanya siasa za kijimbo au kitaifa na kwenda nayo sambamba, kulingana na hali halisi ya wakati ule.

Tunasubiri tamko lake rasmi wakati wowote kuanzia sasa kuthibitisha uelekeo huu.

Mwandishi na mwanasheria msomi moja humu JF, alishauri upinzani hasa chadema kujikita na kuconcentrate kwenye uchaguzi wa 2030 badala ya huu wa mwakani....
Je, huu ndio mwanzo wa ushauri huu kutekelezwa?
 
Nilishawaambia CHADEMA kuwa wasipoteze muda kwenye nafasi ya Urais .maana nafasi hiyo ni maalumu kwa ajili ya Rais Samia ambaye anaungwa mkono na mamilioni ya watanzania ,ambao wanasubiri tu muda ufike ili wampigie Kura za ndio Rais Samia kwa kishindo.
 
Huyo mama, umri wa kustaafu umewadia, kulea wajukuu ni uamuzi Bora sana Kwa sasa.
 
Nilishawaambia CHADEMA kuwa wasipoteze muda kwenye nafasi ya Urais .maana nafasi hiyo ni maalumu kwa ajili ya Rais Samia ambaye anaungwa mkono na mamilioni ya watanzania ,ambao wanasubiri tu muda ufike ili wampigie Kura za ndio Rais Samia kwa kishindo.
"Ni Bora hata tumpe promo Makonda kuliko Mama Kwa sasa!!

Ameshakiuka taratibu za kampeni na kanuni ndani ya chama,ameanza kugombea kabla ya wakati na rushwa ameanza kuzitoa Kwa kusambaza piki piki na bajaji zenye jina lake dhidi ya wagombea wengine!

Amekosea kama makada wetu marehem lowasa na membe!amekiuka taratibu za chama chetu !hatoshi kabisa !amevunja kanuni"!

Alisikika kada maarufu akitamka Kwa uchungu sana kuvunjwa Kwa kanuni!
 
Huyo mama, umri wa kustaafu umewadia, kulea wajukuu ni uamuzi Bora sana Kwa sasa.
Umri wa miaka 64 kwa kazi ya urais si umri mkubwa sana. Tumkatae kwa uwezo wake mdogo usiohusiana na umri wake.

Kushabikia vitu petty kama umri, jinsia... katika mambo nyeti kama urais matokeo yake ndiyo hayo mnayoyaona sasa.
 
Andika tu atagombea, UDIWANI kata ya Ikungi ili awe Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na MOYO wako UFURAHI...buku 7 oyeee!
atatoa taarifa rasmi mwenyewe kama amefikia hatua hiyo unayopendekeza, ila kwasasa zingatia hoja iliyopo mezani 🐒
 
Atajijua mwenyewe, mwisho wa siku anapigania tumbo la na familia yake mengine yote porojo tu.
 
Shida ipo wapi? Hata asipokuwa na cheo chochote bado ataendelea kuwa mwanasiasa aliye upande wa wananchi.
hakuna shida kamanda, political dynamics ni mambo ya kawaida kabisa kwenye political scene 🐒

kukosa kila kitu ni sehemu ya matokeo ya mageuzi na mabadiliko katika ulimwengu wa siasa....

so just relax.
hata hivyo imependekeza destination nzuri sana kwamba akae huko kwa wanainchi sasa, maana kwa kiasi kikubwa bado wanainchi hawajamuelewa vizuri labda akikaa nao anaweza fahamu mahitaji ya wanainchi sio kiongozi wa kupambana na mamlaka 🐒
 
Back
Top Bottom