Tetesi: Lissu kugombea ubunge Singida 2025

Tetesi: Lissu kugombea ubunge Singida 2025

taharuki na matumbo joto kwa wanasiasa wabunge wa majimbo ya SINGIDA baada ya tetesi hizi kusambaa kama bush fire 🔥...

ameamua kubadili gia angani mapema, baada ya kutathimini kwa kina, kujiridhisha na kuthibitisha kwamba, mazingira ya chama chake si rafiki na hayampi matumaini, hamasa, wala sapoti ya dhati kuwania nafasi ya uongozi wa juu wa chama wala kipaumbele cha kuwania nafasi ya uongozi wa wa juu serikali, yaani Urais... mnyetishaji alidokeza....

lakini pia hali ya kisiasa nchini ilivyoelemea upande moja hasa wa chama Tawala na na kudhihirika bayana kwamba, anaetazamiwa kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama Tawala, anauungwa mkono hata na vyama vya kisiasa vya upinzani na kwa hivyo ushindi kwake ni wa wazi hata kama tutasingizia kuibiwa, itakua ni vichekesho kumshinda yule mama....... mnyetishaji aliendelea kutiririka....

kwa kiasi kikubwa sana, hii imemkatisha tamaa na, imedhoofisha jitihada na harakati zake za kutaka kuleta na kuchochea mabadiliko nchini, kupitia nafasi ya juu ya uongozi wa nchi, na kwahivyo ameamua kukita kambi SINGIDA, baada ya kukosekana hamasa kwenye siasa za kitaifa, hasa kutoka upande wa upinzani ikiwemo chama chake cha Chadema ambacho kina viashiria vyote vya mgawanyiko miongoni mwao....

mpango sasa ni kutafuta Jimbo SINGIDA kwajili ya 2025, na ndio maana umeona karibu mwezi mzima tupo hapa. kama mwenyekiti Taifa anajua hili au hajui hilo nadhani siwezi kusema, wao ni viongozi inawezekana wanawasiliana mara kwa mara....
mnyetishaji alidokeza....

kwa hakika kiongozi huyo ni gineaus anae jua kusoma vizuri sana, upepo wa kisiasa, alama za nyakati na mazingira ya kufanya siasa za kijimbo au kitaifa na kwenda nayo sambamba, kulingana na hali halisi ya wakati ule....

tunasubiri tamko lake rasmi wakati wowote kuanzia sasa kuthibitisha uelekeo huu....

mwandishi na mwanasheria msomi moja humu JF, alishauri upinzani hasa chadema kujikita na kuconcentrate kwenye uchaguzi wa 2030 badala ya huu wa mwakani....
Je, huu ndio mwanzo wa ushauri huu kutekelezwa?
Acha kuweweseka!
 
Nilishawaambia CHADEMA kuwa wasipoteze muda kwenye nafasi ya Urais .maana nafasi hiyo ni maalumu kwa ajili ya Rais Samia ambaye anaungwa mkono na mamilioni ya watanzania ,ambao wanasubiri tu muda ufike ili wampigie Kura za ndio Rais Samia kwa kishindo.
Hata JPM alipewa za Ndiyo mwaka 2020. Umesahau kuweka namba ya simu yako
 
Acha kuweweseka!
kisiasa ukiguswa mahali flani, hupanic , unatulia kidogo na kujipanga na comeback ya kivingine...

hivi ndivyo unavyoweza kusema, muungwana ameona na kuamua kuchukua hatua... :pulpTRAVOLTA:

na kisiasa its good, kuliko kushupaza shingo kwenye mfupa ambao hauwezekaniki na huna meno hata ya kutafuna hata nyama tyui:pedroP:
 
Back
Top Bottom