Tetesi: Lissu kuhama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa

Tetesi: Lissu kuhama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa

Sasa kam ni kichaka wewe huo moyo wa lisu kichaka chake umekijuaje.
Huna akili wewe
Huyu bwege ndiyo anapishana na teuzi kila siku kwa uzushi wake. Hii habari kila leo inaandikwa na wazushi wa CCM leo yeye kaifanya habari ya kiuchunguzi,mpumbavu sana huyu mshamba.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ni kuwa ndugu Lissu anatarajia kuondoka na kuihama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa.hii ni baada ya kutoridhika na mwenendo na aina ya siasa zinazoendeshwa na ndugu Mbowe. Lissu anaamini kuwa masuala mbalimbali ambayo CHADEMA inayahitaji hasa suala la katiba mpya hayawezi kufanikiwa wala kupatikana kwa kufanya mazungumzo muda wote na CCM au kwa njia ya vikao vya maridhiano ambavyo vimekuwa vikifanywa kati ya CHADEMA na CCM.

Tundu Lissu anadai na kusisitiza ya kuwa CCM haipo tayari kuwapa katiba mpya Watanzania na kwamba haiwezi kujikaanga kwa mafuta yake.lakini pia Lissu anadai ya kuwa Mwenyekiti wake ameshatekwa nyara kiakili na CCM na kwa sasa hana nguvu wala uwezo wa kusimamia misimamo ya chama na ile ya awali.Lissu anadai ya kuwa kwa sasa Mbowe hawezi kuivusha CHADEMA katika kuwaongoza wanachama kupigania kile wanachama wanachohitaji.anasema Mbowe amekipotezea mvuto na ushawishi chama kwa wananchi kwa maamuzi yake ya tamaa na faida za muda mfupi.

Anasema Mbowe anakiburuza chama kwa kutaka mawazo yake ndiyo yaongoze chama badala ya mawazo na mahitaji ya wanachama. Amedai kuwa CHADEMA kupitia mbowe limekuwa kama Tawi tu la CCM. Lissu anasema hataki na hawezi kuwa muhuri wa kuhalalisha mambo ambayo hakubaliani nayo.anasema ni vipi chama kiingie katika uchaguzi kwa katiba ile ile na sheria zile zile na mfanano ule ule na kanuni zile zile na wasimamizi wale wale ambao wamekuwa wakiwaumiza na kuwaonea kila uchaguzi ikiwepo kuengua wagombea wao au kufukuza mawakala wao vituoni halafu wategemee kupata matokeo tofauti na ya 2020.

Hivyo Lissu ameamua kuchukua uamuzi wa kuondoka na kuhama CHADEMA, ili aende chama kingine ambako atakuwa huru kusimamia kile anachokiamini katika mazingira huru na ya amani.maana kwa sasa anadai ya kuwa wakati mwingine Mbowe huwaletea tu maamuzi na kutaka chama chote kuyakubali japo hakikushirikishwa katika hatua zote. Katika Kuhama huko Lissu yupo na viongozi mbalimbali waandamizi ambao atahama na kuondoka nao,ambao wamekuwa wakimuunga mkono na kutokubaliana na misimamo ya ndugu Mbowe. Viongozi hao wengine wamedai kuchoshwa pia na ubabe na vitisho vinavyokuwa vinatolewa na Mbowe pale anapotaka kutimiza na kupitisha ajenda zake.

Mimi Mwashambwa ningependa kusema kuwa kinachoua na kusambaratisha vyama vya upinzani hapa nchini ni kukosa ajenda na sera za kugusa maisha ya watu. lakini pia kuimarika na kuongezeka kwa ushawishi wa CCM kwa wananchi kumekuwa mwiba mkali kwa vyama vya upinzani.. Kwa sasa CCM chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan imekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwa watanzania.hii ni baada ya kuwapa watanzania mambo mengi sana waliyokuwa wanayahitaji.ikiwepo suala la katiba mpya ambalo serikali ya Rais Samia imekubali kufufua mchakato huo, kurekebisha sheria za uchaguzi.mfano sasa wajumbe wa tume ya uchaguzi hawatakuwa wanapendekezwa moja kwa moja na Rais,kufanyiwa usaili kwa wajumbe wa tume ya uchaguzi,kuondoa utaratibu na habari za kupita bila kupingwa na mengine mengi tu mazuri.

Lissu ni lazima akubaliane na ukweli tu kuwa katiba mpya chini ya uongozi wa Rais Samia itapatikana tu na mchakato utaanza,kwa kuwa Rais Samia na serikali yake ameonyesha dhamira hiyo njema ya kuwapatia watanzania katiba itakayoendana na mahitaji ya wakati.ndio maana akaanza na sheria mbalimbali zitakazo weka uwanja sawa katika uchaguzi ,ili kuondoa manung'uniko na malalamiko ya wagombea wa vyama vingine.

Lakini pia ningependa kumshauri Lissu kuwa ni ngumu sana kupata kile anachokitaka katika nchi hii kwa njia anazozitaka yeye za kutumia nguvu,mabavu,fujo, maandamano na siasa kali za jino kwa jino. Hizo ni ngumu sana kwa sasa.kwanza ajiulize atawapata wapi watanzania hao wakuunga mbinu hizo na kutekeleza? Watanzania wa leo hii nani wakuhatarisha maisha yake wakati waliona namna wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na CHADEMA walivyo vigeugeu na wanavyobadilika kama vinyonga baada ya muda mfupi? Lissu ni lazima afahamu na kuisoma vyema historia ya nchi yetu.

Lissu ni lazima afahamu aina ya siasa zetu,aina ya malezi tuliyokulia na kukuzwa,misingi tulioachiwa na waasisi wetu wa Taifa letu na namna ilivyojengwa. Ni lazima Lissu afahamu kuwa misingi ya watanzania siyo ya kupigana sisi kwa sisi.watanzania tumekulia katika mazingira ya amani na kupendana.hakuna mtanzania anayeweza kuwa tayari au kutaka kuona Taifa likiingia katika machafuko kwaajili ya matakwa ya wanasiasa.

Kwa hiyo lissu kama hayafahamu hayo basi ni bora astaafu tu siasa na kuendelea na mambo mengine tu au ajikalie kimya tu.maana hata huko ambako atahamia bado tu hatafanikiwa kwa namna yoyote ile na badala yake ndio ataona mambo yanakwenda Mrama na kombo zaidi na zaidi.watanzania ni wapenda amani sana na hatupo tayari kuipoteza amani yetu. Sisi ni wapenzi na waumini wa maridhiano na kukaa pamoja mezani kumaliza mambo yetu na siyo kwenda barabarani kufanya fujo.

CCM ya sasa ni imara sana na inaeleweka vyema sana kwa wananchi,imeziba mianya yote iliyokuwa inawapa umaarufu na ajenda upinzani na inajenga chuki na kuchukiwa na wananchi. Imejishusha na kujiweka karibu na wananchi,imejinyenyekeza na kujiweka chini ya miguu ya wapiga kura kwa kuwa Sikivu na yenye kuwajali wanyonge.ndio maana inaungwa mkono na mamilioni ya watanzania,ndio maana inapigiwa kura za ndio na ndio maana nguvu ya upinzani imekwisha na siyo tishio tena hapa Nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Pumbavu ,inakuhu nini lissu akiama chadema? Chadema sio mali ya mtu kama ambavyo ccm imekua genge la watu flani ,pumbavu
 
Pumbavu ,inakuhu nini lissu akiama chadema? Chadema sio mali ya mtu kama ambavyo ccm imekua genge la watu flani ,pumbavu
Wala haihitaji hasira bali ni kutulia tu kama unanyolewa. Utake usitake ndio hivyo Lissu ameona hawezi kukaa na ninyi manyumbu msio na akili.
 
Kama CCM ya wakati wa Jakaya Kikwete ilishindwa kuisambaratisha CHADEMA kwa propaganda za dizaini hii, hivi CCM ya "Mama wa Ushungi" na yenye wana propaganda wenye very low profile dizaini yako wewe Lucas Mwashambwa sijui mtawezaje na mtatumia mbinu gani iliyosalia kuisambaratisha CHADEMA hii iliyokwisha simika mizizi yake kitaifa na kimataifa kwa utoto huu wa kipumbavu kiasi hiki..!

Na kama hata ile CCM ya John P. Magufuli a.k.a Jiwe iliyokuja na combination ya wa mbinu zote possible kuanzia propaganda za kusifia na kupaka mafuta viongozi wenu, kununua viongozi wa vyama vya upinzani, waliokataa walitekwa, wakateswa, wakatiwa vilema na wengine kuuwawa yote hiyo ikiwa ni mkakati wa aidha kuidhoofisha CHADEMA au kuiondoa kabisa katika suasa za Tanzania, lakini haikuwezekana na badala yake mwasisi na msimamizi wa siasa hizi chafu yaani Rais John P. Magufuli alipotezwa yeye kwa kuuwawa kwa kifo cha kipumbavu kabisa...!

Lucas Mwashambwa mimi naamini humfahamu wala kumjua Tundu Lissu vyema.

Ni wazi kuwa unafikiri Tundu Lissu ni mwanahakarati na mwanasiasa mzandiki na mnafiki dizaini ya kina Samia Suluhu Hassan, Jakaya Kikwete, John P. Magufuli, Mwigulu Nchemba, Steven Wassira, Zito Kabwe, Lijualikali, Kangi Lugola, Nape Nnauye au Paul Makonda eti eeh??.....NO WAY...HUJUI LOLOTE. Na kama unabisha, basi jua tu kuwa hii ndoto yako itabaki mfukoni mwako mpaka ufe nayo..!

Ndugu Lucas Mwashambwa, Tundu Lissu ni mtu very genuine sana, jasiri asiye na hofu, husimama kwenye kweli na hamwogopi yeyote kiongozi au binadamu wa gengeni..

Kama kuna ukweli kwenye sababu ulizozitoa hapo kama justification ya hoja yako, basi umekosea sana...

Maana Tundu Lissu hahitaji mwana CCM dizaini yako aseme matatizo ya CHADEMA...

Kama yapo kweli, basi, mwenyewe TL angesema na angesema mchana kweupe huku TV zikirusha hewani statement yake kuwa anaacha siasa au anaondoka CHADEMA na kwenda CCM au chama kingine chochote..

Kama hajasema hivyo yeye, basi WEWE NI MWONGO na mpiga propaganda tu kama wana CCM wengine wanaoihofia na kuiogopa CHADEMA..

Kwa heri🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻
 
Leo umeandika habari ya Lissu kuhama wakati huwa unasema ni mropokaji na hana maana.

Wamekupunguzia posho tena?

Maana ulipunguziwa posho ukanuna hadi ukaacha kuweka namba baada ya kudai unapokea simu tu za watu kukuchora na kila uteuzi hupati.
 
Kama CCM ya wakati wa Jakaya Kikwete ilishindwa kuisambaratisha CHADEMA kwa propaganda za dizaini hii, sijui hii CCM ya "Mama wa Ushungi" na yenye wana propaganda wenye very low profile dizaini ya Lucas Mwashambwa sijui watawezaje kuisambaratisha CHADEMA hii iliyokwisha simika mizizi yake kitaifa na kimataifa kwa utoto huu wa kipumbavu kiasi hiki..!

Na kama hata ile CCM ya John P. Magufuli a.k.a Jiwe iliyokuja na combination ya wa mbinu zote possible kuanzia propaganda za kusifia na kupaka mafuta viongozi wenu, kununua viongozi wa vyama vya upinzani, waliokataa walitekwa, wakateswa, wakatiwa vilema na wengine kuuwawa yote hiyo ikiwa ni mkakati wa aidha kuidhoofisha CHADEMA au kuiondoa kabisa katika suasa za Tanzania, lakini haikuwezekana na badala yake mwasisi na msimamizi wa siasa hizi chafu yaani Rais John P. Magufuli alipotezwa yeye kwa kuuwawa kwa kifo cha kipumbavu kabisa...!

Lucas Mwashambwa mimi naamini humfahamu wala kumjua Tundu Lissu vyema.

Unafikiri Tundu Lissu ni mwanahakarati na mwanasiasa wa mzandiki na mnafiki dizaini ya kina Steven Wassira, Zito Kabwe, Lijualikali, Kangi Lugola, Nape Nnauye au Paul Makonda, NO WAY...HUJUI LOLOTE...

Ndugu Lucas Mwashambwa, Tundu Lissu ni mtu very genuine sana, jasiri asiye na hofu, husimama kwenye kweli na hamwogopi yeyote kiongozi au binadamu wa gengeni..

Kama kuna ukweli kwenye sababu ulizozitoa hapo kma justification ya hoja yako, basi umekosea sana. Maana Tundu Lissu hahitaji mwana CCM dizaini yako aseme matatizo ya CHADEMA. Kama yapo, mwenyewe TL angesema na angesema mchana kweupe kuwa anaacha siasa au anaondoka CHADEMA na kwenda CCM au chama kingine chochote..

Kama hajasema hivyo yeye, basi wewe ni mwongo na mpiga propaganda tu kama wana CCM wengine wanaoihofia na kuiogopa CHADEMA..

Kwa heri🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻
CHADEMA ya enzi za Jakaya ilikuwa na Zitto Kabwe, Dr Slaa, Halima Mdee, Kitila Mkumbo, Marando, na vipaji vingine vya hali ya juu sana sio kama hii ambayo Mdude Nyagali ndo think-tank yenu. CHADEMA ile ya 2011 ilikuwa ya moto mno... vile vichwa vilikuwa hatari kwa kujenga hoja. CHADEMA ya sasa ni takataka.
 
Kama CCM ya wakati wa Jakaya Kikwete ilishindwa kuisambaratisha CHADEMA kwa propaganda za dizaini hii, sijui hii CCM ya "Mama wa Ushungi" na yenye wana propaganda wenye very low profile dizaini ya Lucas Mwashambwa sijui watawezaje kuisambaratisha CHADEMA hii iliyokwisha simika mizizi yake kitaifa na kimataifa kwa utoto huu wa kipumbavu kiasi hiki..!

Na kama hata ile CCM ya John P. Magufuli a.k.a Jiwe iliyokuja na combination ya wa mbinu zote possible kuanzia propaganda za kusifia na kupaka mafuta viongozi wenu, kununua viongozi wa vyama vya upinzani, waliokataa walitekwa, wakateswa, wakatiwa vilema na wengine kuuwawa yote hiyo ikiwa ni mkakati wa aidha kuidhoofisha CHADEMA au kuiondoa kabisa katika suasa za Tanzania, lakini haikuwezekana na badala yake mwasisi na msimamizi wa siasa hizi chafu yaani Rais John P. Magufuli alipotezwa yeye kwa kuuwawa kwa kifo cha kipumbavu kabisa...!

Lucas Mwashambwa mimi naamini humfahamu wala kumjua Tundu Lissu vyema.

Unafikiri Tundu Lissu ni mwanahakarati na mwanasiasa wa mzandiki na mnafiki dizaini ya kina Steven Wassira, Zito Kabwe, Lijualikali, Kangi Lugola, Nape Nnauye au Paul Makonda, NO WAY...HUJUI LOLOTE...

Ndugu Lucas Mwashambwa, Tundu Lissu ni mtu very genuine sana, jasiri asiye na hofu, husimama kwenye kweli na hamwogopi yeyote kiongozi au binadamu wa gengeni..

Kama kuna ukweli kwenye sababu ulizozitoa hapo kma justification ya hoja yako, basi umekosea sana. Maana Tundu Lissu hahitaji mwana CCM dizaini yako aseme matatizo ya CHADEMA. Kama yapo, mwenyewe TL angesema na angesema mchana kweupe kuwa anaacha siasa au anaondoka CHADEMA na kwenda CCM au chama kingine chochote..

Kama hajasema hivyo yeye, basi wewe ni mwongo na mpiga propaganda tu kama wana CCM wengine wanaoihofia na kuiogopa CHADEMA..

Kwa heri🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻
Ningependa kukwambia tu kuwa Lissu hakuanzia siasa zake CHADEMA bali pale ni mhamiaji au wakuja tu.kwa hiyo yeye kuondoka na kuihama CHADEMA ni jambo la kawaida kwake. Kwani wangapi mliokuwa mnawaamini wameondoka CHADEMA? Lissu ndio atakuwa wa kwanza kuondoka? Kwa hiyo unataka aendelee kukaa ndani ya CHADEMA wakati yeye anasema haoni chama kikikata kiu yake ya kutaka mabadiliko mifuko ya kisiasa na kidemokrasia hapa nchini? Unataka abaki wakati anaona mwenyekiti wake kabadilika na hana misimamo inayoeleweka? Hujawahi kumisiki Lissu akipinga hadharani habari za maridhiano?
 
Leo umeandika habari ya Lissu kuhama wakati huwa unasema ni mropokaji na hana maana.

Wamekupunguzia posho tena?

Maana ulipunguziwa posho ukanuna hadi ukaacha kuweka namba baada ya kudai unapokea simu tu za watu kukuchora na kila uteuzi hupati.
Kwani akihama chama ndio ataacha kuropoka kama alikuwa ni mropokaji? Au hujaelewa hoja iliyopo hapa.
 
Sasa mbona wewe unaongelea nafsi ya mtu mwingine.... kama moyo wa mtu kichaka 😀 😀
Ndio maana nimewaleteeni habari ambazo ninyi kwenu ni chungu na hamuamini kama inaweza kutokea.bila kujuwa kuwa Lissu ni mhamiaji na wakuja tu ndani ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom